Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Nilijua mawakili wa Serikali akina Katuga wana uwezo mdogo ukilinganisha na Lissu.Lakini sikujua ni vilaza wa kupita viwango vya kawaida.
Kuna bΓ adhi ya maswali sijui anauliza ili apate nini.Haijulikani anataka kudhoofisha namna gani ushahidi wa Lissu.Na kuna bΓ adhi ya maswali badala ya kuwa faida ya upande wa mashtaka yanamsaidia mshtakiwa.
 
Jina lake linasadifu yaliyomo. Kule usukumani watu kama yeye wanaitwa Ntuga, Katuga, Gehu, Mwakajinga n.k.
 
Ukichukua historia yake ya mapambano ya kisiasa aliyoisema katika utetezi wake hapa, jumlisha misimamo yake hata Sasa akiwa mfungwa, bila kusahau mihoja aliyokuwa akiijenga akiwa bungeni, na ukasoma ni nini hasa kilichomo Moyoni mwake na akilini mwake kuhusu nchi ya Tanzania.... Ni wazi Kuna kichwa cha kipekee sana katika nchi hii. Baada ya sakata hili Kuna mazwazwa watajuta kumfahamu TAL
 
Magufuli alipotumia mtutu badala ya mahakama kujaribu kumzimisha Lissu huyu Mama alijua anachekesha?
Nimesema... Baada ya hili sakata watajuta kumfahamu TAL

Binafsi nilikuwaga najua kwamba Mh. Tundu ni mwanasheria, ila sikuwahi kujua ni wa KIWANGO HIKI.
Wakati akiwauliza maswali ya dodoso wale mashahidi wa Jamhuri sikuwa napata mantiki ya baadhi ya maswali yake, zaidi TU ya kuuona ufundi wake katika kudodosa. Ila Sasa.... Wakati huu akijitetea, ndipo napata connection murua kabisa
 
Wao wanajalibu ku link it with UHAINI, kuna muda katuga alikuwa anauliza maswali ambayo hayana hoja kabisa na kile wanachokitafuta ni kama walikuwa wanatafuta kuchelewesha muda tu, all in all ngoja tuone kesho kama wataweza ku link maswali ya leo na huo UHAINI.
 
Huyo Katuga kwa kujistukia, linajifanya kumuheshimu Lissu kwa kumuambia Kaka, na lissu sio mnafiki anambaluza hapo hapo

..kitendo cha kumuita kaka kinathibitisha kuwa sio mhaini.

..hivi unafikiri mhaini wa kweli angekuwa kizimbani, waendesha mashtaka wangethubutu kuwa na heshima, au hisani, naye?

Cc Nguruvi3
 

Lissu anapeleka pale pale unapotaka, yaani anAKupa na nyongeza.
 
..kitendo cha kumuita kaka kinathibitisha kuwa sio mhaini.

..hivi unafikiri mhaini wa kweli angekuwa kizimbani, waendesha mashtaka wangethubutu kuwa na heshima, au hisani, naye?

Cc Nguruvi3
Sijajua kwanini ameamua kumwita kaka mtu ambaye anamshikati kwa kosa kubwa namna ile, tena anarudia mara kwa mara wewe ni ndugu yangu, nakuheshimu sana!?
 
Leo wanaanza mapema sibanduk had wamalize na mimi binafsi nakushukuru Waufukweni kwa kutuletea updates
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…