Kiasi kikubwa cha bangi ya hapa nchini ni kushabu, watu wanavuta makapi sio bangi

Kiasi kikubwa cha bangi ya hapa nchini ni kushabu, watu wanavuta makapi sio bangi

View attachment 2068813

Kushabu/Koshabu ni bangi ambayo haijakidhi viwango, unaweza kusema ni makapi pia. Ni kama mabaki ya kaya baada ya kutoa grade ya kwanza ile yenyewe, Inakuaga ina vimbegu na vijiti vingi mno... haina stimu, kelele nyingi, ukivuta utaishia kuumiza kichwa, kuwa mkali, n.k.

Ndio aina ya bangi ambayo huuzwa kwa kiasi kikubwa sana, sana, sana hapa nchini. Ni nadra sana kukuta sehemu wanauza high grade

Wengi wakivuta siku ya kwanza watalia ni vipofu kumbe wamesahau kuwasha taa, hukimbia mawingu, hubeba toroli badala ya kusukuma, hutukana ovyo ovyo, n.k. hii ndio gharama ya kuigiza uchafu kichwani

Ukizoea sana kushabu tayari wewe kichwa panzi, unaweza kuwa kichaa kabisa

Wanaokula kushabu ni masikini wanaoshindwa kupata grade one aidha hawana pesa au hawana maarifa ya kujua viwango wao wanavuta ilimradi iwe bangi tu.

Usije kujidanganya kwamba bangi unayovuta hapa kwetu ni sawa ya wanayovuta huko Marekani, Jamaica, n.k. huko watu wanavuta bangi na sio uchafu ndio maana huji kusikia mtu kawehuka, sijui akili zimemtoka, ana ropoka ropoka, n.k. Kazi ipo huku ambako hata wakulima wa bangi kwenye uvunaji hawajui mbinu za kuvuna vizuri wao wanakurupuka tu, nae muuzaji anaenunua kwa wakulima hata hana elimu ya huu mmea yeye anauza tu ilimradi apate pesa, nao wanunuzi ndio wahanga wakubwa hawajui hata kama wanauziwa kushabu matokeo yake ndio haya mnayoyaona mtu akivuta bangi siku ya kwanza ha tofauti na mwehu, nadhani hata kina afande sele wanavuta kushabu wakijinadi kwamba wanavuta yenyewe matokeo yake ndio kuvua nguo kwenye steji na vituko vingine kibao ambavyo huwezi kuja kuvisikia huko nchi ambazo hawavuti kushabu.

Bangi bangi tu , utofauti wa skanka Na kushabu nikule mzigo unapotoka kwa mkulima.
 
Hahaha

Siku hizi madem wengi mjini wanavuta skanka

Wanasema wakipiga wanajisika burdan

Ova
Yeah mkuu,,, ila wale kaka zake mama/wajomba wakijua unayo skanka hata ya kuvuta tu mwenyewe wanakupa kesi ya uhujumu uchumi wakati hii ni starehe kama zilivyo starehe nyingine
Ova,,,
 
Jay Z nae kaamua kujiajiri kwenye bangi.

Hii brand yake[emoji4][emoji116]
images-635.jpg
images-639.jpg
images-638.jpg
images-637.jpg
 
Unavutia bangi nyuma ya choo,
Unavuta bangi hujala,
Unavuta bangi mchana jua la saa6-8 ,
Unavuta bangi una stress,
Unavuta bangi ya kugongea,
Unavuta bangi ili ukafanye fujo,
Unavuta bangi ili ukabebe vitu vizuto[emoji23]
Kwanini usichizi hakuna kushabu wala nini ni life style yako tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom