Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6.

Nassoro Katuga: Ni kweli kwamba falsafa ya “No Reform, No Election” ililenga CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mpaka mabadiliko?

Brenda: Siyo kweli. Msimamo ni “Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi.”

Nassoro Katuga: Nipo sahihi nikisema kwamba CHADEMA haipo tayari kushiriki uchaguzi?

Ni kweli sasa kwamba CHADEMA ilisema “Hakuna mabadiliko, hakutakuwa na uchaguzi”?

Brenda: Si kweli.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama unafahamu uchaguzi ni jambo la kikatiba.

Brenda: Nafahamu.

Nassoro Katuga: Na unajua kwamba Katiba ni mchakato?

Brenda: Nafahamu.

Nassoro Katuga: “No Reform” ilianza lini?

Brenda: 2024.

Brenda: Naomba kurekebisha.

Jaji Ndunguru: Shahidi anaomba kurekebisha.

Nassoro Katuga: Tunaomba kwanza kumuuliza maswali.

Jaji Ndunguru: Shahidi anaweza kurekebisha katika ushahidi wake in chief. Ila katika cross-examination hakuna nafasi ya kurekebisha, labda asubiri re-examination.

Nassoro Katuga: Shahidi, unaweza kueleza kama Mwenyekiti aliwaelekeza namna ipi ya kuzuia uchaguzi?

Brenda: Alielekeza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama alielekeza njia ya kuvuruga uchaguzi.

Brenda: Alielekeza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama alielekeza namna ya kukinukisha.

Brenda: Alielekeza.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako ulisema kwamba kukinukisha ni kupika pilau. Waeleze Waheshimiwa Majaji kama Mwenyekiti alielekeza mpike pilau siku ya uchaguzi.

Brenda: Hakusema tupike pilau.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama katika ushahidi wako wa msingi ulieleza kama alisema aliwaelekeza mkinukishe kwa namna gani.

Brenda: Sikueleza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, katika ushahidi wako uliwaambia Majaji kwamba tutavuruga uchaguzi kwa njia moja, mbili na tatu, kama ulisema?

Brenda: Sikusema.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama Lissu alituambia tufanye ili kuzuia uchaguzi.

Brenda: Sikusema.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 7.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa umesomewa mara kibao kwamba Lissu alisema kwa umma kwa nia ya kutishia Serikali, ni ushahidi muhimu au siyo ushahidi muhimu?

Nassoro Katuga: “Tutazuia uchaguzi” ni sentensi iliyokamilika yenye maana au siyo sentensi yenye maana?

Brenda: Ni sentensi iliyokamilika yenye kuleta maana.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kuchoma vituo vya kupigia kura au kuchoma karatasi za kupigia kura inaweza kuwa ni kitendo cha kuzuia uchaguzi.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kuharibu mali kunaweza kuvuruga amani na hivyo kusababisha kuzuia uchaguzi.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama kukata vidole vya waliopiga kura kunaweza kutishia wengine wasiende kupiga kura na hivyo kuzuia uchaguzi usifanyike.

Brenda: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Kama ulisikia Mwenyekiti akisema kwamba tutafungua kesi Mahakamani kama njia za kisheria?

Brenda: Sikusikia.

Nassoro Katuga: Ulisema CHADEMA inaamini katika demokrasia?

Brenda: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Hivyo, ni haki mtu kushiriki uchaguzi?

Brenda: Ni haki mtu kushiriki uchaguzi huru na wa haki.

Nassoro Katuga: Ni haki kumzuia mtu kushiriki uchaguzi?

Brenda: Siyo haki.

Nassoro Katuga: Ni kosa kisheria na jinai kwa mtu kuhamasisha mtu mwingine kuuzuia uchaguzi?

Brenda: Sijui.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa mtu yeyote aliyesikiliza hotuba, kutafsiri anavyotaka...

Brenda: Ni haki au siyo haki kwa mtu aliyesikia hotuba ya Mwenyekiti kufanya anavyotaka?

Brenda: Ni haki.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, ni haki kwa mtu aliyesikia hotuba ya Mwenyekiti kutenda anavyotaka?

Brenda: Ni haki.

Nassoro Katuga: Unaukumbuka ushahidi wa PW3?

Brenda: PW3 ni kati ya mashahidi ambao sikuwasikia.

Nassoro Katuga: Ni kweli au si kweli hawa G55 walikuwa ni wanachama wa CHADEMA wa wakati ule?

Brenda: Ni wanachama.

Nassoro Katuga: Ni kweli au siyo kweli kwamba mara baada ya wao kujitoa (waria nia) katika msimamo, baada ya kuona huu msimamo una ushirika uasi?

Brenda: Walijitoa na wengine wakabaki.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Brenda kuhusu video alijibu kuwa aliiona lakini alipoulizwa kama mahakamani ililetwa alijibu haikuletwa na prosecution so kupitia ushahidi huo ni wazi kuwa prosecution case has already fallen down long time ago kwasababu ukimuondoa PW 17 wengine wote walieleza kuwa waliona kwenye jambo Tv ambayo video haipo na kwamba hata huyo 17 yeye ndiye aliyeeleza kuwa alichapisha kwenye mtandao wao sasa kwa mazingira hayo ili mahakama ifikie uamuzi ni lazima ijiulize
1. whether the accused published the alleged statement.
2. whether the accused person made statement amounting to treason puersuant to Section 39(2)(d) Penal code cap. 16 R.E. 2023.
Na hapa ndio dhana ya ile video inakuwa muhimu kwani lissu hakatai kutamka maneno hayo lakini anasema yalichukuliwa out of the context kwani maneno yaliyopo kwenye Information ni machache wakati yeye aliongea maneno mengi kwa mukutadha tofauti ndio maana hoja ya lissu ukitaka kujua kuwa yuko smart kila shahidi wake anamuhoji swali kwamba aliongea kwa muda gani ambapo wote wamejibu ni zaidi ya masaa mawili hii ni kumaanisha kwamba video ya Jambo ingekuwepo ndio majaji wangepima dhana mens rea na sio vipande vipande vya kwenye Hati ya mashtaka ambavyo anapowasomea haizidi hata dakika moja wakati yeye aliongea masaa zaidi ya mawili. Mwisho kabisa hata hao mawakili wa Serikali wanapoteza muda tu huku wakijua wameshashindwa kesi na hata ikitokea kwa ujinga akutwa na hatia, hiyo hatia itakuwa kama kesi za akina mbowe ambazo kwenye rufaa ni asubuhi tu kesi anashinda.

NB: Ni kama hivi mtu anasema alinunua shamba na kuandikishana lakini maandishi hajayaleta mahakamani ili kuthibitisha kuwa waliandikishana hivyo hoja ya kwamba alikuwepo kwenye eneo la kuandikishana na alisain inakuwa haina maana yoyote kwasababu maandishi ambayo amesema waliandikishana alipaswa kuyaleta so hata huyo shahidi PW17 aliyerecord na hakuleta recorded video ni sawa na kazi bure maana alipaswa kuileta ili mahakama iamini kuwa kweli kupifanyika publication tofauti na hapo zinabaki story za vijiweni tu.
 
Rupia ni hela kubwa vile heee.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…