Ndugu, jitahidi kuwa na hekima na busara walau kwa muda mfupi!! Nakuona umejaa kejeli, husuda, ubinafsi, majivuno,ujuaji ,chuki, sifa ,dharau n.k kuhusu wanawake, kwa kifupi umeathiriwa na mfumo dume!!! Huu ni ujinga na unaweza kuondolewa kwa kuelimishwa.
Huwezi kuwadhalilisha mama zetu,dada zetu ,bibi zetu na shangazi zetu halafu tukuache tu eti kisa ni 'mwanafasihi nguli' (kwa unavyojiita na kujipachika )??? Au wewe mwenzetu umezaliwa na mwanaume?? Hivyo vitabu vyote ukivichunguza kwa kutumia fikra tunduizi na kwa umakini wa hali ya juu ,utakuja kugundua vyote vimejaa mfumo dume.
Angalia jamii za Mashariki ya Kati (Wayahudi ,Waarabu,Waajemi n.k) zilikuwa zinamchukuliaje kiumbe anayeitwa mwanamke katika mila na tamaduni zao kwa nyakati hizo, ukitoka hapo nenda Ulaya,Asia,Afrika n.k.
Swali: Unaweza kuzitenganisha vipi mila ,tamaduni pamoja na dini??? Usijibu kwa kutumia mhemko,tumia fikra tunduizi!!!
Ujumbe: Mpe heshima yake mwanamke (mama yako) ambaye Amekubeba kwenye tumbo lake au wewe mwenzetu hukubebwa kwenye tumbo??