Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Ndugai alimuondoa lissu bungeni eti kwa sababu ya utolo kipindi wote wanajua kuwa anaumwa wakti hule and at the same time walijadili bungeni kuhusu kupigwa risasi kwa lissu, nchi imepitiq ujinga mwingi hii.
 
Naona wazi Mawakili wa serikali, wametumia kila mbinu kumchochea shahidi wao Lissu, ili apaniki ila wameshindwa. Sasa huyo Wakili wa pili, ameona ili afaulu hilo, atumie kigezo cha kumuingiza TL na ishu ya kupigwa risasi, akijua wazi atamprovoke kwa maumivu ili akose reasoning.

Sasa hizi ni mbinu za kizamani na ni utopian kwenye uwakili wa kileo. Lengo hapo wakili anataka mtengenezea TL, "Psychological torture" kumfanya Lissu, apunguze au atoke kwenye utulivu, ambao naona mpaka sasa haujapungua.

Kuhusu kesi: Kwa kuwa TL ni shahidi, badae TL, ataruhusiwa kujibu, maeneo yenye ukakasi (kama yatakuwepo).

Hasara za TL kuwa shahidi na mshitakiwa: TL ni shahidi na pia mshitakiwa, hivyo anakosa fursa ya kupinga maswali (Objection) hata kama yanamuumiza, nategemea majaji wanaweza kufanya hivyo kwa niaba yake kwama watataka kuwa fair. Tutarajie hawa jamaa kumhoji TL kwa muda mrefu sana na kwa mbinu nyingi, sababu wana faida moja; TL hawezi fanya "objection" ataanza kuifanya kwa mashahidi wanaofuta baada ya yeye.

Sababu hawezi fanya kazi mbili, na pia kuna maswali anaweza kuulizwa (yanayohitaji objection), kwakuwa ndio anayeyajibu akawa anajikuta anayajibu.
 
Kwa kweli baadhi ya watanzania tuna Roho mbaya sana, ni basi tu. Ndugai mwenyewe wakamfurusha.
Waalamia hawala urafiki wa kweli zaidi ya maslahi binafsi, hivyo usijeukasema watakuwa wanavutiwa na wewe hata hapo baadae ukifanga kosa, pia kuondolewa kwake kumetufundisha kwamba alipokuwa anazuia watu wasitoe maoni na yeye kazuiliwa pia kwa maoni yake kwamba "Tusipoangalia nchi itauzwa hii, kila siku kukopa"
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Lissu: “Nakielewa kwamba taarifa za kufanyika kwa kosa la jinai inaweza kutolewa kwa mdomo au kwa maandishi kwa afisa wa eneo husika wa mamlaka.”

Job Mrema: “Katika eneo husika unalolalamikia, ulipeleka malalamiko?”

Lissu: “Sikupeleka kwa sababu nilikuwa nusu mfu, kwa sababu nilipelekwa Nairobi nikiwa sijitambui. Kwa hiyo, sikuwepo; nilikuwa Nairobi napigania uhai wangu.”

“Niliporudi, nikaenda kwa RPC Moroto kwamba nimerudi, nichukueni maelezo, wakakataa. Nikawaambia nipeni gari langu, nikachukua gari, lakini hawakuchukua maelezo.”

Job Mrema: “Kwenye maelezo yako umeieleza Mahakama kwamba kwa sababu umekuwa mwanaharakati kwa muda fulani, ukataja baadhi ya Polisi kwamba ukasema kuna sehemu wakasema, ‘maliza huyu.’”

Lissu: “Utakuwa umesikia vibaya.”

Job Mrema: “Wewe ni mwanasheria, unajua kwamba ukiwa na malalamiko unatakiwa kutoa taarifa Polisi?”

Lissu: “Unatoa taarifa Polisi kama Polisi siyo wahusika wenyewe. Nimesema nimekuwa nikikamatwa, kufanyiwa vitisho na Polisi wenyewe.”

Job Mrema: “Moja ya statement ulitoa ya Majaji ni CCM na Mahakamani hakuendeki, yalikuwa yanakiuka kifungu cha 51(1).”

Lissu: “Waheshimiwa Majaji, sikubaliani na yeye.”

Job Mrema: “Utakubaliana na mimi kwamba Mahakama ikishatoa maamuzi yake, inatakiwa kufuatwa?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba Mahakama Kuu ilishawahi kutoa amri ya ulinzi wa mashahidi?”

Lissu: “Ndiyo.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba shauri lililoamriwa na kutoa ulinzi wa mashahidi ni tofauti na shauri hili lililopo mbele sasa hivi?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Ni sahihi kwamba kupitia uamuzi huo wa ulinzi wa mashahidi, haijawahi kufanyiwa uamuzi wa kuondolewa?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Kama hukufurahishwa na uamuzi huo, si ungeweza kuchukua hatua?”

Lissu: “Nikichukua hatua ndiyo maana nikaja kuwaambia Majaji hapa kwamba kinachofanyika hapa ni tofauti na amri ya Jaji Mtemwa.”

Job Mrema: “Sijauliza utekelezaji wa amri.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Na ndio lengo lao.
TAL anautulivu sana kichwani na wamegundua kwenye mambo ya sheria hawamuwezi kwa hiyo wanachotumia ni kumpanikisha alopoke jambo lolote lile ambalo baadae watalitumia kwa wale mashahidi wengine tena Mimi Nina hofu na Heche watamuuliza maswali ya kumpa hasira nae aropoke waunganishe dot watumie kwenye uhaini sasa.....awe sana makini mwenyekiti wenu
 
Nadhani anaweza kufanya hivyo. Sema ameamua kwenda nao hivyo hivyo
 
Nadhani alipata funzo kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…