Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuendelea na maswali ya dodoso Mahakamani Agosti 27, 2026

TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: “Ulieleza nini alipotaka kukuhoji maana ya maneno haya?”

Lissu: “Hakuna, alipotaka kunihoji kwa sababu sikuulizwa juu ya maelezo.”

Nassoro Katuga: “Alitaka kukuchukua maelezo ya nini?”

Lissu: “Sijui kwa sababu hakunisomea uhaini. Walikuwa wameshanisafirisha usiku kucha, na kwamba anataka kunichukua maelezo kwa uhaini, nikasema tutakutana Mahakamani.”

Nassoro Katuga: “Ni kweli au si kweli Bwana Bagyemu akikupa nafasi ya kutoa maelezo?”

Lissu: “Ningesemaje wakati nakamatwa na kusafirishwa usiku kucha, halafu nitoe maelezo gani?”

Nassoro Katuga: “Katika ushahidi wako, kwa wakati fulani ulirejea maelezo D16?”

Lissu: “Nakumbuka.”

Nassoro Katuga: “Waambie Waheshimiwa Majaji yale maneno ambayo uliyarejea katika D15, umeyaamini ndiyo maana yapo katika utetezi wako.”

Lissu: “Maneno yepi?”

Nassoro Katuga: “Anasema baada ya kuunda timu, tulitazama na kuona video hiyo ambayo bado ilikuwa mtandaoni. Nilipotizama ndipo nikabaini kuna kosa la jinai.”

Lissu: “Nakumbuka.”

Nassoro Katuga: “Wakati huo wote, huyu shahidi alikuwa anakuhoji, aliona una tuhuma za uhaini?”

Lissu: “Kwa direct ina relation to PW1.”

Nassoro Katuga: “Sasa ulirejea Kielelezo D15 kwa sababu ulikiamini Kielelezo hicho?”

Lissu: “Sikukiamini, bali nilikitumia kuonyesha utofauti wa maelezo. Kwa sababu hayo maneno yanatofautiana, siyo kwa sababu ninayaamini.”

Lissu: “Mimi naweza kuwaamini hawa Polisi?”

Lissu: “Nimeyatumia kwa sababu wote walitazama video moja, mmoja anasema aliona uhaini, mwingine hasemi.”

Nassoro Katuga: “Ni kweli ulisema hiki kielelezo ni chako?”

Lissu: “Ni kwa sababu nakitumia kuonyesha contradiction.”

Nassoro Katuga: “Kwa maneno yako mwenyewe, hiki kielelezo hakijapokelewa kwa mujibu wa 163?”

Lissu: “Kimepokelewa.”

Nassoro Katuga: “Maelezo haya umeyaamini, hujayaamini?”

Lissu: “Kwa kitu gani?”

Jaji Ndunguru: “Ungejibu swali lake.”

Lissu: “Swali lake, naamini kwa kitu gani? Swali lake silielewi.”

Nassoro Katuga: “Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni kweli au si kweli kwamba uliomba yatumike.”

Lissu: “Yatumike kama sehemu ya utetezi wangu.”

Nassoro Katuga: “Waambie Waheshimiwa Majaji, Kielelezo D1 mpaka D16 vitumike kuonyesha Omission au Contradiction?”

Lissu: “Vitumike kuonyesha Omission na Contradiction.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Mkuu hebu endelea kutuwekea huo udambwidambwi kusnzia sehemu ya 294 na kuendelea
 
Leo Katuga amegonga mwamba. Akakae tu.
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: “Kwa kuwa umeiambia Mahakama hii hivi vielelezo vitumike sehemu yoyote, kuanzia D1 hadi D16, kwamba kwenye nyaraka hizi chukueni hiki, muache hiki?”

Lissu: “Hiyo ni kazi ya submission.”

Nassoro Katuga: “Wakati unawaambia Majaji vielelezo vitumike, ukiwaambia watumie vielelezo hivi sehemu hii na sehemu hii isitumike?”

Lissu: “Nitawaambia wakati wa Final Submission.”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa Majaji, naomba ajibu swali langu.”

Jaji Ndunguru: “Shahidi?”

Lissu: “Nitawaambia Mahakama wakati wa Final Submission.”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa Majaji, naomba nisipoteze wenzangu muda.”

Jaji Ndunguru: “Hapana, tulikuwa tunajadili swali la mwisho. Tunaomba lirudiwe.”

Nassoro Katuga: “Sawa. Shahidi, katika utetezi wako hapa Mahakamani uliwaambia Waheshimiwa Majaji kwamba maudhui haya chukueni na haya yaacheni?”

Lissu: “Hiyo sikuwaambia.”

Nassoro Katuga: “Kwa hiyo, kama hujawaambia Waheshimiwa Majaji, watakuwa na haki ya kutumia maudhui yote?”

Lissu: “Hilo sasa ni suala la Majaji.”

Nassoro Katuga: “Waheshimiwa Majaji, naomba kwa ridhaa yenu nimkaribishe Wakili Mkuu wa Serikali, Job Mrema.”

Job Mrema anasogea.

Job Mrema: “Waheshimiwa Majaji, nina maswali machache na shahidi.”

Job Mrema: “Shahidi, naomba kukuuliza swali la kwanza. Ulieleza Mahakama hii wewe ni mwanaharakati, kweli au si kweli?”

Lissu: “Ni kweli.”

Job Mrema: “Waeleze Majaji huo uanaharakati umeuanza lini?”

Lissu: “Nimeanza harakati siku nyingi sana, tangu nikiwa sekondari na baadaye Jeshini.”

Job Mrema: “Hebu waeleze Majaji, uanaharakati ni nini?”

Lissu: “Neno harakati ni mtu anayefanya au kupigania jambo au mambo fulani.”

Job Mrema: “Kama nimekuelewa, wakati umeanza kutoa ushahidi wako umejipambanua wewe ni Wakili. Hebu waambie Waheshimiwa Majaji, huu uanaharakati uliokuwa unaufanya unatambulika kwa sheria za nchi?”

Lissu: “Katiba yetu, Ibara ya 22 mpaka 29, imetoa uwanja mpana wa mwananchi kama mimi kupigania au kuona yanayohitaji kupiganiwa.”

Job Mrema: “Waheshimiwa Majaji, naomba Shahidi apewe hiyo Katiba, awaonyeshe Majaji ni Ibara ya ngapi.”

Lissu: “Kwa nini mimi nimekwambia Katiba imesema nini kuhusu harakati?”

Job Mrema: “Nilikuuliza ni sheria zipi za nchi.”

Lissu: “Nimesema.”

Job Mrema: “Waambie sasa Waheshimiwa Majaji, Ibara ya ngapi inakupa ruhusa ya kufanya harakati?”

Lissu: “Katiba haipo hivyo. Katiba inatoa uhuru unaotuwezesha kufanya harakati kuanzia Ibara ya 12 hadi 29. Katiba ikisema upo huru, una uwezo kwenda kupigania uhuru wa watu magerezani, hiyo ni harakati.”

Job Mrema: “Utakubaliana na mimi kwamba, specifically, hakuna neno ‘harakati’ katika Katiba?”

Lissu: “Specifically, hakuna.”

Job Mrema: “Hizo harakati unazofanya zina mipaka kisheria?”

Lissu: “Ndiyo, zina mipaka kisheria.”

Job Mrema: “Utakubaliana na mimi kuwa unapotafuta haki upande mmoja, hutakiwi kuathiri haki za watu wengine?”

Lissu: “Hiyo ni sawasawa.”

Job Mrema: “Unakubali kwamba ni sahihi maneno ya hati ya mashitaka?”

Lissu: “Ni sahihi.”

Job Mrema: “Utakubaliana na mimi kwamba waliosikia yale maneno walitafsiri kadiri yalivyo?”

Lissu: “Hawakutafsiri kadiri yalivyo.”

Job Mrema: “Waambie Waheshimiwa Majaji, pale utakubaliana na mimi kwamba, kwa mujibu wa sheria zetu za nchi, hakuna mahali zinaporuhusu kuharibu mali za watu au kuchoma kama walivyofanya Oktoba 29?”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Ila Katuga mnafiki sana, sana.
Watu kama hawa ni hatari kama ukoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…