Kesi ya Mbowe: Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi atajwa kumtumia pesa Mtuhumiwa

Kesi ya Mbowe: Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi atajwa kumtumia pesa Mtuhumiwa

Kama wataonekana Wana interest kwenye kesi!Waziri wa ulinzi kutuma fedha Kwa mtuhumiwa ugaidi si jambo dogo!
Mbaya zaidi taarifa za miamala zimefichwa!
Hapo ndio Kuna mashaka,na ndio interest ya Mwinyi kwenye kesi inapopata mashiko!
Sidhani kama hata hapo amekuelewa

Cc magu2016
 
Kwani Mbowe alituma wakati gani? Unafikiri Mbowe alituma wakati Bwire akiwa ameshitakiwa? Ukiwa neutral utakuta unapata ufahamu sana kwenye haya mambo. Jiweke mbali na huko uliko jing'ang'aniza, uwe huru, huwezi kuwa mzito kuelewa.
Mimi nauliza swali na wewe unaniuliza swali sasa nani atajibu swali langu!!.
 
Kumbe hujapitia hiyo cross examination, kuna miamala 19 ambayo ilifanyika kwa Bwire ikiwemo ya watu ambao barua ya maombi haikuhitaji, ni miamala ya mh. Mwinyi tu ndiyo imeondolewa. Mawakili wa utetezi wameanzia mbali kuhakikisha wanafunga mianya yote kabla ya kufika kwenye hoja ya mh Mwinyi. Labda kama ni mvivu wa kufuatilia au ni mzito kuelewa logic za maswali ya mahakamani.

CcBwana PGO
Asante sana sana kwa kuzidi kufafanua
 
Elewa hoja sasa, kama wanadai Mbowe kutuma pesa ni Ugaidi, kwanini isiwe Ugaidi alipotuma Mwinyi?

Mbona hoja ya wazi kwanini huelewi wewe *zi wa kijani?
Hahahahahaha wanajitoa ufahamu, Maji yamezidi unga
 
Hii kesi inavyokwenda Mawakili wa utetezi wanataka kueleza Kila Jambo lililofanyika sirini na kuwataja wahusika. Lakini pia ulimwengu ulivyo Sasa hakuna binadamu wakumwamini. Taarifa nyingine zinatoka Kwa watu waliopewa Madaraka lakini wana hofu ya MUNGU.

Nikiangalia namna Kigogo 2014 anavyopost Leo najiuliza access ya taarifa imekatikaje Baada ya JPM tu kuondoka? Je, palipokuwa panavuja palizibwa vipi mapema hivyo?

Kwa mfano huu ndipo ninapoamini ukitenda Haki utaheshimika na kulindwa, ukiwakosea watu ambao wanakwenda nyumba za ibada kutubu unazalisha watu ambao toba sahihi nikufichua Yale maovu yanayoendelea yasiendelee au jamii ipige kelele usiendelee kuyafanya

Naomba Serikali iangalie kinachoendelea mahakamani kama kina tija Kwa ustawi wa Serikali na nchi kwa ujumla.

Marais wawili kutajwa kwenye cross examination siyo Jambo dog hata kidogo,
Kigogo ni January Makamba. Hataki kumshambulia Mama. Dogo ana hope kuwa atakuja kuwa Rais wa Tz.
Nimefikia kusema ni Mr. January kwa kuangalia picha za juzi alizo post kigogo (ufagio) aka andika jinsi ya kuongeza wateja ktk biashara yako. Ukiangalia picha zile Graphics zake ni sawa na Zile January aliwahi post ktk Instagram account yake mtu akiwa ndani ya Shimo, akivunja ngazi na kukokea moto. Na damu zina vuja. Huyu ni J. Makamba.
 
Kwa haiba ya Rais Mwinyi kipindi akiwa waziri wa ulinzi sishangai kama kumsaidia mtu anaeyemfahamu kumtumia pesa ikawa ni jambo la ajabu.

Uungwana wake si sababu ya kuona kama alitenda jambo baya na jambo lipo kwa mahakama ngoja niishie hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mboye akituma pesa ni zinakuwa za kufadhili ugaidi

Raisi Mwinyi akituma pesa zinakuwa za msaada

Mwinyi+Hangaya tunawataka mahakamani
 
Back
Top Bottom