Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

Mbona hii kesi sasa hivi hata haieleweki ni kama vile Kila mtu anajaribu kumpotezea mwenzake muda,,,Yani maswali ni yale yale Yani kama wanazunguka tu alafu wanaishia pale pale 😀😀au hii posho ya Leo ya kumsifia Vaisiprezidenti mpya kule insta imeanza kunilewesha
 
Mbona hii kesi sasa hivi hata haieleweki ni kama vile Kila mtu anajaribu kumpotezea mwenzake muda,,,Yani maswali ni yale yale Yani kama wanazunguka tu alafu wanaishia pale pale 😀😀au hii posho ya Leo ya kumsifia Vaisiprezidenti mpya kule insta imeanza kunilewesha
Hapo Katuga & co wapo bize kuokoa ushahidi wao kabla ya siku ya "submission" maana mpaka Leo wao 0 Lissu 3.
 
Mbona hii kesi sasa hivi hata haieleweki ni kama vile Kila mtu anajaribu kumpotezea mwenzake muda,,,Yani maswali ni yale yale Yani kama wanazunguka tu alafu wanaishia pale pale 😀😀au hii posho ya Leo ya kumsifia Vaisiprezidenti mpya kule insta imeanza kunilewesha
Ivi kuna idadi kamili ya hayo maswali ya dodoso au hadi siku mbili ziishe?
 
Mbona hii kesi sasa hivi hata haieleweki ni kama vile Kila mtu anajaribu kumpotezea mwenzake muda,,,Yani maswali ni yale yale Yani kama wanazunguka tu alafu wanaishia pale pale 😀😀au hii posho ya Leo ya kumsifia Vaisiprezidenti mpya kule insta imeanza kunilewesha
Katuga amebanwa kwa hivyo Hana jinsi. Anahangaika kurudia makosa. Mpaka anamwambia Lissu unaipa mahakama kazi ngumu.
 
Katuga taangu mwaka 2007 yupo mahakamani anashughulika na Kesi anajua ujela jela wa kila aina so hayo ni matusi ya kawaida sana kwake. Acha Uwakili wa kina Tundu Lissu huyo Katuga Ame practice kweli kweli kuanzia Kisutu pale mpaka mahakama ya Rufaa. Sidhani katika carrer yake Tundu Lissu amewahi kuwakilisha hata Kesi 5 kwa mwaka!
Sasa huko mahakamani alikuwa anafanya kazi gani kama uwezo wake ndo huu?. Usikute Kuna watu walifungwa kabisa kwa uwezo wa namna hii ?.
 
Hatua ya maswali ya dodoso (Cross Examination) kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, yanatarajiwa kutamatishwa leo Agosti 27, 2026 na kufungua mlango kwa shahidi mwingine wa Lissu kupanda kizimbani kwaajili ya kutoa utetezi wake.


Jana Agosti 26, 2026, Tundu Lissu alihitimisha kutoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Jaji, Dunstan Ndunguru, ambapo ambapo baada ya hatua hiyo, upande wa Jamhuri (Washtaki) walipewa nafasi ya kuuliza maswali hayo kwa mshtakiwa.

Katika utetezi wake wa Jana, Lissu alidai kwamba Ushahidi uliotolewa na Askari Polisi wa upande wa Jamhuri, ulikuwa unatofautiana kwa maelezo waliyoyaandikaa Polisi na yale waliyoyawasilisha mahakamani.

Mwenendo wa Kesi ya Uhaini Mahakamani sehemu ya 289

Majaji wameingia muda huu na Mwenyekiti ameingia Mahakamani.

Anasimama Karani wa Mahakama anasema Criminal Session No. 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.

Iwapendeze Majaji Naitwa Ajuye Zengeli, Nassoro Katuga, Job Mrema, Cathbert Mbiringe, Winiwa wote tunaiwakilisha Jamhuri na Mtuhumiwa yupo hapa. Tuko tayari kuendelea na maswali ya Dodoso.

Mh. Lissu naomba nipate nafasi ya kuconsult mawakili wangu kidogo.

Anasimama Dr. Nshala anashauriana nae hapo kizimbani kwa dakika kama tano.

Sasa niko Tayari.

Katuga: Kaka angu Shikamoo?

Mhe. Lissu: Marahaba

Katuga: Kama nilikuelewa unasema kuna tuzo ulipewa ilitokana na kupigania haki kwa nchi za Afrika. Je ulitaja hizo nchi za Afrika ulizopogania?

Mhe. Lissu: Sikutaja

Katuga: Ulisema heshima imeongezeka ulifanya sensa wapi?

Mhe, Lissu: Heshima haipatikani kwa sensa. Inatokana na watu wanaoheshimika wakakuheshimu.

Katuga: Kwahiyo imeongezeka ni kwasababu wazungu wamesema?

Mhe. Lissu: sijasema wazungu nimesema Jumuiya za Kimataifa na zinaheshimika kweli.

Katuga: Ulisema mgombea wa Mlimba alirudisha fomu akakuta ofisi imefungwa? Je ulikuwepo?

Mhe. Lissu: Hizo ni taarifa rasmi sio lazima niwepo, nilisoma kwenye taarifa rasmi.

Katuga: Ukitoa mashahidi kutoa Jeshi la Polisi hawa waliolindwa hawajulikani na mtu yeyote?

Mhe:Lissu: Ndio

Katuga: Haya maneno umesema kuonesha ukweli wako?

Mhe. Lissu: Kweli

Katuga: Uamuzi wa Majaji ulisemaje kuhusu mashahidi wa siri?

Mhe. Lissu: wawaone wao.

Katuga: Uliwaambia kuwa hawawajui majina na kila kitu?

Mhe. Lissu: ni ushahidi wangu hawawajui ndio

Katuga: kwahiyo hawawajui majina?

Mhezx Lissu: Sasa mtu gani anaitwa P2, Sijui P

Katuga: Kwahiyo hayo ya P1, P2 sio majina?

Mhe. Lissu: Sio majina hayo nimesema.

Katuga: Hizo si ni synonim?

Mhe, Lissu: Synonim sasa ni majina? Hayo sio majina.

Katuga: Umesema ni sheria gani shahidi anapaswa kutoa jina?

Mhe, Lissu: CPA na sheria ya Ushahidi zote zinasema jambo hilo.

Katuga: Naomba Kifungu?

Mhe, Lissu: Kifungu cha 192 cha CPA

Katuga: kisome sasa wapi wanasema wataje majina?

Mhe, Lissu: kisome uone kinasemaje ngoja nikusomeee kinapotaja hitaji la jina?

Katuga: sitaki ukisome.

Mhe. Lissu: Hutaki tena nisome.

Katuga: Kwahiyo neno la kuwa lazima watoe jina lipo?

Mhe: Lissu: Unadhani kwanini mashahidi huwa wanaulizwa majina yao Mahakamani?

Katuga: Hilo sijakuuliza.

Mhe, Lissu: Hiyo sasa utajua mwenyewe kama hujaniuliza.

Katuga: Pw 17 alisema kuna muda waandishi wa habari walitolewa mkabaki wenyewe na kikao cha ndani? Uliwahi kukanusha hilo?

Mhe. Lissu: Nikanushe la nini? Ndio ukweli

Katuga: Una volunteer sana information.

Mhe.Lissu: Ndio kazi yangu.

Katuga: Majibu yako yana vutia sana.

Mhe. Lissu: then, you should be happy.

Katuga: Kwahiyo nichekecheke

Mhe. Lissu: Fanya hivyo

Katuga: Kwahiyo mliwatoa waandishi nje, wewe na wenzako?

Mhe. Lissu: Tuliwatoa.

Katuga: Mliwatoa kwasababu hayo mengine hayakuwa sehemu ya mliyowaitia. Kwahiyo yale ambayo mlitaka wayachapishe ndio mliruhusu wawepo?

Mhe. Lissu: Ndio.

Katuga: Ambayo hukutaka yachapishwe mliwatoa waandishi?

Mhe. Lissu: Yote tuliyotaka watu wajue waliyajua.

Katuga: Je kwenye ushahidi wako ulisema sheria mahsusi kwamba ukigundua kosa la uhaini unapaswa kuwasiliana na DPP?

Mhe.Lissu: Nikitaje cha nini? Haina maana hakipo kama sikukitaja.

Katuga: Mimi lazima nikuulize maswali nisipofanya nitakuwa sifanyi kazi yangu

Mhe. Lissu: Fanya kazi yako.

Katuga: Ulisema kuna mgogoro binafsi na Wambura na Kingai?

Mhe. Lissu: nimesema kuna chuki kubwa dhidi yangu. Nimekuwa persecuted maliciously 24yrs.

Katuga: Umewahi kufungua malicious prosecution

Mhe. Lissu: Haina maana yoyote sijawahi kuwafungulia lakini haiondoi ukweli wowote.

Sehemu ya 290

Katuga: Ulisema Mashahidi waliolindwa walifanyaje?

Mhe. Lissu: Walikuwa ni washitakiwa na watuhumiwa wa makosa

Katuga: Sheria inawazuia wasiwe mashahidi

Mhe. Lissu: Haiwazuiii.

Katuga: Mashahidi wa Jeshi la Polisi walieleza kuwa walikamata wote?

Mhe. Lissu: Walisema wamewakamata waliowatambua.

Katuga: Kwahiyo kuna wengine hawakukamatwa?

Mhe. Lissu: Ntajuaje sasa?

Katuga: Ile kauli yako ya tutavuruga uchaguzi ulisema mtu yeyote anaweza kutafsiri anavyoona?

Mhe, Lissu: Sahihi

Katuga: Walisema hawa mashahidi kuwa waliyopanga yalitokana na maneno yako?

Mhe. Lissu: Najuaje sasa watu siwajui na siwafahamu. Nasemaje watakuwa wanasema ukweli.

Katuga: Katika ushahidi wako umeiambia mahakama hii tukufu kuwa hawa mashahidi hawasemi kweli?

Mhe. Lissu: Nimeiambia mahakama kuwa huu ushahidi ni wa wahalifu na ni waongo.

Katuga: Katika utetezi wako ulisema kuwa wewe uliwachochea?

Mhe. Lissu: Wapi nimesema hivyo? Sijasema mimi.

Katuga: Wanasema maneno yako ndio yaliwachochea sasa wewe uliwaambia majaji kuwa maneno haya hayawezi kuwachochea.

Mhe. Lissu: Nimewaambia Majaji maneno haya hayawezi kuwa uchochezi sio kosa pia. Labda kama ulikuwa umelala.

Katuga: Waheshimiwa naogopa kurudia maswali. Amekaa kimya anatafuta tafuta. Sasa wale mashahidi waliolindwa

Mhe, Lissu: mimi nimekwambia mashahidi waliofichwa hiyo kulindwa umetoa wapi?

Katuga: Witness protection ni nini kiswahili?

Mhe, Lissu: Mashahidi waliolindwa. Lakini sasa mimi nimesema kwangu ni mashahidi waliofichwa. Hiyo ya kulindwa ni yakwako.

Katuga: Je wale mashahidi walifichwa kweli?

Mhe. Lissu: ni ushahidi wangu kuwa hao mashahidi hawajulikani

Katuga: Huo ni ushahidi wa kuona au kusikia.

Mhe. Lissu: Ni ushahidi wa inference hakuna anayewajua isipokuwa mapolisi.

Katuga: Hizo ni speculations au ushahidi wa direct.

Mhe. Lissu: Huo ni ushahidi.

Katuga ameenda kunong'ona na wenzake.

Anauliza sasa swali: Nimehama kwenye inference. Maneno unawezekana maneno ya mashahidi wakulindwa inawezekana walikuwemo humu ndani wakati kesi inaendelea.

Mhe. Lissu: Nimeshasema hawajulikani na mtu yeyote.

Katuga: Ni kweli au sio kweli?

Mhe. Lissu: Ni ushahidi wa inference. Huelewi nini? Kwasababu mnawajua nyie peke yenu.

Katuga: Mimi sitoki hapa

Mhe. Lissu: Hata mimi sitoki.

Katuga: Mahakama inakunote

Mhe. Lissu: Kwanini wewe haikunote?

Katuga: kwahiyo ni kuona au kusikia?

Katuga: Shahidi shule si ulikuwa unafundishwa multiple choice?

Mhe. Lissu: Mimi sijafundishwa multiple choice. Mimi nimefundishwa critical thinking. Sheria unafundishwaje multipe choice? Ndio maana unakuwa mjinga.

Katuga: Hii kauli hawa mashahidi inawezekana walikuwepo mahakamani ni maoni au ushahidi?

Mhe. Lissu: Ni ushahidi wangu maoni kivipi.

Katuga: Kwenye ile video kuwa Majaji ni Maccm ulisema hukumbuki?

Mhe. Lissu: Nilisema nakumbuka. Huwa sikatai maneno yangu.

Katuga: Una kesi nyingine ya jinai ya kuchapisha taarifa za uongo?

Mhe. Lissu: Ipo Kisutu anawatajia hadi namba nyingine ya kesi.

Katuga: Ulisomewa hoja za awali na imeanza kusikilizwa?

Mhe. Lissu: Imesomwa lakini sikumbuki.

Katuga: Uliposomewa hoja za awali na kwamba ulitoa maneno kuwa majaji ni Ma CCM? Ulijibuje?

Mhe. Lissu: Sikumbuki. Sasa unaniulizaje hayo mengine.

Katuga: Mwenyekiti wa CHADEMA ni kweli ulitangaza kutogombea uchaguzi wa Mwaka jana?

Mhe. Lissu: Sikumbuki.

Katuga: Chama chako kilishiriki Uchaguzi mwaka jana?

Mhe. Lissu: Uchaguzi gani sasa? Hakikushiriki.

Sehemu ya 291

Katuga: Kutokulipiwa na matibabu na umeeleza vitu vingi kuhusu uchaguzi. Imani yako uliposema imani yako na mahakama haipo kwahiyo huna imani?

Mhe. Lissu: Hilo ni la kuuliza kweli. Kwenye maswala haya sina IMANI KABISA NA MAHAKAMA.

Katuga: Maswala yapi?

Mhe. Lissu: Si ya Uchaguzi tunazungumzia.

Katuga: Kwahiyo hukupanga kuiomba Mahakama kutengua vifungu fulani vya Katiba?

Mhe. Lissu: Sikupanga.

Katuga: Uliamua kutafuta njia nyingine mbadala?

Mhe. Lissu: Njia ya mbadala ya Kidemokrasia.

Katuga: Jana nilikuulizia kuzuia uchaguzi ni njia ya kidemokrasia.

Mhe. Lissu: Haswaa.

Katuga: Kukinukisha ni njia ya kidemokrasia?

Mhe. Lissu: Haswaa ni njia ya kidemokrasia.

Katuga: Kuhamasisha uasi je?

Mhe. Lissu: Njia ya kidemokrasia kabisa. Mwalimu Nyerere alisema uasi dhidi ya mifumo kandamizi ni halali kabisa.

Katuga: Kifungu cha 52 cha Media Service Act iko sawa na kifungu cha 55?

Mhe. Lissu: Iko sawa.

Katuga: Sheria ya Huduma za Habari iliundwa ku regulate huduma ya habari?

Mhe. Lissu: Ndio

Katuga: Kuzuia uchaguzi uliopo kwa mujibu wa sheria ni kuipinga serikali?

Mhe. Lissu: ni kuzuia uchaguzi. Kuipingaje tena serikali?

Katuga: Kuhamasisha uasi, kukinukisha. Ni kuipinga serikali au kuipindua serikali.

Mhe: Lissu: Hatukuwa tunazungumza habari za serikali.

Katuga: Mbona nakuuliza swali kwa heshima tu

Mhe. Lissu: Huna heshima hata kidogo. Uitoe wapi?

Katuga: Unakumbuka ulisema kuipinga serikali sio kosa?

Mhe. Lissu: Nimesema.

Katuga: Sasa ulikuwa unamaanisha nini?

Mhe. Lissu: Nassoro Katuga nimesema kifungu cha 55 hakijasema serikali peke yake

Katuga: Mimi mdogo ndio maana unanionea.

Mhe. Lissu: Wewe mdogo ungekuwa hapa? Una udogo gani wakili mkuu wa serikali?

Katuga: Ulisema mapolisi kujiandika maelezo ni kinyume cha sheria na je uliwatajia sheria.

Mhe. Lissu: Sikuwaambia lakini kifungu kipo na kinajulikana.

Katuga: Sasa mbona unaniambia sina adabu halafu wewe hujibu maswali.

Mhe. Lissu: Unataka niseme yakwako?

Katuga: Ulisema vielelezo vilivyoingia mahakamani uliviingiza wewe?

Mhe. Lissu: Viliingizwa na Mahakama.

Katuga: Kwahiyo umeridhika na content za hivyo vielelezo?

Mhe. Lissu: nimeridhika vitumike kuonesha sina hatia.

Katuga: Naomba D1 hadi D16.

WANAMTAFUTIA WAMPATIE VIELELEZO.

Katuga: Unakumbuka D1 ni kielelezo cha Kaaya ambae ni PW2 na uliomba yatumike kwa nia ya kudodosa shahidi kwa mujibu wa kifungu cha 163?

Mhe. Lissu: Kweli

Katuga: ni kweli tulisema kuhusu ommission na contradiction?

Mhe. Lissu: Nilisema.

Katuga: Ulisoma kifungu cha 163 hapa Mahakamani? Na ukasema hakuna neno omission kwenye kifungu hicho na neno pekee lililopo ni contradiction?

Mhe. Lissu: Nakumbuka.

Katuga: Ulimuuliza Kaaya ameajiriwa mwaka 2009 na ameenda Zanzibar au hajaenda? Na akajibu hayamo? Unakumbuka?

Mhe. Lissu: Nakumbuka.

Katuga: kutokuwepo kwenye maelezo yake ni contradiction au ommission?

Mhe. Lissu: Omission.

Katuga: Kwenye hiki kielelezo ni contradiction gani ipo hapo?

Mhe..Lissu: Mahakamani alisema ni Uhaini lakini kwenye maelezo amesema ni makosa ya jinai.

Katuga: Uhaini ni madai au jinai?

Mhe. Lissu: Jinai ziko ngapi sasa? Alitakiwa kueleza kuwa jinai ni ipi?

Katuga: Ni bado unasema kwenye hiyo nyaraka kuna contradiction

Mhe. Lissu: Nimeshaonesha.

Katuga: D2 unakumbuka ulimuhoji kwamba yeye ni mtaalamu wa picha aliyetangazwa kwenye GN 725 akajibu maneno hayo hayamo.

Mhe. Lissu: Ndio.

Katuga: Je hiyo ni Contradiction?

Mhe. Lissu: Ni comtradiction ndio kwasababu zilitajwa GN. mbili tofauti. Ni contradiction ya akichokisema kwenye maelezo yake ya maandishi.

Katuga: Yale majibu yote aliyosema hayamo yalikuwa ni contradiction au ommission?

Mhe. Lissu: Ni omission

Katuga: Ulisema hiyo omission inaenda kwenye root ya kesi

Lissu: Tutasema hayo mengine kwenye final submission mimi ni shahidi wa facts.

Sehemu ya 292 itaendelea
 

Attachments

  • IMG-20260827-WA0022.jpg
    IMG-20260827-WA0022.jpg
    86.8 KB · Views: 12
Nassoro Katuga: Ile kauli yako ya “Tutazuia uchaguzi, tutakinukisha,” uliiambia Mahakama mtu yeyote anaweza kuitafsiri anavyotaka?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Wale mashahidi walisema hapa kwamba walichopanga kuzuia uchaguzi, kwa ushahidi wao, ni kwa sababu ya maneno yako.

Lissu: Ndiyo walivyosema.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako umeiambia Mahakama kwamba hawa mashahidi hawasemi kweli?

Lissu: Nimesema hivyo kwamba hawa mashahidi ni waongo na ni wahalifu, hawafai kuaminiwa.

Nassoro Katuga: Achana na kusema general ni waongo. Katika utetezi wako, specifically katika ushahidi wako, uliwaambia Waheshimiwa Majaji kwamba maneno haya hayawezi kuwachochea?

Lissu: Nimesema kwamba maneno haya hayana shida kisheria na hayawezi kuchochea.
Hoja ya tafsiri ya maneno kuwa zaidi ya moja ni sahihi, mfano JK Nyerere alishawai kusema "dhumuni la kupigania uhuru ni kuzalisha vijana waasi dhidi ya ukandamizaji" sentensi hii unaweza kuitafasiri kama maana mbaya au nzuri kwasababu neno lilombele yake lina maana zaidi ya moja "ukandamizaji" inaweza kuwa kukandamiza kitu ardhini ukutani au popote lakini pia inaweza kuwa kuonewa sasa hapa kwenye kuonewa napo kuna tafsiri mbili unaweza kuonewa na mtu anaeonekana mwema lakini umeonewa au na mfu anaeonekana mbaya lakini vyote ni uonevu.

Ukiangalia kwa kina sentensi ya JK Nyerere unaweza kusema aliunga mkono uwasi, and at the same time unaona kana kwamba ni neno zuri.

Hapa wamefeail kumpa kesi ya uhaini kesi ingekuwa uchochezi basi kungekuwa na mvutano wa uchochezi mzuri na mbaya hapo ndo wange win...
 
Mbona hii kesi sasa hivi hata haieleweki ni kama vile Kila mtu anajaribu kumpotezea mwenzake muda,,,Yani maswali ni yale yale Yani kama wanazunguka tu alafu wanaishia pale pale 😀😀au hii posho ya Leo ya kumsifia Vaisiprezidenti mpya kule insta imeanza kunilewesha
Hata mimi sielewi, nilitegemea UHAINI hapo kuna wanajeshi kadhaa wameshtakiwa, Silaha zimekamatwa na mambo ya dizaini hiyo. Kuna njama zinathibitishwa zilipangwa.

Sasa wanabishana tu mara video mara maneno, sijui utazuia uchaguzi. Sasa kuna serekali inapinduliwa kwa sentensi mbili duniani?

Kama Taifa tuna safari ndefu sana.
 
Sasa mtu hajateuliwa halafu anajifanya ni mtaalamu wa picha mjongeo wakati yeye ni wa picha mnato, inakuwaje ni "omission" na siyo "Contradiction"?

Yaa Katuga anaona anaweza kumtega Lissu kiboya namna hiyo?
Exactly, anajaribu kumpa mfano wenye contradiction ndani yake kisha akimrudisha kwenye vielelezo vya D1 na D2 anataka hapite mule mule we umeona wapi mpishi anathibitisha upishi wake (mpishi bora) kwa kushika mwiko mkononi....? Kama sio mtaalamu sio mtaalamu tu toa ushibitisho katuga kama kweli ni mtaalamu wa hizo mambo.
 
Back
Top Bottom