Kesi ya Mbowe: Mbowe na viongozi wa CHADEMA msiposikiliza ushauri wa Godbless Lema anaeshauri muondoe mawakili mahakamani, mtakuja kujiulaumu sana

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?, ni hoja yenye nguvu. Na kwa kuwa kesi imevuta hisia za watu wengi, wenye nguvu na wa kawida, ndani na nje ya nchi, ni busara kusubiri hukumu. Tofauti na hilo, ni kuitisha mahakama

Serekali ipi unayozungumzia hii hii ya majizi ya kura? Tuna mifano ya kesi nyingi za kubambikia, hata rais huyu alipoingia madarakani alikiri hilo la kesi za kubambikia. Na hayo rais aliyokiri tulikuwa tunasema kuwa ni siasa chafu za Magufuli mkawa mnasema Magufuli ni rais mzalendo. Chanzo cha kesi hii ni Sabaya ambaye yuko jela sasa kwa uhalifu, na hao akina kingai, akina afande Jumanne ambaye sasa kasimamishwa kazi kwa uhalifu aliotenda wakati wa utawala wa kihalifu wa Magufuli.

Kinachoendelea sasa hivi mahakamani ni ushahidi wa kutunga wa kundi la wahalifu toka vyombo vya dola, lengo ni kumkomoa Mbowe kwa maagizo ya rais Samia na genge lake ili asiendelee yeye na chama chake, kuhamasisha upatikanaji wa katiba mpya. Hivyo njia pekee ni kujitoa kwenye huo upuuzi, ili hiyo mahakama itekeleze vizuri agizo la rais na genge lake la kumkomoa Mbowe.
 
Serikali siyo wajinga kumfungulia Mbowe kesi ya ugaidi. Mbowe mwenyewe anajuwa namna alivyolikoroga.

Muulizeni kati ya Desemba 2020 na March 2021 mpaka tunamzika DIKTETA Magufuli alikuwa wapi? Muulizeni ni kitu gani aliomba kwenye ubalozi wa Denmark na alijibiwa nini?

Nendeni na ubalozi wa Canada mkaone status ya papers zake kwa alichokiomba. Mmasingizia alikuwa kwenye biashara zake Dubai, ana biashara gani Dubai?

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?

Mbowe alitaka kuweka nchi kwenye status of instability immediately baada ya uchaguzi kukamilika. Serikali ilipogundua njama ndipo akalazimika kukimbia.

Nani kasikia masekondari ya shule za Kisslami yanachomwa tena baada ya Mbowe kuwa mikono salama pale Ukonga?

Na kwa kiasi kikubwa amshukuru Samia ambaye ameacha Mahakama itende haki kwani ingekuwa hajawahi kukimbia nchi wakati wa Mwendazake, saa hizi Mbowe angekuwa na msaidizi wake Ben Saanane huko kuzimu.

Nashangaa Wana CDM mnamtukana Rais SSH eti DIKTETA mwanamke wakati ameacha uhuru wa habari na utawala wa sheria uendelee.
Congenital liar
 
Niwe mkweli tangu mwanzo wa hii kesi na baadae kidogo nikaunganisha alama nikagundua hukumu imeshaandaliwa maana haiwezekani jaji aruhusu kile kinachoitwa kukiri kwa watuhumiwa kuwa yale maelezo waliyolazimishwa kutoa kituoni yaendelee kutumika kama ushahidi ikiwa upande wa utetezi ulimuomba jaji ayatupilie mbali maana hawakusaini kwa ridhaa yao walisaini kwa kuteswa, nami nilifikiri hivyo mapema kuwa Mh Mbowe aondoe mawakili ili jaji amfurahishe ziro na bibi mwanga.
 
Siku chache zilizopita, nilileta mada hapa niki-suggest Mbowe aacha kujitetea mbele ya hizi mahakama zetu kutokana na mwenendo mzima wa hii kesi. Leo hii kupitia You tube, nimemsikia Godbless Lema akimshauri Mbowe aondoe mawakili na akae kimya mahakamani ili wafanye kile wanachokita. Lema pia kaongea na katibu mkuu wa chama na anapanga kuongea na makamu mwenyekiti wa chama kuhusu jambo hili. Isitoshe, Lema kakumbusha uamuzi wa mke wake kutoa mawakili wakati ule wa kesi ya yake alipokuwa ananyimwa dhamana.

Katika kufafanua, Lema kataja mapungufu kadhaa yanayoonekana katika hii kesi na mfano mmojawapo ni Jaji kutumia mawazo yake(opinion) kufanya maamuzi badala ya kutumia vifungu vya sheria katika kuamua mapingamizi. Mbali na kutaja mapungufu yanayojitokeza, Lema anahoji kama katika hatua hizi za mwanzo taratibu zinakikuwa, tunatarajia kweli hukumu itakuwa fair?(swali la msingi sana hili).

Binafsi naungana na Lema kuwa kuna umuhimu wa kuondoa mawakili na Mbowe akae kimya mahakamani tuwaache wafanye wanalotaka kufanya. Hapa tunarudia kosa lilelile la kuwa wagumu kufanya maamuzi kama tulivyofanya kwenye kususia chaguzi zinazoendeshwa na hii tume ya uchaguzi isiokuwa huru. Na hapa niwaambie tu, wakifanikiwa kumfunga Mbowe halafu tukalalamika kuwa taratibu zilikiukwa, majibu yao(MATAGA) yatakuwa mawili: (1) kwanini hamkujitoa (2)Mkakate rufaa kama hamridhiki na maamuzi ya mahakama.

Kuhusu hili la kusubiri kwenda Mahakama ya Rufaa kupinga kitachoamuliwa, naungana pia na Lema kupinga hoja hii kwani hata hao Majaji wa Mahakama ya Rufaa upatikanaji wao ni ule ule wa kuteuliwa na Raisi,hivyo bado lolote linaweza kutokea. Kwahiyo, nashauri viongozi wa CHADEMA na wana familia ya Mbowe watafakari upya kama ni sahihi kuendelea kuweka mawakili mahakamani au Mbowe akae kimya na awaache waamue wanavyoona inafaa.
View attachment 2001948

Ni jambo la afya katika chama kuwa na mawazo tofauti. Hata hivyo tuzingatie zaidi mawazo ya wanasheria wetu akiwamo bwana Lissu kwa sasa.

Ni vizuri tukawa wawazi kwetu wenyewe:

"Neno la mwisho kwenye dhuluma hizi tunalo sisi wenyewe. Siku tukiamua kuyajaza magereza yao itakuwa mwisho."

Tungali na karata bado za kucheza. Twende nao tukiwaumbua kwenye kesi hii hadi mwisho maadam mwisho wenyewe unawezekana uko karibu.
 
Hakuna mtu anaeamini kuwa hii kesi ina uhalali, hivyo wengi watasifu na kupongeza uamuzi huo na labda kusikitika/kulaumu kuwa uamuzi huu umechelewa.

Hata kama Mbowe atafungwa tu NI MUHIMU kesi iendelee na ushahidi utolewe/uhojiwe kwa nguvu na ueledi wote.

Lengo la msingi (primary objective) la kesi za kisiasa si kumuokoa mlengwa na adhabu bali kubainisha uovu unaotendwa na watawala. Kwani kushinda hutegemea maamuzi ya watawala. Hivyo, si jambo la kutarajia sana.

Mbowe akifungwa bila kutumia fursa hiyo kuonyesha uozo wote wa kesi hii itakuwa ni fursa iliyopotea kuweka wazi kwa wananchi na dunia jinsi mambo yalivyo ovyo nchini. Itakuwa hasara kubwa. Unafungwa halafu ukweli unabaki mashakani. Wengine wanaaminishwa kuwa umebwaga manyanga baada ya kuzidiwa na uthibitisho wa mashtaka!
 
Lema mbinafsi sana... YEYE ALIKIMBIA NCHI kwa sababu ya usalama wake leo anamshauri mwenzie aende jela

Unaongea utoto gani dogo? Anamshauri mwenzake aende jela wakati yuko jela tayari?! Hapo alipo anashauri hatua zichukuliwe ili huo uhuni wa kizee wa serikali ukae wazi peupe. Lema alikuwa siku zote hapa nchini, amekimbia kunusuru uhai wake wakati nchi hii ilipokuwa mikononi mwako kiongozi muovu Pombe.
 
Pasipo kujali cheo, madaraka ama hadhi ya mtu aliyokuwanayo, wote siku moja tutapimwa kupitia matendo yetu na kupata hukumu ya haki. Kila mmoja wetu anasimsma katika upande aliiuchagua yeye, upande wa njia ya kweli ama ule wa uovu.

Bwana Yesu Kristo aliwafundisha wanafunzi wake somo zuri sana, ambalo nukuu yake inapatikana katika vitabu vya injili za Mathayo 6:9-13 na Luka 11:2-4.

Sehemu muhimu ya ujumbe uliopo katika kipande kutoka katika hiki cha injili, hutufundisha jinsi ya kumuomba Mungu na Baba yetu aishiye mbinguni. Sehemu lengwa ya tafakari yetu ipo katika sehemu hii; "Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule mwovu”

Watu wa Mungu hujaribiwa na Mungu wao, ndivyo ilivyokuwa kwa Adam na Eva, kwa Abraham na pia hata kwa Kristo mwenyewe alipokuja duniani kwa mara ya kwanza. Ombi la kuepuka kuingia majaribuni linaendana na kipimo cha kutakiwa kuthibitisha imani ya mtu kwa Mola wake.

Ombi la kuhitaji kuokolewa kutoka kwa yule muovu ni njia ya kumuepusha mtu asianguke katika dhambi na hatimaye mauti na kuzimu.

Katika shauri hili la kesi ya ugaidi lipo katika sura halisi iliyopo ndani ya kipande hiki cha injili. Yapo majaribu na zipo hila za yule muovu.

Maamuzi yaliyofanywa na wapangaji wa mashitaka, jaji Siyani katika kesi ndogo, madai ya Rais wetu na IGP Siro, mashahidi upande wa waendesha mashtaka, watuhumiwa, mashahidi upande wa utetezi, mawakili kutoka pande zote mbili, na hata jaji aliyepo hivi sasa. Wote wapo katika mizani ya kweli na haki, wapo katika kipimo mbele ya macho yacMola wao, na pia wakumbuke kuwa kuna siku ambayo i karibu sana, nao watawekwa katika hukumu ili haki yote ikapate kutendeka kwa kila nafsi iliyozaliwa na mwanamke.

Kumbuka, jaribu ni kipimo cha imani yako kwa Mola wako. Lakini ukinasa katika hila zitokanzao na ovu wa shetani, basi umechagua dhambi, mauti na kuzimu, haijalishi cheo wala mamlaka mtu aliyokuwa nayo.
 
Unaamini kwa kuandika propaganda ndefu ndio utatupoteza maboya kwa kinachoendelea huko mahakamani? Huu utoto ulioandika hapa hauendani na ushahidi unaotolewa mpaka sasa mahakamani. Kinachofanyika hivi sasa huko mahakamani ni kupotezeana muda kwa ushahidi wa kulazimisha toka kwa kundi la wahalifu walioko kwenye vyombo vya dola, ili kukidhi matakwa ya siasa chafu. Kufikia Ijumaa ya wiki ijayo, mawakili wachukue hatua za kujiondoa maana ni utoto wa uzeeni unaoendelea kwenye hiyo kesi.
Kwanini sasa mnayoa ushauri wa kutaka kuwaondoa Mawakili na Mbowe asijibu? Mnakaanga samaki kwa mafuta yake.

Majibu mnayo ya ambacho Mbowe ametenda ila mnataka kui FOOL public kuwa anaonewa.

Kama ushahudi ni wa kuunga unga WHY WORRY? Si ndiyo sasa mtamnasua Mbowe kirahisi?

You peolple you have to be matured, Mbowe is a mere suspect like any other person in custody until proven GUILTY by the Court. The more mna doubt rule if law the more mnaonyesha mtu wenu ni mwovu.
 
Hata kama Mbowe atafungwa tu NI MUHIMU kesi iendelee na ushahidi utolewe/uhojiwe kwa nguvu na ueledi wote.

Lengo la msingi (primary objective) la kesi za kisiasa si kumuokoa mlengwa na adhabu bali kubainisha uovu unaotendwa na watawala. Kwani kushinda hutegemea maamuzi ya watawala. Hivyo, si jambo la kutarajia sana.

Mbowe akifungwa bila kutumia fursa hiyo kuonyesha uozo wote wa kesi hii itakuwa ni fursa iliyopotea kuweka wazi kwa wananchi na dunia jinsi mambo yalivyo ovyo nchini. Itakuwa hasara kubwa. Unafungwa halafu ukweli unabaki mashakani. Wengine wanaaminishwa kuwa umebwaga manyanga baada ya kuzidiwa na uthibitisho wa mashtaka!

Huna wazo baya, ila bado unaamini kuna mwananchi mwenye uelewa wa mambo asiyejua utawala wa hila wa watawala hawa, ila anasubiri aonee kwenye kesi hii ya Mbowe? Ushahidi kuwa wananchi wameshaamka ila hofu tu ndio kikwazo ipo kwenye idadi kiduchu ya wapiga kura.
 
Siku chache zilizopita, nilileta mada hapa niki-suggest Mbowe aacha kujitetea mbele ya hizi mahakama zetu kutokana na mwenendo mzima wa hii kesi. Leo hii kupitia You tube, nimemsikia Godbless Lema akimshauri Mbowe aondoe mawakili na akae kimya mahakamani ili wafanye kile wanachokita. Lema pia kaongea na katibu mkuu wa chama na anapanga kuongea na makamu mwenyekiti wa chama kuhusu jambo hili. Isitoshe, Lema kakumbusha uamuzi wa mke wake kutoa mawakili wakati ule wa kesi ya yake alipokuwa ananyimwa dhamana.

Katika kufafanua, Lema kataja mapungufu kadhaa yanayoonekana katika hii kesi na mfano mmojawapo ni Jaji kutumia mawazo yake(opinion) kufanya maamuzi badala ya kutumia vifungu vya sheria katika kuamua mapingamizi. Mbali na kutaja mapungufu yanayojitokeza, Lema anahoji kama katika hatua hizi za mwanzo taratibu zinakikuwa, tunatarajia kweli hukumu itakuwa fair?(swali la msingi sana hili).

Binafsi naungana na Lema kuwa kuna umuhimu wa kuondoa mawakili na Mbowe akae kimya mahakamani tuwaache wafanye wanalotaka kufanya. Hapa tunarudia kosa lilelile la kuwa wagumu kufanya maamuzi kama tulivyofanya kwenye kususia chaguzi zinazoendeshwa na hii tume ya uchaguzi isiokuwa huru. Na hapa niwaambie tu, wakifanikiwa kumfunga Mbowe halafu tukalalamika kuwa taratibu zilikiukwa, majibu yao(MATAGA) yatakuwa mawili: (1) kwanini hamkujitoa (2)Mkakate rufaa kama hamridhiki na maamuzi ya mahakama.

Kuhusu hili la kusubiri kwenda Mahakama ya Rufaa kupinga kitachoamuliwa, naungana pia na Lema kupinga hoja hii kwani hata hao Majaji wa Mahakama ya Rufaa upatikanaji wao ni ule ule wa kuteuliwa na Raisi,hivyo bado lolote linaweza kutokea. Kwahiyo, nashauri viongozi wa CHADEMA na wana familia ya Mbowe watafakari upya kama ni sahihi kuendelea kuweka mawakili mahakamani au Mbowe akae kimya na awaache waamue wanavyoona inafaa.
View attachment 2001948
Salary Slip , Lema na wewe mna mawazo mazuri sana ambayo na mimi nimeyafikiria huko nyuma hata kabla ya kusoma andiko lako na la Lema. Nikajiuliza tena: hawa ni mashetani, azima yao ni kumfunga. Sasa Mbowe akisusia, what next after kususia? Aozee jela (ingawa na hata akimaliza kesi ataozea jela maana wana ushetani wa kumfunga)
Nijibu tafadhali, akisusia, what next ?
(my opinion: Chadema na wapenda haki wote, have a duty to SEEK support from high level International diplomatic mission to exert maximum pressure on the gov to drop this politically motivated and fabricated case

Kwa Mwenendo wa Liganga, ni wazi atamfunga! Court of appeal kuna akina Mugasha and co. Ltd wa huumu ya NEC na MaDED kusimamia uchaguzi, huko nako ni wale wale! Nani bold Judge yuko Court of Appeal? Hakuna kabisa!
 
Serikali siyo wajinga kumfungulia Mbowe kesi ya ugaidi. Mbowe mwenyewe anajuwa namna alivyolikoroga.

Muulizeni kati ya Desemba 2020 na March 2021 mpaka tunamzika DIKTETA Magufuli alikuwa wapi? Muulizeni ni kitu gani aliomba kwenye ubalozi wa Denmark na alijibiwa nini?

Nendeni na ubalozi wa Canada mkaone status ya papers zake kwa alichokiomba. Mmasingizia alikuwa kwenye biashara zake Dubai, ana biashara gani Dubai?

Kwa nini Serikali ihangaike kumtengeneza Mbowe mashtaka ya kubumba? Ni nguvu gani aliyonayo?

Mbowe alitaka kuweka nchi kwenye status of instability immediately baada ya uchaguzi kukamilika. Serikali ilipogundua njama ndipo akalazimika kukimbia.

Nani kasikia masekondari ya shule za Kisslami yanachomwa tena baada ya Mbowe kuwa mikono salama pale Ukonga?

Na kwa kiasi kikubwa amshukuru Samia ambaye ameacha Mahakama itende haki kwani ingekuwa hajawahi kukimbia nchi wakati wa Mwendazake, saa hizi Mbowe angekuwa na msaidizi wake Ben Saanane huko kuzimu.

Nashangaa Wana CDM mnamtukana Rais SSH eti DIKTETA mwanamke wakati ameacha uhuru wa habari na utawala wa sheria uendelee.
Uongouongo haukupeleki popote
 
Kwanini sasa mnayoa ushauri wa kutaka kuwaondoa Mawakili na Mbowe asijibu? Mnakaanga samaki kwa mafuta yake.

Majibu mnayo ya ambacho Mbowe ametenda ila mnataka kui FOOL public kuwa anaonewa.

Kama ushahudi ni wa kuunga unga WHY WORRY? Si ndiyo sasa mtamnasua Mbowe kirahisi?

You peolple you have to be matured, Mbowe is a mere suspect like any other person in custody until proven GUILTY by the Court. The more mna doubt rule if law the more mnaonyesha mtu wenu ni mwovu.

Hizo mahakama zingekuwa huru huu utoto ulioongea hapa ungekuwa na maana. Tunataka mawakili wajitoe ili mumfunge vizuri kwa huo ushahidi wa kipuuzi unaoendelea hapo mahakamani, na jaji kujigeuza sehemu ya ushahidi wa jamuhuri. Hatuna uzoba wa hivyo kwenye jambo la wazi hivyo.
 
Salary Slip , Lema na wewe mna mawazo mazuri sana ambayo na mimi nimeyafikiria huko nyuma hata kabla ya kusoma andiko lako na la Lema. Nikajiuliza tena: hawa ni mashetani, azima yao ni kumfunga. Sasa Mbowe akisusia, what next after kususia? Aozee jela (ingawa na hata akimaliza kesi ataozea jela maana wana ushetani wa kumfunga)
Nijibu tafadhali, akisusia, what next ?
(my opinion: Chadema na wapenda haki wote, have a duty to SEEK support from high level International diplomatic mission to exert maximum pressure on the gov to drop this politically motivated and fabricated case

Kwa Mwenendo wa Liganga, ni wazi atamfunga! Court of appeal kuna akina Mugasha and co. Ltd wa huumu ya NEC na MaDED kusimamia uchaguzi, huko nako ni wale wale! Nani bold Judge yuko Court of Appeal? Hakuna kabisa!
Tuko katika hatua mbaya sana ingawa ndio tunaelekea kupata ukombozi wa kweli. Yote haya lazima yatokee kwanza kabla ya mabadiliko kutokea.
 
Jambo nililolipenda kwenye kesi hii ni kuvuliwa nguo kwa Serikali , Polisi na Majaji .
Naungana na Lema. Wajitoe kwa maelekeZo ya Mbowe, then wandike resume kwanini wamejitoa ambayo itasambazwa dunia nzima clearly showing how the judiciary and gov have already made a judgement. kaeni mlijadili hili....
 
Back
Top Bottom