Mbuyimayi
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 575
- 1,156
Walio kuwa wanaishi katika hilo eneo walikuwa wakiabudu na kuitukuza miungu, mabaali na maashera hivyo Mungu ndio akamua kuwapokonya nchi yao na waangamizwe pengine wakawe fundisho kwa wale wa aina hiyo. Kwa nini wao mulize Mungu.
Kuhusu Israel uzao wa Yakobo kuwa taifa teule pia muulize Mungu ilikuwa vipi akaamua manabii kupitia katika uzao huo. Hata yeye Mungu/Bwana Yesu kuja duniani alizaliwa katika uzao wa Daudi myahudi? Maana kama Bwana Yesu angezaliwa katika uzao wa wagunya kwa mfano penginepo wagunya ndio wangekuwa taifa teule.
Ni wazi shetani naye ana watu ambao ni taifa teule lake na kwa hila zake akataka kujinasibisha na hilo taifa teule la Mungu.
Muhimu ni kujitahidi kuzishirikisha na kutumia akili zetu hizi za uwanadamu maana tutawajua kwa matendo yao ila hapo sasa unafiki na ugumu wa nyoyo za binadamu kuukubali huu ukweli mchungu ndio inakuwa kimbembe.
Nakuelewa sana mkuu na huu mtizamo wa aina yako ni wa wengi lkn kama nilivyotangulia kusema katika hizi zama ni kweli hatuwezi tukafikiria ktk namna tofauti na huru zaidi kuliko kuegemea ktk tu nchi ya ahadi na dhana ya kupewa na mambo ya kubarikiwa
Sisemi nani yupo sahihi lakini dhana ya kumuondoa mtu eti tu tulipewa na mbaya aliowapa alijua hapo kuna watu na italeta mgogoro wa miaka na miaka na mbaya zaidi aliowapa akawapa ulinzi Wa kusema wamebarikiwa na watakao wabariki nao wanapata baraka dah, hii dhana ya baba muumba kuwapa ubora 'race' fulani tu ina maana tayari kaweka matabaka hapo ndo nauliza why?
Wapalestina na Waisrael wote wana changamoto zao kama jamii na wana matendo yao yaliyo chanya na hasi katika historia zao
Mfano sisi Waafrica bado tunaamini kwa wengi wetu mambo ya kulala mwanaume na mwanaume sio sawa lkn kuna 'parade'zinafanyika Tel Aviv Israel kusheherekea hilo sasa kama baraka ipo ktk 'race '/ jamii yote ya Israel na baraka zao ni zao la kukuabudu mungu mmoja nae kapinga kupitia hivyo vitabu matendo hayo sasa hapo baraka zinasimama kwa matendo yao au ndo uzao tu na vyoyote vile umaalumu wao wa kipekee upo wp hapo kuliko jamii zote ulimwenguni ?
Pia Wapalestina wana mapungufu yao tu mengi kulingana na mitizamo yao lkn kubwa dunia nzima kutumia maandiko matakatifu kutatua tatizo hilo naona kama sio suluhu ni ku 'block' mawazo na njia mbadala za kuleta amani hapo maana wote wana haki ya ukaazi hapo
Ktk zama hizi za 'Enlightenment ' dhana ya tulipewa na baraka sijui au 'superior race' nikurudi nyuma ktk 'giza' tujifunze kupendana kama binaadam kwa ujumla wetu