Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?, ni hoja yenye nguvu. Na kwa kuwa kesi imevuta hisia za watu wengi, wenye nguvu na wa kawida, ndani na nje ya nchi, ni busara kusubiri hukumu. Tofauti na hilo, ni kuitisha mahakama
Serekali ipi unayozungumzia hii hii ya majizi ya kura? Tuna mifano ya kesi nyingi za kubambikia, hata rais huyu alipoingia madarakani alikiri hilo la kesi za kubambikia. Na hayo rais aliyokiri tulikuwa tunasema kuwa ni siasa chafu za Magufuli mkawa mnasema Magufuli ni rais mzalendo. Chanzo cha kesi hii ni Sabaya ambaye yuko jela sasa kwa uhalifu, na hao akina kingai, akina afande Jumanne ambaye sasa kasimamishwa kazi kwa uhalifu aliotenda wakati wa utawala wa kihalifu wa Magufuli.
Kinachoendelea sasa hivi mahakamani ni ushahidi wa kutunga wa kundi la wahalifu toka vyombo vya dola, lengo ni kumkomoa Mbowe kwa maagizo ya rais Samia na genge lake ili asiendelee yeye na chama chake, kuhamasisha upatikanaji wa katiba mpya. Hivyo njia pekee ni kujitoa kwenye huo upuuzi, ili hiyo mahakama itekeleze vizuri agizo la rais na genge lake la kumkomoa Mbowe.