TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI
Nassoro Katuga: Kuna mahali popote katika mashitaka yako kuna sehemu inasema umeshitakiwa kwa kuchapisha video?
Lissu: Ndiyo, nimeshitakiwa.
Leo mnakimbia, enheeee!
Nassoro Katuga: Video?
Lissu: Ndiyo, nashitakiwa kuchapisha maneno katika mtandao wa Jambo TV wa YouTube.
Mnataka kukimbia!
Nassoro Katuga: Video inakuwa na vitu viwili: sauti na picha/mjongeo.
Lissu: Video lazima iwe na kuonekana na kusikika.
Nassoro Katuga: Nakuuliza, maneno yanasikiwa au yanaonwa?
Lissu: Kama maneno ya kusikia, utasikia, na maneno ya kuona, utaona.
Nassoro Katuga: Dooooooooooh! (Kachoka kabisa.)
Nassoro Katuga: Katika sheria ya ushahidi, kuhusiana na maneno, anatoa ushahidi wa kuona au kusikia?
Lissu: Kama ni maneno tu, shahidi atasema, “nimesikia.”
Nassoro Katuga: Rudi kwenye mashitaka yako kwamba unashitakiwa kwa nini.
Lissu: Kutoa maneno na kuyachapisha katika mtandao wa Jambo TV wa YouTube.
Nassoro Katuga: Sasa ulisema upande wa mashitaka hawajathibitisha hiyo video kwa sababu hawajaileta?
Lissu: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Mashahidi wa Jamhuri wakikuja kusema nini kuhusu video?
Lissu: Walisema wameona video akisema hivi.
Huwezi kutenganisha video na maneno.
Nassoro Katuga: Unajua kuwa kila shahidi ana haki ya kuaminiwa?
Lissu: Shahidi anastahili kuaminiwa kama ana stahili kuaminiwa kwa grounds za kuaminiwa (credible).
Nassoro Katuga: Iambie Mahakama hii, kama katika mashahidi wa Jamhuri wale wamesema wameona video, ni kifungu gani cha sheria kinachosema kwamba kama wanasema wameona video lazima walete hiyo video?
Lissu: Siyo sheria, ni common sense tu. Ili uaminike na uthibitishe, lazima ulete video.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo mtu akisema ameona radi imempiga mtoto, lazima alete radi hapa Mahakamani?
Lissu: Radi na video vinahusiana nini?
Nassoro Katuga: Mtu anayepandisha video mtandaoni anaweza kuifuta?
Lissu: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Unajua ile mtandaoni wanasema kitu kina “pop, paap!” alafu kinapotea?
Lissu: Kitu gani hicho?
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI