GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi 18 Agosti 2025

GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi 18 Agosti 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Shauri la Jinai Na. 8607/2025 Jamhuri vs Tundu Lissu - Mahakama ya Hakimu Mkazi DSM Kisutu

Kesi ya jinai inayomkabili mwanasiasa na mwanasheria maarufu Tundu Lissu imeendelea leo Agosti 13, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Wanafunzi wa mashtaka na wafuasi wa Lissu wamekusanyika nje ya mahakama huku hali ya ulinzi ikiwa imara.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga, anatarajiwa kutoa uamuzi wa hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili. Upande wa Lissu umeipinga mara kwa mara ombi la Jamhuri la kuahirisha shauri hilo bila kuchukua hatua ya kupeleka kesi Mahakama Kuu, jambo ambalo linaleta wasiwasi miongoni mwa wananchi waliokusanyika kufuatilia kesi hiyo.

Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, Agosti 4, 2025, ilikubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa zingine za mashahidi wa upande wa mashtaka, hatua iliyolenga kulinda usiri wa mashahidi na usalama wa mchakato wa kisheria.

Updates

Asubuhi saa 1:00, Wananchi wamefurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Taifa, Tundu Lissu.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Joseph Osmund Mbilinyi akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mmoja kati ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akivutana na askari wa Jeshi la Polisi katika Mahakama ya Kisutu ambako kesi inayomkabili mwenyekiti wao, Tundu Lissu, inaendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 13, 2025 ambapo Mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.

Nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wananachi wakisubiri uamuzi wa shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu haijaanza hadi sasa Saa Nne Asubuhi

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, iliyokuwa imepangwa kuanza kusikilizwa saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mpaka sasa saa nne bado haijaanza.

Wakati huu, Lissu pamoja na jaji hawajaingia ndani ya ukumbi wa mahakama, huku wananchi na wanahabari wakiendelea kusubiri.

Hongera sana kamanda kwa kutuhabarisha. Big up sana.
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, iliyokuwa imepangwa kuanza kusikilizwa saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mpaka sasa saa nne bado haijaanza.

1755071309231.png
Wakati huu, Lissu pamoja na jaji hawajaingia ndani ya ukumbi wa mahakama, huku wananchi na wanahabari wakiendelea kusubiri.

Kiti ambacho amekuwa akikitumia Tundu Lissu Kizimbani kikiondolewa kabla ya kuanza kwa usikilizaji wa kesi yake ya uhaini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Nadhani watoa maelekezo wamechelewa kuamka maana jana walikuwa kwenye tone tone ya ccm. Hakimu hawezi kuendelea hadi apewe maelekezo.
 
Wamuache mtaani kuchangamke mpaka pesa walizochangisha ziwaue
 
Back
Top Bottom