Kuna mwamba namjua, kwanza kabisa yeye anaamini chochote kilichotengenezwa na binadamu kinamapungufu .
Hivyo yeye alijikita sana katika kuyachunguza hayo madude ya mchina (bonanza ), akayajua udhaifu wake ulipo , ili likupe pesa akagundua lile bonanza linakitu kama pini ambayo pindi utakapo ingiza coin ya sh 200 , hii coin ikiigusa tu hiyo pini ndiyo hilo bonanza hukupatia pesa, na ili bonanza litoa pesa akagundua pia lazima liwe limeshaingiza kiasi kilichopangwa katika mfumo wake kwanza na baada ya hapo huanza kukubali kutoa pesa .nje na hapo kila coin utakayoiweka haigusi ile pin na mchezaji hujikuta kaliwa .
Jamaa akakaa chini na kutafakari kwa kina sana namna ya kufanya ili aweze kumpiga mchina vizuri kwa kupitia hayo mabonanza aliyoyatapaza ovyo huko mtaani . Na kuja na njia ifuatayo
- alichukua coin ya sh mia mbili na kuitoboa pale katikati hali iliyopelekea upande mmoja wa coin asa ule upande msumari uliotokezea kuwa na mvimbo au muinuko , akachukua msasa na kupunguza muinuko ule ili coin ile isiweze kugoma pindi atakapoingiza kwenye mlango wa bonanza wa kuingizia pesa .
- lakini pia , ili mbidi awe mvumilivu kidogo , kwani alitakiwa kuwahi asubuhi na mapema sehemu lilipo bonanza husika ambalo alikuwa ameliweka kwenye target ya kulimanga pesa siku hiyo . Hivyo angesubilia hapo kwa muda labda tuseme toka asubuhi mbaka jioni huku akilifuatilia ni mara ngapi limetoa au kutokutoa kabisa , bonanza ambalo lilikuwa halijatoa sana ni wazi lilikuwa na kiasi kikubwa sana cha pesa ukilinganisha na lile linalotoa toa hovyo . Hivyo yeye alilitaka hili ambalo halitoi hovyo maana hili ndilo lilikuwa lenye pesa nzuri ndani yake .
- yeye alikuwa akifika anaweka ile coin yake kwa kuhakikisha hakuna anaye mfuatilia na baada ya coin kuingia ule mvimbo au muinuko wa coin pindi ulipogusa tu ile pin , bonanza bila ubishi lilikuwa linacheua ( kutoa ) pesa ya kutosha . Na baada ya hapo angeondoka haraka sana tayari kwa mkakati mpya wa kulipiga bonanza jingine .
Note :coin alimbidi kuzitengeneza nyingi maana ikishaingia kule kuitoa isingewezekana hivyo ilimbidi kuzitengeneza coin za mtindo huu mara kwa mara itakapo kufanya huu uhuni .
Hali hii iliwasumbua sana wachina kwani pindi walipofungua mfumo wa bonanza na kuona uhuni huu uliwauma sana walipeana taarufa juu ya swala hili na kuamua kubadilisha mfumo wa kuingizia coin .
Lakin mbaka wanafanikiwa jamaa tayari naye alikuwa kasha waliza sana mbaka kuweza kununua bodaboda yake na kwasasa achezi tena madude hayo kajikita safii katika kazi yake ya bodabod .