Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Yaani mtu anashitakiwa kwa uhaini kwa sababu amesema anaenda kuzuia uchaguzi kwa njia za kidemokrasia
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 19

Tarehe 3 Desemba 2024 tukakaa kutafakari kama CHADEMA, wakati huo mimi sijawa Mwenyekiti wa CHADEMA bado.

Kama wanaua wenyeviti wa vitongoji, uchaguzi Mkuu utakuwaje?

Ndiyo yakazaliwa maneno ya NO REFORMS, NO ELECTION.

Tukasema tutafanyeje? Tukasema tutaenda kwa Watanzania, kwa kila aliye rafiki atusikilize na kila anayetuona adui atusikilize.

Tarehe 10 Desemba 2024, Mwenyekiti Mbowe akatangaza hadharani kupitia waandishi wa habari kuhusu NO REFORMS, NO ELECTION.

Jaji Ndunguru: Tarehe ngapi unasema?

Lissu: Tarehe 10 Desemba 2024.

Tukajiliuza kwenye vikao vya chama, Kamati Kuu, je, utekelezaji utakuwaje?

Tukasema tuna uchaguzi Mkuu wa chama Januari, mwezi ujao.

Tumalize kwanza uchaguzi wa chama, kisha tuwapelekee wajumbe wa Mkutano Mkuu, tupate mandate, halafu tupate mkakati wa utekelezaji.

Waheshimiwa Majaji, tarehe 20 Januari 2025 tukafanya kikao cha Baraza Kuu la chama.

Baraza Kuu la CHADEMA, kwa haraka haraka Waheshimiwa Majaji, ni equivalent ya Halmashauri Kuu ya NEC ya CCM.

Na Kamati Kuu ya CHADEMA ni equivalent ya Kamati Kuu ya CCM.

Na Baraza Kuu ndiyo linatengeneza ajenda ya Mkutano Mkuu.

Kwa hiyo, Kamati Kuu ya tarehe 20 Januari tulipeleka ajenda ya NO REFORM, NO ELECTION ili iende Mkutano Mkuu.

Na ilipita Mkutano Mkuu iwe sera rasmi ya chama.

Na Baraza Kuu la chama likapitisha kwa moyo mmoja NO ELECTION, NO REFORM, na kukubali kuipendekeza kama ajenda katika Mkutano Mkuu uliokuwa unafanyika kesho yake, tarehe 21.

Kwa hiyo, tarehe 21 Januari 2025 kwenye Mkutano Mkuu wa chama yalifanyika mambo mawili:

1. Mkutano Mkuu ulijadili na kupitisha hoja ya NO REFORM, NO ELECTION.

Baraza Kuu jana na Mkutano Mkuu ule, Mwenyekiti alikuwa Freeman Aikael Mbowe, mimi nilikuwa sijachaguliwa.

2. Jambo la pili, tukafanya uchaguzi wa kihistoria ambao haujawahi kutokea Tanzania na nchi yoyote Afrika.

Completely free and transparent election haijawahi kutokea, na tuliita mabalozi waje kushuhudia.

Na mimi nikashinda na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Kwa Katiba yetu, Mwenyekiti anayeshinda anateua Katibu Mkuu, manaibu Katibu Wakuu na Wakurugenzi 5 wa chama.

Kama Mwenyekiti mteule, nilimteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu na Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Na samahani, nilimteua Wakili, sikumbuki vizuri jina, kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Kwa hiyo, baada ya hapo tukaanza kuandaa mkakati wa utekelezaji wa NO REFORM, NO ELECTION.

Tarehe 31 Januari 2025 tukaita Kamati Kuu Bagamoyo, tukapitisha mkakati mkuu wa Bagamoyo.

Kwamba tunaenda kuhamasisha nchi nzima kutumia njia za kidemokrasia.

Njia za kidemokrasia ni maandamano, boycott (kususia), njia za kidemokrasia zinazoruhusiwa na sheria Tanzania.

Tutaenda nchi nzima kutumia njia za kidemokrasia za amani, wala hatukusema tunaenda kumpiga mtu au kuchoma gari ya mtu.

Tunaenda kuhamasisha, na ili umma uhamasike tulisema tutaenda nchi nzima.

Na nchi nzima kwa njia za kidemokrasia za amani.

Lazima tuzungumze na Watanzania kujua hatua katika kuleta mabadiliko.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 20

Lazima tuzungumze na Watanzania katika makundi yao mbalimbali.

Tukatengeneze mkakati wa kuwafuata kwa makundi, kama taasisi za kidini. Tukaenda kuwaona Shura ya Maimamu ya Sheikh Ponda.

Jaji wa Kushoto: Shura au Sura?

Lissu: Shura ya Maimamu. Shura ni neno la Kiarabu, maana yake ni baraza.

Hatukwenda BAKWATA kwa sababu ni CCM.

MAHAKAMA KICHEKO.

Tuliomba kuwaona TEC, lakini hatukuweza kuwaona.

Tuliomba kuwaona Baraza la Wakristo, lakini hatukuonana nao kwa sababu ya muda.

Tukaomba kuwaona Jukwaa la Wahariri na tulionana nao.

Tukaomba kuonana na Tanzania Law Society, na wakatuita Bagamoyo kwenda kuzungumza na Governing Council.

Waheshimiwa Majaji, nchi hii siyo kisiwa. Tukasema tutafute majirani.

Tukamfuata Raila Amolo Odinga, tukamwambia tutakuja kukuona. Una marafiki ndani ya CCM.

Alikuwa rafiki wa karibu wa Magufuli. Tukaenda mimi, Makamu Mwenyekiti Heche na Mjumbe wa Kamati Kuu Lema.

Tukasema tuwaone wazee ambao hawajakata kauli, maana kuna wazee wengi wamekata kauli.

Mzee Warioba bado hajakata kauli, na tulienda kumuona, tukazungumza naye.

Na tuliwaona kila tuliyeweza kumuona, kumueleza.

Na Rais Mseven ana marafiki wengi ndani ya CCM.

Nikaitwa Chuo Kikuu cha Makerere, chuo cha Baba wa Taifa. Mwezi Machi 2025, nikaitwa Chuo Kikuu cha Makerere kwenda kuzungumza kuhusu Legacy ya Mwalimu Nyerere.

Nikaalikwa mkutano mwingine Rwanda, Angola, kwamba tunasikia nyie watu mnataka kususia uchaguzi. Njoo utueleze mbele ya The African Platform of Democracy.

Nikarudi baada ya wiki moja, nikaja kuanza ziara Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kwa mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Rukwa, kuanzia tarehe 21 Machi hadi 30 Machi.

Kuhusu No Reform, No Election, na mipango yetu haikuwa siri.

Hatukuwa tunapanga kuipindua Serikali wala kupanga uhaini, kwa sababu kila kitu tulikuwa tunakifanya hadharani.

Ziara yetu tulimalizia tarehe 31 Machi 2025.

Tukiwa Iringa Mjini kwenye mkutano wa hadhara, Naibu Katibu Mkuu wa chama, Amani Sam Golugwa, sikumbuki kama alipiga simu au alituma ujumbe wa WhatsApp.

Kwamba tumeandaa kikao cha watia nia wetu wote nchi nzima.

Watia nia ni wale ambao tulikuwa tumewahamasisha kugombea uchaguzi Mkuu ujao.

Kwamba tumewaita na kuwahamasisha muda wote na wamejitokeza, na kwa kuwa hatushiriki kwenye uchaguzi tufanyeje?

Tuzungumze na watia nia wote tarehe 3 Aprili 2025 kwenye ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, na nikasema sawa.

Nikasema, kama tumewahamasisha muda wote, ni lazima tuwaeleze.

Mimi na Mheshimiwa John Heche tukamaliza ziara yetu tarehe 31 Machi 2025, na tarehe 1 Aprili tukarudi wote Dar es Salaam.

Na tarehe 3 Aprili, Waheshimiwa Majaji, ndiyo tukafanya huo mkutano na watia nia.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Vyovyote itakavyokuwa utakuwa uking'emuka. Hahaha, tafuta emoji perfect ya mng'emuo ili iwe safi kabisa.
 
Lisu bwana katika ushahidi wake anasema yeye kampambania Mbowe atoke alipokuwa na Kesi ya Ugaidi na hii ni baada ya kuzungumza na Samia.

Ila vijana wake wanamtukana Mbowe anapohudhurua ufunguzi wa bwawa la mwalimu Nyerere.
 
We ndo huna maoni umeanza kuniattack pesonally While
I can smell your hunger,insecurity from hundred miles away
So predictable at your word I know what you gonna say
Hakuna ukwel wowote unaojaribu kueleza since humu ndani si kwa vibwengo wote tupo conscience we smell your intentions even before the court schedule starts
NB:My last reply ndo hii level yangu so ya kuvutana shati na wewe
 
ndio,
endelea kuifanya kazi yako ndugu mtuhumiwa, ili hatimae na majaji nao waendelea kufanya kazi yao ya kutoa haki bila kuwachelewesha kwa porojo ambazo hazikusaidii ๐Ÿ’
Kuna aina tatu ya kujibu maswali kulingana na aina ya swali lenyewe
1.Swali kwa swali
2.Swali kwa maelezo
3.Swali kwa jibu

Tukija kwenye Kesi ya Tundu Lissu lipo hapo kwa Swali kwa maelezo kulingana na kesi yenyewe ni ya kisiasa anachofanya bado ni kuchora mazingira ya hoja kabla ya hajagusa kiini chenyewe ili akija kugusa penyewe inakuwa rahisi kueleweka tofauti na akijibu moja kwa moja
 
Hauoni kuna link kati ya matukio ya nyuma na kinachoendelea sasa. Hawa walianza kumsakama back in a day, subiri bado tupo njiani soon tutafika kwenye point yenyewe.
Kuna picha hapo anatengeneza uone jinsi gani CCM na Serikali yake inavyohodhi mambo kinyume na sheria na hapo kwenye kutengeneza hoja yake Kuna mambo mengi yatafunuliwa kabla ajagusa penyewe kwa kweli yule Mwamba kasoma tuache masihala
 
MaCCM ni majitu ya kiquma na kichoko sana.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA

SEHEMU YA 21.

MAJAJI WANATETA, LISSU ANASUBIRI.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Kwa hiyo, tarehe 3 Aprili 2025 ndiyo tukafanya huo mkutano ambao ndiyo umezaa kesi hii.

Mzungumzaji mkuu ni mimi mwenyewe, na Mwenyekiti wa chama ndiyo kazi yake hiyo, kuelezea msimamo wa chama.

Huwezi kuwa Jenerali halafu katika kuzungumza na watu unatanguliza manahodha.

Uliandaliwa na Ofisi ya Katibu Mkuu, ambaye ndiye mtendaji mkuu.

Mimi nilijulishwa tu na Naibu Katibu Mkuu.

Haya maneno ya kwamba niliandaa mkutano ni kutokujua taratibu za chama, na sikupaswa hata kujibu.

Hawajui kwa sababu hawaulizi, na hawaulizi kwa sababu wanajiona ni watu wakubwa sana.

Nani aliandaa? Kuandaa siyo kazi ya Mwenyekiti.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, ushahidi mlioletewa Mahakamani na mashahidi 17, kuna maneno ambayo ukiyasoma unamaliza dakika.

Mkutano ambao niliongea na watia nia ulikuwa wa zaidi ya masaa 3.

Kwa sababu hata hiyo video ninayodaiwa kuchapisha na Jambo TV, siwezi kusema nilitumia dakika ngapi, kwa sababu hiyo video sijaiona hadi leo hii.

Naweza kusema mbele ya Mungu, mkutano niliozungumza ulikuwa ni mrefu na mkubwa hasa.

Mimi nitayaeleza hapa yote.

Ili mjue, Waheshimiwa Majaji, kama kuna uhaini au ni njia ya kumweka ndani asitusumbue sisi wenye nchi.

Mimi ni mzungumzaji na nitaeleza yote. Mimi nitaeleza kwa sababu ni mzungumzaji.

Mtu akija akisema ni mkutano wa ndani wa masaa matano, anaweza kuwa sahihi; masaa manne anaweza kuwa sahihi, na masaa matatu anaweza kuwa sahihi.

Vyombo vya habari vilikuwa vingi sana, sivikumbuki, na nakumbuka Jambo TV tu kama alivyosema PW16.

Kwa sababu siku ya tarehe 4 Aprili 2025 nilielekea Lindi kwa Baba Askofu Pissa kumueleza mambo yetu yote pale Lindi, na akanipa na Lozari.

Na tukaenda Mtwara.

Tarehe 9 Aprili 2025, saa 12 jioni, nikiwa namalizia mkutano wangu Mbinga Mjini, nilivamiwa na polisi.

Tukapigwa sana na kuumizwa sana. Nikakamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Mbinga, na sikukaa sana, nikapelekwa kwa RPC Songea anaitwa Chilya, namkumbuka sana.

Nikamuambia RPC Chilya, nina njaa sana, siwezi kufika kesho. Na nina mdogo wangu Songea, naomba umpigie aniletee chakula.

Akapiga simu, akaleta chakula mida ya saa 4 usiku, nikala chakula ofisini kwa RPC.

Na RPC Chilya akaniambia, tunakupeleka Dar es Salaam usiku huu huu.

โ€œMaagizo yangu ni kukupeleka Dar es Salaam usiku huu.โ€

Nikamuuliza, โ€œMaagizo kutoka kwa nani?โ€

Akasema, โ€œKutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma.โ€

Dodoma kwa Camilius Wambura na Kingai, wale waleeeee!

(MAHAKAMA INACHEKA)

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Kwelinkabisa mkuu. TAL bado yupo kwenye mstari.
 
Gentleman,
mimi sihitaji kuvutana na mdau yeyeote wa JF kwenye jambo lolote lile la kisiasa au vinginevyo. Members wote wa JF ni kaka, dada, mama, baba, mashangazi, wajomba, ndugu jamaa na marafiki zangu wa mama moja Tanzania.

Gentleman,
hakuna sababu hata moja baina yangu, wewe au mdau mwingine yeyote yule wa JF ya kuhasimiana au kuogopana kwasababu tu ya utofauti wa maoni, mirengo, dini au kabila. To me that's very nonsense.

tutofautiene kadiri inavyowezekana, but at the end tubaki kama ndugu na watoto wa mama Tanzania.

so my friend,
just relax and lets move forward together regardless our differences in opinion on the ongoing case.

i'm sorry for everything,
and plz forgive me gentleman wherever i have wronged or hurts you with my comments
 
Mungu amfanyie wepesi.
 
ok.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ