Hayo matango usiniambie.
Nililima mwaka juzi yakazaa balaa.
Bei ndogo hasara silimi tena labda kidogo ya kula.
Nimejaribu kulima mazao mengi sana nyanya, vitunguu, tikiti, mahindi, alizeti, mihogo, hoho, viazi lishe, pilipili mbuzi au habanero au mwendokasi.
Nimelima ndizi, papai.
Sasa napanda minazi mingi sana.
Kilimo unatakiwa ujue soko lako, muda sahihi, eneo sahihi na kiwango cha kulima kwa usahihi. Ukikosea kimojawapo ya hivyo tu utakichukia kilimo wakati mazao hayo hayo wenzio wanapiga pesa ndefu.