Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu amefanya majumuisho ya mwisho Mahakamani 23/9/2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu amefanya majumuisho ya mwisho Mahakamani 23/9/2026

Angalizo : JamiiForums huu uzi wangu usiunganishwe na uzi wowote, hiyo tabia inakera wateja wenu na maoni ya Wateja wenu yanasomeka kwamba wanavutiwa na uwasilishaji wangu wa updates.

Nawasihi mtuhehimu wateja wenu , msiwe mnajiamulia mambo ambayo wateja wenu hawayataki.

TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 1


WAHESHIMIWA MAJAJI,

Nipo hapa kuwaonyesha kwamba hilo jambo haliwezekani.

Waheshimiwa Majaji, nilikamatwa katika mji wa Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, jioni ya siku ya tarehe 9 Aprili 2025.

Nilichukuliwa nikiwa ninazungumza katika mkutano halali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama ambacho nimekiongoza tangu tarehe 22 Januari 2025.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kukamatwa huko, nilisafirishwa usiku huo huo hadi Dar es Salaam.

Mchana wa kesho yake, tarehe 10 Aprili 2025, nilisomewa mashtaka katika kesi mbili zilizofunguliwa dhidi yangu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Waheshimiwa Majaji, katika kesi ya kwanza nilisomewa shtaka la uhaini, kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Adhabu, Sura ya 16.

Katika kesi ya pili nilisomewa shtaka la kutoa taarifa za uongo, kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act).

Waheshimiwa Majaji, kesi ambayo imenileta mbele yenu leo inatokana na kesi ya kwanza niliyosomewa mashtaka yake Kisutu, yaani shtaka la uhaini.

Baada ya takribani miezi minne na nusu ya mashauri mawili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aliwasilisha taarifa katika Mahakama hii kuhusiana na shtaka hilo la uhaini.

Waheshimiwa Majaji, taarifa yenyewe ina tarehe 12 Agosti 2025.

Taarifa hii inanituhumu kwa mambo yafuatayo:

Kwamba, nikiwa na utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma kuwezesha kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025, kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na nilidhihirisha nia hiyo kwa kitendo changu cha kutamka, kusema na kuchapisha maneno yafuatayo:

«“Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi; ni kweli, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi. Hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha sana sana. Huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga huu uchaguzi kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.”»

Waheshimiwa Majaji, haya ni maneno niliyowasomea ambayo nilisema. Yana kitu kinachoitwa ellipsis (doti doti). Zipo ellipsis nne; kuna ellipsis kabla ya maneno “wanasema” na kuna ellipsis katikati ya maneno haya.

Maana yake ni kwamba kuna maneno ambayo yameondolewa.

Na hilo ni jambo muhimu sana katika hoja zangu za mwisho.

Uthibitisho kwamba kuna maneno yameondolewa ni uwepo wa hizo ellipsis.

Waheshimiwa Majaji, mashtaka tangu mwanzo yanasema kwamba nilifanya kosa hilo katika Wilaya ya Kinondoni mnamo tarehe 3 Aprili 2025.

Wakati wa usikilizwaji wa awali wa kesi hii, mnamo tarehe 22 Septemba mwaka jana, upande wa Mashitaka ulitoa maelezo ya ziada (Additional Information in Support of their Charge).

Waheshimiwa Majaji, kwenye maelezo ya ziada yaliyotolewa wakati wa uwasilishwaji wa awali...
 
SEHEMU YA 2

Waheshimiwa Majaji, upande wa Mashitaka ulidai kwamba mimi ndiye niliyeitisha mkutano wa watia nia wa chama changu mnamo tarehe 3 Aprili 2025, ambapo nilisema hayo maneno.

Kwa madai ya upande wa Mashitaka, mkutano huo uliitishwa na mimi.

Waheshimiwa Majaji, maelezo hayo yapo katika ukurasa wa 131 wa rekodi ya Mahakama.

Waheshimiwa Majaji, upande wa Mashitaka vilevile ulidai kwamba mimi ndiye niliyewaalika waangalizi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo.

Na waandishi wa habari ninaodaiwa kuwaalika walidaiwa kutoka katika vyombo vya habari vifuatavyo: Mwananchi Communications Ltd., Jambo TV na Clouds Media.

Hayo vilevile yapo katika ukurasa wa 131 wa rekodi ya Mahakama, Waheshimiwa Majaji.

Waheshimiwa Majaji, inadaiwa vilevile kwenye hayo maelezo ya ziada kwamba kauli hiyo niliyoitoa katika mkutano huo iliwachochea baadhi ya wananchi wa umma.

Ambao walianza kuhamasishana katika maeneo mbalimbali yaliyotajwa kama Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma, Dar es Salaam na Mbeya.

Na walianza kuhamasishana ili kuzuia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwa kutumia nguvu (through violence).

Na baadhi yao, inadaiwa, walikamatwa na askari Polisi wakati wakitekeleza maelekezo yangu.

Waheshimiwa Majaji, hayo yapo katika ukurasa wa 132 wa rekodi ya Mahakama.

Waheshimiwa Majaji, maelezo ya ziada ya mwisho yanasema kwamba kauli hiyo niliyoitoa katika mkutano wa tarehe 3 Aprili ilikuwa ni kitendo cha uhalifu (amounted to a criminal offense).

Na matendo hayo yaliripotiwa kwa Afisa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (Zonal Crime Officer).

Waheshimiwa Majaji, kuna kitu nimekisahau kwenye hayo maelezo ya ziada.

Inadaiwa kwamba hayo maneno niliyoyasema kwenye mkutano niliyachapisha mwenyewe kwenye chombo cha habari kinachoitwa Jambo TV, na yalirushwa moja kwa moja kwa umma na chombo hicho.

Waheshimiwa Majaji, taarifa iliyowasilishwa Mahakamani pamoja na maelezo ya ziada ya Mashitaka niliyoyasema ndiyo kiini cha kesi hii.

They are the centre of this case.

Na Waheshimiwa Majaji, kwa vile yapo katikati ya huu mgogoro, hoja zangu za leo na pengine kesho zinahusu taarifa hii ya ziada na ushahidi ulioletwa.

Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na tuhuma hizi na kwenye maelezo ya ziada:

“With regards to the Information, the allegations and additional particulars given at the preliminary, I have the initial comment.”

Kauli yangu ya kwanza, Waheshimiwa Majaji, sijawahi kuficha wala kukana kusema maneno niliyowahi kuyasema.

Waheshimiwa Majaji, ukiangalia ukurasa wa 97 wa rekodi ya Mahakama ya Ukabidhi Kisutu, tarehe 18 Agosti mwaka jana, niliiambia Mahakama maneno yafuatayo:

“It’s true I stated those words in an open meeting. The issue is whether those words amount to treason.”

Swala siyo nilisema au sikusema.

Swala ni je, hayo maneno yanatengeneza uhaini?

“I did not say those words just once, but I repeated them at Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Lindi and Mtwara, according to the committal records.”

Nikaendelea kusema:

Hayo maneno ya kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 hayajawahi kuwa siri.

Nikasema:

“The question is: do these words constitute treason or any other offence?”

Je, maneno haya yanatengeneza kosa la uhaini au kosa lingine la jinai?

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wangu wote, pamoja na mimi hapo kizimbani, chini ya kiapo wamesema kwamba maneno hayo yametolewa sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Haijawahi kuwa siri.

Waheshimiwa Majaji, kauli yangu ya pili ya awali ni kwamba utetezi wangu (my defence has never been that I am ashamed of what I have said).

Haijawahi kuwa utetezi wangu kwamba naona haya au aibu kusema haya maneno.

Utetezi wangu siku zote ni kwamba nilichokisema siyo uhaini.

Na siyo kosa lolote la jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
 
SEHEMU YA 3

Waheshimiwa Majaji,

Sasa baada ya kueleza sheria inavyosema, swali muhimu ni hili:

Upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kila kipengele cha kosa hili kwa ushahidi gani?

Kwa sababu siyo kila ushahidi unaowasilishwa Mahakamani unathibitisha kosa linaloshtakiwa.

Kosa hili lina vipengele maalumu. Na kila kipengele lazima kiunganishwe na ushahidi wa kutosha.

Jambo la kwanza ni allegiance, yaani utii kwa Jamhuri ya Muungano.

Kwanza, sheria inaanza na mtu ambaye yuko chini ya allegiance kwa Jamhuri ya Muungano.

Hili si jambo la kupuuzwa.

Mahakama inapaswa kujiuliza: Je, upande wa mashtaka umeonyesha kwa ushahidi kwamba kipengele hiki kimetimizwa?

Ikiwa ni jambo lisilopingika kwamba mshtakiwa ni raia wa Tanzania, basi suala linalofuata ni kama vipengele vingine vya kosa vimeonyeshwa kwa kiwango kinachotakiwa na sheria.

Jambo la pili ni nia inayotakiwa na sheria.

Waheshimiwa Majaji, hapa ndipo kiini cha kesi hii kilipo.

Kifungu cha 39(2)(d) hakisemi tu kwamba mtu amesema jambo fulani.

Kinazungumzia mtu ambaye anaunda nia ya kusababisha au kuhamasisha mtu au kundi la watu kutekeleza lengo lililotajwa katika kifungu hicho, na kisha anaonyesha nia hiyo kwa maandishi, uchapishaji au kitendo cha wazi.

Kwa hiyo, Mahakama inapaswa kutenganisha mambo mawili.

Kwanza, maneno yaliyosemwa.

Pili, nia ambayo sheria inataka ithibitishwe.

Maneno yanaweza kuthibitishwa kwamba yalisemwa. Lakini swali la kisheria ni: Maneno hayo yanaonyesha nia gani?

Na zaidi, je, yanaonyesha nia mahsusi inayotakiwa na kifungu cha 39(2)(d)?

Jambo la tatu ni kitu kilichokusudiwa kutokea.

Waheshimiwa Majaji, lazima kuwe na jibu la wazi kuhusu swali hili:

Mshtakiwa alikusudia nini kitokee?

Upande wa mashtaka unasema kulikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025.

Lakini Mahakama lazima itenganishe nia ya kutaka uchaguzi usifanyike, nia ya kutaka mabadiliko ya kisiasa, nia ya kushinikiza Serikali, nia ya kuhamasisha maandamano, nia ya kuhamasisha uasi na nia mahsusi inayotakiwa na kifungu cha 39(2)(d), ya kutishia Executive, Legislature au Judiciary.

Si kila moja ya mambo hayo ni kitu kimoja kisheria.

Kwa hiyo, swali si tu kama maneno yalitamkwa.

Swali ni kama upande wa mashtaka umeonyesha uhusiano wa moja kwa moja kati ya maneno hayo na nia mahsusi inayounda kosa chini ya kifungu cha 39(2)(d).

Jambo la nne ni nani aliyetishiwa.

Waheshimiwa Majaji, kifungu kinataja taasisi maalumu: Executive, Legislature au Judiciary.

Kwa hiyo, Mahakama inapaswa kujiuliza:

Ni taasisi ipi hasa iliyokusudiwa kutishiwa?

Na kitendo gani hasa kilikuwa tishio dhidi ya taasisi hiyo?

Ikiwa jibu ni Serikali, basi ni lazima ionyeshwe ni kwa namna gani kitendo hicho kilifikia kiwango cha intimidation kinachotakiwa na kifungu.

Ikiwa ni Bunge, ni lazima lionyeshwe.

Ikiwa ni Mahakama, ni lazima lionyeshwe.

Hatuwezi kuchukua neno moja au sentensi moja na kuliondoa kwenye mazingira yake bila kuonyesha uhusiano wake na kipengele cha kosa.

Jambo la tano ni kwamba masharti ya kifungu hayaishii kwenye maneno.

Waheshimiwa Majaji, kifungu cha 39(2)(d) kinahitaji nia hiyo idhihirishwe kwa kuchapisha maandishi, uchapishaji au overt act or deed whatsoever.

Kwa hiyo, ushahidi kuhusu video, maandishi, machapisho ya mitandao ya kijamii au hotuba haupaswi kuangaliwa tu kwa swali la:

Je, mshtakiwa alisema haya?

Bali:

Je, chapisho au kitendo hicho kinaonyesha nia mahsusi inayotakiwa na kifungu cha 39(2)(d)?

Hapo ndipo tofauti kati ya ushahidi wa tukio na ushahidi unaothibitisha kila kipengele cha kosa inapojitokeza.

Kuhusu mashahidi 17 wa upande wa mashtaka, Waheshimiwa Majaji, upande wa mashtaka uliita mashahidi 17 na kuwasilisha vielelezo mbalimbali.

Lakini idadi ya mashahidi si kipimo cha kama kosa limethibitishwa.

Mashahidi 17 hawawezi kuchukua nafasi ya kipengele cha sheria ambacho hakijathibitishwa.

Mahakama inapaswa kuangalia kila shahidi kwa swali hili:

Ushahidi wa shahidi huyu unathibitisha kipengele gani cha kosa?

Ikiwa shahidi anathibitisha tu kwamba mkutano ulifanyika, hilo halitoshi peke yake kuthibitisha treason.

Ikiwa shahidi anathibitisha kwamba hotuba ilitolewa, hilo peke yake halitoshi.

Ikiwa shahidi anathibitisha kwamba video ilirekodiwa, hilo peke yake halitoshi.

Ikiwa shahidi anathibitisha kwamba video ilichapishwa mtandaoni, bado Mahakama inapaswa kujiuliza:

Chapisho hilo linaonyesha nia mahsusi inayotakiwa na kifungu cha 39(2)(d)?

Waheshimiwa Majaji, kuna tofauti kati ya shahidi anayesema “Niliona au nilisikia” na ushahidi unaothibitisha “Hiki ndicho kilichokusudiwa kisheria.”

Mahakama ndiyo yenye jukumu la kutafsiri ushahidi huo kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo, ushahidi wa mashahidi kuhusu mazingira ya kisiasa, uchaguzi, mikutano ya CHADEMA, machapisho ya mitandao ya kijamii au kauli zilizotolewa lazima hatimaye uunganishwe na kipengele mahsusi cha kosa.

Kuhusu kauli ya tarehe 3 Aprili 2025, Waheshimiwa Majaji, upande wa mashtaka umejenga sehemu kubwa ya kesi yake kuzunguka kauli zinazodaiwa kutolewa tarehe 3 Aprili 2025 katika mkutano wa CHADEMA.

Lakini Mahakama haipaswi kuishia kwenye swali la kama kauli hizo zilitolewa.

Inapaswa kujiuliza:

Kauli hizo, zikisomwa kwa ukamilifu na katika mazingira yake, zinathibitisha kila kipengele cha kosa linalodaiwa?

Na hasa:

Zinaonyesha nia ya kutisha Executive, Legislature au Judiciary kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 39(2)(d)?

Waheshimiwa Majaji, maneno hayawezi kutenganishwa na mazingira ambayo yalitamkwa.

Ikiwa ushahidi unaonyesha kwamba kulikuwa na mjadala kuhusu uchaguzi, marekebisho ya uchaguzi, Katiba, maandamano au shinikizo la kisiasa, Mahakama inapaswa kuangalia mazingira hayo yote.

Hii si kusema kwamba mazingira hayo yanaondoa moja kwa moja kosa.

Bali hoja ni kwamba mazingira hayo yanaweza kuwa muhimu katika kuamua nia ya mshtakiwa ilikuwa nini.

Na hilo ndilo jambo ambalo kifungu cha 39(2)(d) kinahitaji Mahakama ilitathmini.

Waheshimiwa Majaji, baada ya mashahidi 17 kusikilizwa, swali si:

Je, Serikali imeleta mashahidi wengi?

Swali sahihi ni:

Je, ushahidi wao, kwa pamoja na kila mmoja kwa nafasi yake, umeprove kila ingredient ya offence beyond reasonable doubt?

Kwa sababu kama kuna kipengele kimoja muhimu ambacho hakijathibitishwa, basi wingi wa mashahidi hauwezi kuziba pengo hilo.

Na kama ushahidi wa mashahidi 17 unaonyesha kwamba maneno yalitamkwa lakini hauonyeshi nia mahsusi inayotakiwa na kifungu cha 39(2)(d), basi Mahakama lazima itenganishe kati ya kitendo kilichothibitishwa na kosa linalotakiwa kuthibitishwa.

Waheshimiwa Majaji, msingi wa utetezi wangu ni huu:

Kesi hii haipaswi kuamuliwa kwa kuangalia ukubwa wa ushahidi, bali ubora wa ushahidi katika kuthibitisha kila kipengele cha kosa.

Si idadi ya mashahidi inayounda kosa.

Si idadi ya vielelezo inayounda kosa.

Ni sheria na ushahidi unaokidhi kila kipengele cha sheria.

Na pale ambapo kipengele cha kosa hakijathibitishwa, haiwezekani kukamilisha kosa kwa kuunganisha ushahidi usiohusika moja kwa moja na kipengele hicho.

Ndiyo maana, baada ya kupitia mashahidi 17 na vielelezo vilivyowasilishwa na upande wa mashtaka, hoja yangu ni kwamba Mahakama inapaswa kujiuliza kwa kila kipengele:

Where is the evidence?

What element of the offence does this evidence prove?

Na mwisho:

Has that element been proved beyond reasonable doubt?

Hapo ndipo Mahakama itakapoweza kuamua kama ushahidi uliopo unathibitisha kosa linaloshtakiwa chini ya kifungu cha 39(2)(d).
 
SEHEMU YA 4.

Hili ambalo nimezungumza sasa hivi halikuzungumzwa kabisa katika kesi ya Grey Kungu Matata wala Khatibu Gandi.

Katika kesi hii, Mahakama lazima ilitolee uamuzi.

Ndiyo maana nilisema, njia yoyote mtakayoichagua itaandika historia na kuweka sheria.

Utaratibu upoje watu wengine wanapokuwa wanachochewa kufanya makosa?

Ni lazima Mahakama Kuu ijadili na kutoa mwongozo.

Kwa vyovyote vile, Mahakama yenu itakuwa imetengeneza sheria.

Uzito wake si kuwa na hatia au kutokuwa na hatia kwa mtu mmoja. Hapana. Uzito wake ni kutunga sheria na kutoa mwongozo.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kuweka hizo parameters, naomba sasa nipendekeze kwenu masuala ambayo mnatakiwa myatolee uamuzi, na yote yanatokana na maelezo ya ziada na sheria.

La kwanza ni kama Mshtakiwa aliitisha mkutano wa tarehe 03 Aprili, kama inavyodaiwa.

La pili ni kama Mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari katika mkutano wa tarehe 03 Aprili 2025, kama inavyodaiwa.

La tatu: Kama Mshtakiwa alitengeneza nia kwa mtu au kikundi kuhamasisha/kuchochea mtu au kikundi kuzuia Uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kutishia Serikali.

La nne: Ni kama maneno ambayo anadaiwa/kutuhumiwa kuyaongea Mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote linalojulikana na sheria za Tanzania.

Na kama jibu ni ndiyo, ni kosa la uhaini?

La tano: Kama maneno yanayodaiwa kuzungumzwa na Mshtakiwa yanatengeneza matendo chini ya sheria ya uhaini.

Namba 6: Ni kama Mshtakiwa alichapisha hayo maneno katika mtandao wa Jambo TV, kama inavyodaiwa.

Namba 7: Ni kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika na maneno yanayodaiwa ya kihaini.

Namba 8: Ni kama upande wa mashtaka umedhibitisha mashtaka yao kwa mujibu wa viwango vinavyotakiwa na sheria.

Namba 9: Ni hukumu gani Mahakama ifanye baada ya kupata majibu ya masuala hayo namba 1 hadi 8 niliyoyasema hapo juu.

Waheshimiwa Majaji, katika tafakari yenu kuhusu ushahidi ambao upo katika rekodi, nawaalikeni muongozwe na kanuni kuu zifuatazo za sheria.

Ni hizi zifuatazo:

Kanuni ya kwanza: Sheria zinazotoa adhabu zinatakiwa kutafsiriwa kwa umakini mkubwa.

Kanuni za kutafsiri jinai haziwezi kufanana na kanuni za kutafsiri madai, na zinatafsiriwa kwa upendeleo wa Mshtakiwa.

Hii inapatikana katika kesi maarufu ya Regs Vs Mwanangomeni, ukurasa wa 134 na 135.

Pili, Amin S/o Mrisho Vs Republic, 1971.

Tatu, Issa Hassan Uki Vs Republic, Criminal Appeal Number 129 of 2017, Mtwara, ukurasa wa 23.

Hizo zote, Waheshimiwa Majaji, zina-support kwamba sheria za jinai zinatakiwa kutafsiriwa kwa faida ya Mshtakiwa.

Kanuni ya pili: Haya yanayoitwa makosa, ukiambiwa umefanya makosa, umefanya matendo yanayokatazwa na sheria, na kama hayajakatazwa na sheria siyo kosa.

Msingi wa kanuni hii upo kwenye Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mtu hawezi kuadhibiwa kwa kitendo ambacho siyo kosa wakati anafanya.

Pia ipo katika Section 5 of the Penal Code.

Order 1 of Paragraph 5 ya General Police Orders za mwaka 2021 inasema kwamba makosa ni yale yanayokatazwa na sheria tu.

Pia ipo katika kesi ya Bahame Sitta na Wenzake Vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 166 of 2019, Court of Appeal at Shinyanga, tarehe 11 Novemba 2022, ukurasa wa 13 na 14.

Hizo ndiyo Principle of Legality.

Kama hakijakatazwa na sheria, siyo kosa.

Kanuni kuu ya tatu: He who alleges must prove.

Anayetoa tuhuma lazima azithibitishe.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
SEHEMU YA 5.

Waheshimiwa Majaji, Kanuni hii ipo katika kifungu cha 117 cha Sheria ya Ushahidi.

Anayeshitaki ana wajibu wa kuthibitisha, na anaye shitakiwa hana wajibu wa kuthibitisha chochote.

Kanuni Kuu ya 4: Ni kwamba, the standard of proof required in a criminal case is beyond reasonable doubt.

Kanuni hii ipo katika kifungu cha 2(3)(a) cha Sheria ya Ushahidi.

(Waheshimiwa Majaji, hii inatakiwa kuwa namba 5.)

Kanuni namba 4: In a criminal case, the burden of proof is the burden of the prosecution and it never shifts.

Ili kuunga mkono kanuni hii, napendekeza kwenu kesi ya Oscar Lwela Vs Jamhuri of 2013, Court of Appeal, Mbeya, 21 June 2013, page 13.

Waheshimiwa Majaji, Kanuni Kuu ya 6 ni kwamba evidence must be assessed cumulatively and as a whole rather than examining each piece of evidence separately.

Kanuni hii mtaikuta katika kesi ya Oscar Lwela ambayo nimeshaitaja.

Nguva Vikings (Babu Seya) na Wenzake Vs Republic, Criminal Appeal Number 56 of 2005. Ipo reported in 2010 TZCA 191.

Kanuni Kuu ya 7: A conviction in a criminal case must be based on the strength of the prosecution case and not on the defence case.

Ili mtu apatikane na hatia, anatakiwa apatikane kwa uimara wa upande wa Mashitaka.

Hii mtaikuta katika kesi ya Babu Seya niliyoitaja.

Kesi ya Mohamed Vs Republic, Criminal Appeal Number 25 of 2005, Court of Appeal, Dar es Salaam.

Kesi ya Vitalis Joseph Vs Republic, Criminal Appeal Number 384 of 2021, Court of Appeal.

Waheshimiwa Majaji, Kanuni Kuu ya Nane inasema hivi:

When prosecution witnesses give contradictory evidence on a crucial point, its effect is to render the prosecution's evidence all unreliable.

Pale upande wa Mashitaka unapotoa ushahidi unaojichanganya katika upande muhimu, matokeo yake ni kuufanya ushahidi wa Mashitaka kuwa hauaminiki.

Mtaikuta kwenye kesi ya Makonyo John (Kibuna) and Two Others Vs Republic, Criminal Appeal Number 305 of 2018, Court of Appeal Mwanza, 13 May 2022, at page 26.

Kuna kesi nyingine ya Khamis Said Adam Vs Republic, Criminal Appeal Number 529 of 2016, Court of Appeal of Arusha, 11 December 2018, page 11.

Kuna kesi ya Maramo Slaa Hofu and Three Others Vs Republic, Criminal Appeal Number 246 of 2011, Court of Appeal Arusha.

Kesi nyingine maarufu ni Mohamed Matula Vs Republic (1995) TLR 3.

Waheshimiwa Majaji, Kanuni Kuu ya 9 inasema hivi:

Particulars of a charge must disclose the ingredients.

Maelezo ya shtaka lazima yaonyeshe viini muhimu vya shtaka.

Na pale ambapo shtaka linahitaji mazingira ya kiushahidi ambayo, yasipokuwepo, kosa halifanyiki, basi hizo factual circumstances lazima ziwepo na must be disclosed.

Ipo katika kesi ya Isdory Patrice Vs Republic, Criminal Appeal Number 224 of 2007, Court of Appeal of Arusha, 13 October 2007, page 14.
 
SEHEMU YA 6.

Waheshimiwa Majaji, hizi Kanuni 3 ni za Uhaini.

Kanuni ya Kwanza ni kuhusu Uchapishaji — Publication under Section 39(2).

Means the act of sending out or sharing or printing.

Haina maana ya kitu kingine chochote zaidi ya hii. Picha na video siyo publication.

Ipo katika kesi ya Grey Kungu Mataka and Others Vs Republic (1971), Vol. 1 EA 4795, ipo katika pages 5 to 10.

Kuchapisha maana yake ni kubadilishana makaratasi.

Waheshimiwa Majaji, Kanuni ya Pili kuhusu Uhaini:

Inasema hivi: A conviction on a charge of treason requires a proof of covert act or deed.

Inasema inahitaji kuthibitishwa kwa kitendo cha wazi na siyo maneno.

Ipo katika kesi ya Khatibu Ghandi na Wenzake Vs Republic (1996) TLR 12, page 12.

Kanuni ya Tatu na ya mwisho inayohusu Uhaini inahusu maneno.

Inasema maneno matupu hayatengenezi kitendo cha wazi katika kesi ya Uhaini, isipokuwa kama hayo maneno yanaelezea matendo ya Uhaini.

Ipo katika Khatibu Ghandi, page 65.

Na ya mwisho inahusu maneno vilevile:

The position that, as a general rule, words do not constitute covert act or deed applies to treason to individual persons.

Khatibu Ghandi, page 67.

Kwa maneno mengine, maneno ya mtu mmoja aliyeshitakiwa peke yake hayawezi kuwa Uhaini.

Waheshimiwa Majaji, hizo ni Kanuni 3 ziwaongoze katika ushahidi wa kesi hii.

Naomba sasa, kwa ruhusa yenu, nianze kujiongoza katika maswali ambayo niliyaendeleza.

Nifanye analysis ya ushahidi sasa.

Nianze na: Je, mshtakiwa ndiye aliyeitisha mkutano wa tarehe 03 April 2025?

Swala la nani aliyeitisha huo mkutano.

Waheshimiwa Majaji, kwenye ukurasa wa 131 wa rekodi, imedaiwa na upande wa Mashitaka kwamba mnamo tarehe 03 April 2025, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa CHADEMA, niliitisha mkutano wa watia nia wa uchaguzi wa 2025.

Waheshimiwa Majaji, kwanza, kwa nini hii issue ni muhimu?

Kwa nini swala la nani aliyeitisha mkutano ni muhimu kwenye kesi hii?

Waheshimiwa Majaji, kwenye Kifungu cha 49 cha Kanuni ya Adhabu:

Kinasema: Kila kitendo kinachofanyika ili kuwezesha lengo la kutenda kosa kinahesabika kuwa ni tendo la wazi linalothibitisha kutenda hiyo nia.

Kuitisha mkutano maana yake ni kwamba watakuja kusema that is a covert act — ni kuthibitisha nia yake ya kutenda Uhaini.
 
Back
Top Bottom