Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

Hatari zaidi ya sasa? Hiyo ni kesi ya siasa za kishenzi, aisusie uone kama haijaisha.
Kwani mawakili wasomi wameshindwa kuja na hoja za kumchomoa gaidi mbowe mpaka msuse[emoji23][emoji1787]
 
Wacha ujinga wako Tindo . Mdude aliposhinda Mahakama zilikuwa huru, Sabaya alipohukumiwa miaka 30, Mahakama ziko huru.

Nyinyi mnajuwa uovu wa Mbowe ndiyo maana suruwali zinawabana.

Nasema hivi mahakama haziko huru hilo wala halina mjadala. Mdude alifungwa na mahakama hizo hizo kwa maagizo ya Magufuli, na aliachiwa kwa maagizo ya Samia na sio kwa uhuru wa mahakama. Kama mahakama zingekuwa huru mdude asingefungwa. Sabaya amefungwa kwa ushahidi usioacha shaka, na hata asingefungwa tusingeshangaa maana hakuna mahakama hapa, bali kuna majengo ya kukomolea watu watu walio kinyume cha watawala.

Huyo Sabaya amefungwa maana atakuwa alihitilifiana na mama enzi za Magufuli, vinginevyo kama ni waliotenda uhalifu ndio wanachukuliwa hatua, basi hata Makonda alitakiwa awe jela maana amefanya unyama kuliko wa Sabaya, na ushahidi wa ukatili wake uko wazi.
 
Umetumia vigezo gani kufikiria hivyo mkuu? Maana kama hakuna kilichotokea kwa alichofanyiwa Lissu ndio unategemea kitokee nini kwa kufungwa Mbowe?
 
Nimeshangaa chama ambacho kinaamini katika uhuru wa mahakama kuongea upumbavu huo
 
Ukiwaondoa mawakili ni Mbowe kukaa Kimya bado kama wameamua kumfunga watamfunga tu. Na hao mataga watakuja na hoja kwamba kama siyo kweli si mngepinga? Kwa nini hamkujitetea mbele ya mahakama kama mna hoja? Watasema mlijua kosa lenu ndio maana mlikubali yaishe kwa kunyamaza na kuwaondoa mahakamani. Binafsi naona afadhali hii ya kuendelea kuwa na mawakili na hadi sasa tumeshajua kuwa kumbe Mbowe kabambikiwa kesi na Sirro, Kingai, Mahita, Jumanne na Sabaya . Tungejua wapi kwamba Sirro na wenzake walienda kunywa Mbege kwa yule Kahaba na kisha wakamuomba awe shahidi kwenye kesi ya Mbowe. Tumeyajua mengi mno kwenye hii kesi. Kama kusingekuwapo mawakili tungejuaje hata yule hakimu mteuliwa kuwa huamua kesi kwa maoni yake tu? Acha mawakili waendelee na Mbowe asinyamaze tujue mengi nyuma ya pazia.
 
Hata Mbowe mwenyewe siku hizi hawaamini kivile watu wake aliowatoa mbali ndani ya Chadema. Hawachelewi kumgeuka. Nani alijua haya ya akina Mdee na Covid-19 wenzake, Katambi, Zitto, Waitara, Pauline Gekul, Kitila, Mollel, Selasini, Komu, Bananga, Kalist, Nassari, Silinde, nk. Mbowe aendelee tu na mikakati yake ya kujitetea, hawa wengine ni ndumila kuwili tu
 
Jambo nililolipenda kwenye kesi hii ni kuvuliwa nguo kwa Serikali , Polisi na Majaji .
Na mimi nakuunga mkono. Sote tumejua kuwa Rais na serikali yake na akina Sirro, Mahita, Tigo, Jumane na Kingai hubambika watu kesi. Kauli na hukumu ya Rais kwa Mbowe inaitesa mahakama, Maana mahakama muda wote wanatafuta mwanya wa kuhalalisha Kauli na hukumu ya Rais. Hii Kauli ya Rais itamhukumu hadi mwisho wa maisha yake hapa dunian. Kauli ya kuhujumu haki
 
Sheatani siku zote haeleweki. Wewe mwenyewe unahoji eti kwani Mbowe ana nguvu gani halafu hapohapo unaorodhesha kuchomwa moto sekondari za Kiislamu ukihusisha na Mbowe. Kwani sasa hizo nguvu kapata wapi?
 
A bitter truth, lakini lets give it a try, tukiondoa mawaili wote mahakamani ni dalii ya kukata tamaa na kukubali kosa ambalo mwenyekiti hajafanya, tuache kesi iebdelee ili watu waone uongo wa mamlaka zetu na uonevu wake, mapaka sasa tumeshapata picha ya kesi nzima kutokana na utetezi wa mashahidi wa jamhuri anbao wengi mazungumzo yao hayana direct connection na kesi ya ugaidi bali ni utunzi usio na mtiririko
 
Ulifanya makosa makubwa kuacha kufuatilia hii kesi. Wenzako tumefaidi mengi na tumejua kuwa kumbe hatuna jeshi la polisi bali ni kikundi tu cha wahalifu kilichohalalishiwa kushika bunduki. Tumejua kuwa kumbe eti Mbowe anashitakiwa kwa kutishia maisha ya jambazi Sabaya. Polisi walishirikiana na Sabaya kumfungulia kesi Mbowe.
 
Binge la idea
 
So sad
 
Just look a delusional and frustrated individual spewing rubbish from both sides of the mouth.

If you gat nothing meaningful to say, don't open your mouth and spew trash from both sides.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…