Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu aendelea kujitetea - Agosti 24, 2026

dalili ya kukata pumzi ni " vibaraka wanaotumiwa na mabwenyenye ya maghariabi" hv nyie machawa hua mnaona wazungu wanatuonea sana wivu sisi kwa KIPI?

shenzi sana
relax gentleman,
ukweli ndivyo ulivyo,

una kera mbaya sana, itabidi uzoee tu :NoGodNo:
 
Sina shida na mshtakiwa, lakini nahisi ingekuwa bora zaidi kutumia jina la hayati katika kujenga hoja nzito. Moja ya kitu ambacho nakishangaa na kinaweza kumpunguza sehemu ya wafuasi na public sympathy ni pale anapomtaja hayati kwa mzaha na kama kejeli hivi. Kwa upande wangu naona hicho kitu si kizuri sana kwa upande wake hata kama alimuumiza kweli.
Ukishakufa Wewe SI kitu, kwenye Biblia muhubiri 9:...Bora mbwa aliyehai kuliko Simba aliyekufa!
 
Gentleman na wewe unaamini hukumu ya kitanzi itapitishwa juu ya huyu mtanganyika?
sheria za nchi ziko wazi kabisa gentleman kwenye hilo,

binafsi naamini Mungu pekee na si vinginevyo.

sheria zifuate mkondo wake na hivyo ndivyo haki inapaswa kutolewa kwa anaestahili:NoGodNo:
 
sheria za nchi ziko wazi kabisa gentleman kwenye hilo,

binafsi naamini Mungu pekee na si vinginevyo.

sheria zifuate mkondo wake na hivyo ndivyo haki inapaswa kutolewa kwa anaestahili:NoGodNo:
Mkondo wake ni kutoka nje!
 
ANAENDELEA TUNDU LISSU

SEHEMU YA 2.

Na kwa pamoja, Tume ya Afrika ilisema Serikali kwa pamoja ina wajibu wa kufuata na kuzingatia Mkataba wa Haki za Binadamu na Wananchi uliouridhia mwaka 1984.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, nilitaka niongeze haya kwa sababu niliona ni muhimu katika masuala haya ya mimi ni nani na kwa nini kesi hii imeletwa.

Sasa leo nataka nizungumze kuhusu mchango wangu wa kupigania haki za binadamu nchini Tanzania.

Ushahidi wa leo utasema ni kwa nini nashitakiwa leo.

Nashitakiwa kwa sababu ya msimamo wangu.

Ni political prosecution kwa sababu ya msimamo wangu katika kupigania haki na utawala bora.

Siyo kwa sababu mimi ni mhaini, bali ni kwa sababu ya kazi niliyoifanya na ninayoendelea kuifanya.

Sasa, kwa kuanzia, Waheshimiwa Majaji, naomba niseme kwamba...

Nimetumia maisha yangu karibu yote ya utu uzima kupigania haki za watu.

Struggle for human rights and struggle for democracy.

Sikuanza juzi.

Sikuanza tarehe 3 Aprili mwaka jana.

Waheshimiwa Majaji, nilianza nikiwa sekondari.

Mwaka 1988 karibu nifukuzwe shule kwa sababu ya kutetea wanafunzi waliokuwa Form 4, na mimi nikiwa Form 6.

Na Majaji katika Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, kuna Majaji niliosoma nao wanafahamu hili, ila sitowataja.

Niliponea chupu-chupu kufukuzwa shule; nilianzia huko.

Mwaka 1990 niliingia Jeshini. Tulikuwa tunaenda Jeshini, siku hizi sijui kama watu wanaenda Jeshini.

Tukiwa Jeshini mwaka 1990, mjadala wa vyama vingi ukaanza.

Waheshimiwa Majaji, majeshi yetu haya, Polisi, JWTZ na Usalama wa Taifa, wote hawa walikuwa CCM.

Na ninaamini bado ni CCM, bado hawajakomboka.

Wote hawa, ulikuwa huingii Jeshini kama huna kadi ya CCM.

Mjadala ulipoanza, ikawa hapana vyama vingi.

Na mimi nilikuwa serviceman, Kikosi namba 841, Itende, Mbeya.

Niligombana na Majenerali wale waliokuwa hawataki vyama vingi na wengine waliokuwa Polisi, akina Mahita.

Niliwaambia kuwa kauli ya Mwalimu Nyerere kwamba wanaopinga vyama vingi ni wajinga. Nyie Majenerali, hamjaisikia? Tena nikiwa serviceman.

Nikagombana nao sanaaaaaa.

Rais Ali Hassan Mwinyi alipoteua Tume ya Mfumo wa Chama Kimoja au Vyama Vingi vya Siasa nchini Tanzania. Inaitwa Tume ya Nyalali kwa sababu Jaji Mkuu Francis Nyalali alikuwa Mwenyekiti wake.
Mkuu,kazi yako imetukuka. Asante kwa update🙏
 
Manyanza Asante kwa kazi bora kbs kwa siku ya leo.🙏
Mungu akubariki sana ndugu Manyanza kwa mtiririko huu usiochosha.
Hakika umefanya kazi njema.

Dereva wangu ameshindwa kujizuia kulia baada ya kufuatilia huu ushahidi wa Lissu.
Alikutana na Lissu Massana Hospital - Mbezi Beach akamuelezea jinsi mdogo wake alivyofanywa huko Nyamongo.

Lissu alimsaidia yule mdogo wake mpaka haki yake ikapatikana, hakutaka kupokea hata senti, ng'ombe wala nini, zaidi ya shukurani ya mdomo na barua.

Anasema Lissu ni mtu wa haki, popote ambapo haki inachezewa, utamkuta Lissu hapo akipigania haki kutendeka.
 
Gentleman,
mimi sihitaji kuvutana na mdau yeyeote wa JF kwenye jambo lolote lile la kisiasa au vinginevyo. Members wote wa JF ni kaka, dada, mama, baba, mashangazi, wajomba, ndugu jamaa na marafiki zangu wa mama moja Tanzania.

Gentleman,
hakuna sababu hata moja baina yangu, wewe au mdau mwingine yeyote yule wa JF ya kuhasimiana au kuogopana kwasababu tu ya utofauti wa maoni, mirengo, dini au kabila. To me that's very nonsense.

tutofautiene kadiri inavyowezekana, but at the end tubaki kama ndugu na watoto wa mama Tanzania.

so my friend,
just relax and lets move forward together regardless our differences in opinion on the ongoing case.

i'm sorry for everything,
and plz forgive me gentleman wherever i have wronged or hurts you with my comments :NoGodNo:
I appreciate you brethren,Umeshow umaturity even to your young brother.
Brother, this is what I believe—I have faith that you are my brother. If we hold together, I believe our warship will never ever be swallowed by the sea
 
Back
Top Bottom