Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

Kitu ambacho Mbowe anatakiwa kukaa nacho mbali kwa sasa na akitoka salama ni ushauri wa Lema na Lissu.

Si ajabu ni ushauri wao ndio uliomfikisha huko alipo na wenyewe washasepa.

Ni watu hao hao walimshauri pia CDM isusie viti maalum bila ya ridhaa ya hakina mama, matokeo yake wakavichukua kwa mlango wa nyuma na kupelekea mgawanyiko.

Kuondoka kwa hakina Halima Mdee kumeacha pengo kubwa sana CDM. Mbowe mahakama ndio itaamua mwisho wa siku. Pamoja na hayo Halima Mdee alikuwa mzuri sana kwenye kutoa pressure serikalini na mhamasishaji yaani hii kesi ya Mbowe angeigeuza ya ukandamizaji wa demokrasia kwa namna yake ya kuleta vurugu huko mahakamani.

Mfano polisi kuwapangisha mstari kuingia ndani ya mahakama au treatment zingine CDM wanazopewa wakienda mahakamani angetumia fursa hiyo kutengeneza mazingira ya uonevu wa polisi na ku associate na kesi yenyewe huku kesha kura virungu kadhaa na nundu za kuonyesha.

Mama juzi alikuwa Glasgow zile picha na wababe wa dunia sio photo shop maana yake huko kwa mabeberu awajali kesi ya Mbowe; sasa akiacha kupigana mwenyewe si anakwenda jela kirahisi bila ya kupambania uhuru wake.
 
Kwani sheria inasemaje, ukiondoa mawakili kesi inasimama au inaendelea?
 
Hizi kauli mlizitoa mwanzoni kabisa wakati amekamatwa toka Mwanza. Mlitakiwa msimamie ule msimamo wa kuisusa kesi badala ya kugeuka vinyonga na kujaza mawakili tele
 
Absolutely true
 
Mawakili wakijitoa na mh. Mbowe akakaa kimya mahakamani manufaa yake yatakuwa nini?
 

Utashangaa sana. Kuna idadi kubwa sana ya Watanzania (hata wenye shule kubwa tu) wa sio na uwezo wa kuona wala kupambanua facts.

Aidha, ni muhimu sana kuweka kumbukumbu yote na sahihi kuthibitisha uovu pasi na shaka. Ikijatokea fursa ya kurejea kesi ili waliohusika na uhuni wote wa wapatilizwe ipasavyo na walioonewa warejeshewe gharama na hadhi zao (full restitution).
 
Point asee
 
Mtu amekaa magereza utarejeshaji? ni uhuni tupu
 
Kwa hiki ulichoandika na alichosema Lema ni TAYARI ujumbe umefika na wanajua kuwa kuna ufuatiliaji mkubwa.Kama hawana plan B ni lazima waiteme kesi!!
 
Kesi iendelee ili tuweke rekodi sawa sawa kwa ajili ya manufaa ya kukobele, hii kesi imeibua mambo mengi sana.
Sure. Kesi iendelee ili iweke rekodi ya uozo kwa vizazi vijavyo. Mana kupitia kesi tumejua polisi wetu walivyo vilaza,majaji wanavotumika. Juzi mmeona clip polisi wanafungia watu ndani ya mahakama kisa wasimuage Mbowe mambo ya upumbavu uliovuka reli.
 
Mkuu 'Salaryslip', ushauri wenu, wewe na Lema sio ushauri mzuri hata kidogo. Ninakubaliana nawe kuhusu zile chaguzi, lakini kwa hapa kwenye hii kesi ya Mbowe sikubaliani nawe.

Sababu ya kutokubaliana nawe ni hii: Hata akisusa, aondoe mawakili kotini, kama wamenuia kumfunga watamfunga tu kwa njia yoyote.

Kuruhusu kesi iendelee, hata kama kutakuwa na mizengwe, kuna faida kubwa ya kuwapa wananchi (mahakama kuu kabisa kuliko mahakama nyingine yoyote) fursa ya kujua bila ya shaka yoyote uwenda wazimu wa serikali. Wao wananchi watapima, na kukiwepo uongozi mzuri wa kuwaongoza huko mbeleni, wataweza kutoa hukumu inayostahili wao wenyewe kwa hao wanaowanyima haki wengine.

Pili, kesi hii kwa kwenda mahakamani imefungua mwanga si hapa nyumbani tu, bali hata kwenye jumuia ya kimataifa nini yanayoendelea hapa nchini. Hawa viongozi unaowaona wakifanya maigizo mengi hapa, usidhani hawataki kusifiwa waonekane kuwa ni watenda haki. Si kila mara unasikia maneno "Utawala Bora" (Good Governance) hayawaishi kutoka midomoni kwao?
Wanamfunga Mbowe, kwa kesi ambayo dunia nzima inajua ni ya kihuni, halafu waendelee kuimba "Good Governance", si wataonekana kama majuha!

Lakini pia usijifanye kusahau mara hii. Hivi Mbowe na wenzake hawakutolewa jela hivi karibuni tu kuhusu ile kesi iliyoondoa maisha ya Kwilina?
Kwa nini mtake kuwarahisishia kazi hawa waovu wanaotunyanyasa sasa hivi?

Kwa ufupi, wewe mkuu 'salary', pamoja na Lema mnataka kuwakingia aibu serikali.
 
Nikuulize swali.

Wewe umo kwenye orodha ya mashahidi upande wa mashtaka?

Utaitwa lini mahakamani kutoa ushahidi wako, maana inaelekea ushahidi ulionao wewe ungekuwa ndio utolewe mwanzoni kabisa mwa kesi hii, lakini hadi sasa haya unayoyaeleza bado hayajawasilishwa mahakamani.

Inakuwaje akina Kingai na wenzake waachiwe kuweka mashtaka yanayoonekana dhahiri kwamba ni ya kutunga tu, halafu wakuache wewe na ushahidi mzito namna hii ambao ungemaliza kesi haraka na kuiacha serikali ikiwa na heshima yake mbele ya wananchi inaowaongoza?
 
Manzoni mlisema Serikali ifute kesi ya Mbowe kukwepa aibu maana haina ushahidi. Sasa mnabadili gia angani Mbowe awaondoe mawakili. Mimi nasema kesi iendelee mpaka mwisho na haki itendeke.

Kesi iendelee; ifike mwisho hata kama haki haitatendeka.
 

Hayati Mkapa aliwahi kusema haamini katika dhana ya upinzani katika nchi za Afrika. Wakati akisuluhisha mgogoro wa Burundi. Ni aina gani ya upinzani unafikiri itatufaa Watanzania? Tanzania tunahitaji upinzani (in the first place) au tumelazimishwa tu?
 
Stop nonsense
 
Dunia is changing at a very fast rate, ya Ken si ya leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…