Kidini unaruhusiwa kumuoa mtoto wa nje ya ndoa - Sheikh Kulunge

Sheria ya kutompa nasaba mtoto wa zinaa ilikuwepo kama adhabu na deterrent kwa wazazi ili waogope kufanya ngono zembe. Sasa inakuwaje hiyo adhabu igeuke kuwa fursa ya baba kumuoa binti yake mwenyewe?

Adhabu kiaje?
Ndoa sio adhabu Mkuu. Ni makubaliano. Kama binti kampenda. Why not wakati sheria haiwakatazi?

Kumbuka Ndoa ni suala la kisheria. Halihusiani na damu
 
Adhabu kiaje?
Ndoa sio adhabu Mkuu. Ni makubaliano. Kama binti kampenda. Why not wakati sheria haiwakatazi?

Kumbuka Ndoa ni suala la kisheria. Halihusiani na damu
Huyo ni binti uliyemzaa wewe, anakujua kama baba yake wa kibiolojia tangu utotoni. Kisaikolojia, hawezi kuwa na maamuzi huru mbele yako kwa sababu ya nafasi uliyonayo kwake kama mzazi. Unaposema kama binti amependa, unajua kabisa kisaikolojia hiyo inaitwa grooming au manipulation ya mtoto wako mwenyewe?
 
Sheria ya kutompa nasaba mtoto wa zinaa ilikuwepo kama adhabu na deterrent kwa wazazi ili waogope kufanya ngono zembe. Sasa inakuwaje hiyo adhabu igeuke kuwa fursa ya baba kumuoa binti yake mwenyewe?
Tunaomba ufafanuzi sasa.
 
Kuna Masheikh na Shehena hili ni shehena kabisa. Sidhani kama akiulizwa athibitishe hoja yake Quran na Sunnah kama anaweza. Maana Waislamu tumeachiwa vitu viwili ambavyo tuliambiwa tukivifuata hatutapotea, navyo ni Quran na Sunnah.

Wangemwambia alete ushahidi wa kutoka sehemu hizo, kama ni hadithi alete iliyomo ndani ya vitabu sita vya Sahih kuthibitisha hilo.

Kwenye dini nilishakataa katakata kusikiliza maneno ya mtu anayejiita kiongozi wa dini akiyaita mawaidha, nafuata vitabu na maamrisho tuliyoachiwa. Siku hizi watu wanaongea wasikike wameongea na si kulingania imani
 
Astaghifilullah!Laana kum!
 
We sema tu unataka kusikia P.funk na Diamond wametafuna mabinti zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…