Kesi ya Uhaini: Amani Golugwa, amemaliza kutoa ushahidi kesi ya Lissu

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 5.

Lissu: Uliulizwa juu ya Mkutano wetu na Shura ya Maimamu.

Kama yale maneno niliyosema kwa Sheikh Ponda au kwa Warioba, neno “tutakinukisha”.

Ukasema hatukusema “tutakinukisha”.

Hebu eleza.

Golugwa: Nilikuwa nasema hali ya kawaida ya flow ya mazungumzo haiwezi kufanana.

Ila muktadha wa mazungumzo ya msingi ulisemwa.

Hilo neno moja kutosemwa halina maana kuondoa ujumbe wa msingi.

---

Lissu: Leo umeulizwa na Wakili Katuga kuhusu ushahidi wako.

Ile picha/rekodi inayochukuliwa na chombo cha habari ni mali ya chombo.

Ukaulizwa utaje sheria au kifungu, ukasema hujui kifungu, ila hivyo ndiyo unavyojua.

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa uhalisi wa ninavyofahamu, kwamba anaye-rekodi amekuja na vifaa vyake.

Inakuwa ni mali yake na chini ya mamlaka yake.

Na mhusika ndiyo anaweza kutumia jinsi anavyotaka, kama kuchapisha na kusambaza.

---

Lissu: Umeulizwa leo kuhusu maneno yafuatayo:

Kama nimesema Majaji ni MaCCM, ukasema sikumbuki.

Kama nimesema Mahakamani hakuendeki, ukasema sikumbuki.

Kama nimesema Polisi wanaingiza kura na vibegi mgongoni, ukasema sikumbuki.

Wewe ukasema nimesema nilichosikia.

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, nilikuwa namaanisha nilichokisema kinatokana na kile nilichokisikia.

Kwa hiyo, mimi nimesema yote kutokana na niliyoyasikia.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6.

Lissu: Kuhusu vurugu za Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Ukasema kweli palikuwa na vurugu.

Na kuhusu Tundu Lissu kuvuruga Uchaguzi Mkuu na uhusika wake, ukasema siyo kweli kwamba Tundu Lissu alikuwa amesababisha hizo vurugu, kwa sababu CHADEMA tulikuwa tumefungiwa na Tundu Lissu alikuwa yupo gerezani.

Golugwa: Baada ya CHADEMA kufungiwa, hatukujihusisha na swala lolote la uchaguzi.

Na Tundu Antipas Lissu alikuwa gerezani/hakuwa kwenye picha ya uchaguzi.

Hivyo, siyo kweli kwamba Tundu Lissu amesababisha vurugu.

Lissu: Uliulizwa kuhusu hotuba ya Jaji Othuman Chande kuhusu vurugu za Uchaguzi Mkuu zilipangwa.

Ukasema hukumbuki.

Ukaulizwa kama Jaji Chande alisema wanasiasa waliwashawishi vijana, ukasema hukumbuki.

Ukaulizwa na Wakili Ajuaye kuhusu uchaguzi kuvurugika.

Ukasema uchaguzi ukivurugika, waliopo madarakani wanaendelea.

Ulikuwa na maana gani?

Golugwa: Katiba yetu inatupa fursa kusogeza uchaguzi mbele.

Maana ya pili ni maana iliyopo katika nia ya ndani iliyopo katika msimamo huu, kwamba CHADEMA ipo tayari hata kwa uchaguzi kusogezwa mbele ili kupata mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Ajuaye ameshachoka anataka zigo liishe.. aende zake vacation kabla gawio halijaisha na zege bado liko saiti 😁
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 7.

Lissu: Na shahidi, umeulizwa tafsiri yako ya kuhamasisha uasi, yalitakiwa kutafsiriwa kwa muktadha wake na yalilenga watia nia.

Ulikuwa una maana gani?

Golugwa: Waheshimiwa Majaji, katika huo Mkutano watia nia walieleweshwa, walionyeshwa hizo sheria mbovu na Katiba.

Na kama kauli ya kisiasa, tunakwenda kinyume na hizi sheria ili kinyume chake tupate sheria nzuri.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, zile dakika 30 zimeishia wapi?

Jaji Ndunguru: Umeziongeza.

Lissu: Basi samahani, Waheshimiwa Majaji. Kama zimeshaisha, naomba niishie hapa.

Jaji Ndunguru: Shahidi, umeshamaliza kutoa ushahidi wako, unaweza ukaenda.

Jaji Ndunguru: Bado break ni saa na nusu.

Lissu: Saa na nusu, Waheshimiwa Majaji? Nahitaji kuongea na mashahidi wangu.

Jaji Ndunguru: Basi tutakutana saa 9 na nusu.

MAJAJI WANATOKA

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Mbona Lissu kamweka Shemeji yake Mwisho kabisa ktk Mashahidi wake lengo kumfanya Heche apate Field ya kujibu au???


Kweli ujinga wangu kukosa Dada mjini 😂😂
 
Wanaume wanaendelea kumenyana misuli
 
Asante sana Manyanza
Bado tuna changamoto ya JamiiForums kuunganisha nyuzi, huyu aliyetoa uzi wake wa kwanza hayupo mahakamani, ameanzisha na kupotea. Mlione hili Moderator
 
View attachment 3665032
Hii ndio T.shirt ambayo Tundu Lissu amesema wamembania asivae

Ujumbe wenyewe: “LISSU — SIXTEEN BULLETS SURVIVOR.” Itakumbukwa leo ni kumbukumbu ya kupigwa kwake risasi mwaka 2017.
Amani Sam Kesi hii iliisha, Mh Rais Samia amuone Ampe hata Wizara moja, ni mtu sahihi, ana uwezo
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

MAHAKAMA IMEREJEA

1. Majaji wa Mahakama Kuu wameingia.
2. Lissu ameshakaa tayari.
3. Mawakili wa Serikali wapo tayari.
4. Watu wote wameshaingia Mahakamani.

Jaji Ndunguru: Tuendelee upande wa mashitaka.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, kwa upande wetu anapungua Nassoro Katuga.

Tupo tayari kuendelea na shahidi wa nne kwa upande wa utetezi.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, na mimi nipo tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru: Shahidi?

Lissu: Shahidi wangu wa nne anaitwa Brenda Jonas Rupia.

Jaji Ndunguru: Shahidi, unaitwa nani?

Brenda: Naitwa Brenda Jonas Rupia.

Jaji Ndunguru: Jina la mwisho ni L au R?

Brenda: R.

Lissu: Brenda as John Rupia au Jonas Rupia?

Jaji Ndunguru: Umri wako?

Brenda: Miaka 34. Tarehe 10 nitakuwa na miaka 35.

Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?

Brenda: Naishi Basihaya, Kata ya Bunju.

Jaji Ndunguru: Unafanya kazi gani?

Brenda: Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi CHADEMA.

Jaji Ndunguru: Dini yako?

Brenda: Mkristo.

Jaji Ndunguru: Utaapa?

Brenda: Mimi Brenda Jonas Rupia ninaapa mbele ya Mahakama hii tukufu kwamba ushahidi nitakaoutoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu; Mungu nisaidie.

Jaji Ndunguru: Unamuongoza au ataendelea mwenyewe?

Lissu: Nikimuachilia mwenyewe ataogelea, halafu meza kuu hiyo inamngojea.

Jaji Ndunguru: Kwani kuna shida gani? (Jaji anacheka.) Utamuongoza shahidi wako.

Lissu: Nitakuuliza maswali, lakini wakati wa kujibu utawaangalia Majaji.

Na vilevile utaongea taratibu, Majaji wanaandika.

Nisikilize mimi na ujibu maswali kwa ku-relax.

Brenda: Sawa.

Lissu: Unasema unaishi Basihaya, Kata ya Bunju, ndiyo wapi?

Brenda: Basihaya, Kata ya Bunju, Mkoa wa Kinondoni, Dar es Salaam.

Lissu: Mkoa?

Brenda: Kwa kichama Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Lissu: Kiserikali hatupo katika chama.

Brenda: Mkoa wa Dar es Salaam.

Lissu: Umesema wewe ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, umeifanya tangu lini?

Brenda: 12 March 2025 nilipoteuliwa na Kamati Kuu ya chama.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kabla ya 12 March 2025, katika chama, ulikuwa nani?

Brenda: Kabla ya tarehe hiyo nilikuwa Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Kichama Kinondoni.

Lissu: Unafikiri Majaji wanaweza kujua BAWACHA ni kitu gani?

Brenda: Waheshimiwa Majaji, BAWACHA ni kifupi cha Baraza la Wanawake CHADEMA.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji hiyo nafasi ya Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Kichama Kinondoni.

Brenda: Waheshimiwa Majaji, nilichaguliwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, 2024.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji nafasi nyingine yoyote uliyowahi kuwa nayo.

Brenda: Waheshimiwa Majaji, nimewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Mwananyamala, Jimbo la Kinondoni.

Na baada ya hapo nimechaguliwa kuwa Katibu wa BAWACHA Jimbo la Kinondoni.

Lissu: Tarehe?

Brenda: Sikumbuki vizuri, lakini ni kuanzia 2015.

Lissu: Sasa shahidi, nje ya chama, hizi nafasi za kichama ulizo nazo na ambazo umekuwa nazo, waeleze Waheshimiwa Majaji professionally wewe ni nani kitaaluma?

Brenda: Kitaaluma nimesomea Bachelor's of Science in Accounting.

Lissu: Chuo gani?

Brenda: University of Gloucestershire.

Lissu: Inatamkwa Shaa au Shaya?

Brenda: Putito Potaro, just like that.

Lissu: Umesomea mwaka gani?

Brenda: 2010 hadi 2013.

Lissu: Ukipata tuzo gani?

Brenda: Nimepata Certificate of Degree in Science and Accounting.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji utaalamu wako mwingine kama unao.

Brenda: Hapana, hakuna.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uzoefu wako wa kazi za kitaaluma nje ya kazi za kisiasa.

Brenda: Mwaka mmoja baada ya kuhitimu chuo nilifanya kazi ya accounting kwa mwaka mmoja.

Baada ya hapo nilianza kufanya biashara.

Lissu: Kazi gani na wapi?

Brenda: Nilipomaliza kazi, nilifanya kazi kwa mwaka mmoja katika kampuni ya TAZ'S CARS kama Accountant wao.

Na baada ya mwaka mmoja nikaacha kazi, nikaanza kufanya kazi Kariakoo.

Lissu: Nataka uwaeleze Majaji kwa fullest details wajue.

Brenda: Mara baada ya kumaliza chuo 2013, nikakaa miezi michache, nikaanza kufanya kazi hadi 2014.

Nikaanza kufanya kazi Kariakoo ya kuuza human hair na baadaye electronics.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 


Iki chama Mashahidi wote wa Jehova
Mana Wate Wakristo Chama cha Wakristo kama sitakosea✍️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…