Umepaniki Mkuu..
Seriously..!! Kutokuwepo kwenye system ndio justification ya unaowatuhumu kuwa ni wapumbavu..
Typical promotion of selfishness.
Pole sana manake, mosi inaelekea wala huelewi hoja hasa ni nini hapo?!
Pili, unless nawe kama upo kwenye system au nawe ni mwanasiasa vinginevyo inaelekea pia hujui ubinafsi wa wanasiasa!!
Inaelekea hujui kwamba wanasiasa wetu wanaingia kwenye siasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na sio ya umma!!!
Inaelekea hujui wanasiasa wengi wanasukumwa kufanikisha mambo yao kuliko ya wale waliowachagua!!
Hivi watu wazima na watoto wao nyumbani wanafikia hadi kuomba kura kwa kupiga magoti lakini bado unaamini wanalilia kura kwa nguvu kiasi hicho ili wakakuhudumie wewe?!!
Sasa ukishayajua hayo utashangaa kuona wanasiasa walio kwenye sytem wakifurahia kubaki madarakani?!
Hivi Mbunge wa CCM atajali kuona miswada ya kijinga wanaipitisha kwa kura ya ndiyooooo simply because ni miswada iliyoletwa na serikali yao, huku na yeye anapiga posho yake kama kawaida?!
Hivi leo Wabunge wa CCM watajali akitokea mwendawazimu mmoja miongoni mwao akataka mishahara na posho zao zipande kwa 100% na muhula wa ubunge upande kutoka 5-7 or to 10 years wakati hiyo itamuongezea ulaji ambao ndio hasa wanaufuata bungeni?
Sasa na yule mwenzangu mimi anasherehekea nini kwa kuwa na bunge la chama kimoja litakalotumika ku-endorse miswada mbalimbali bila kujali kama ina maslahi kwa wengi au hapana?!
Au anasherehekea kuwapa watu rungu la kwenda kupitisha miswada ya kijkinga?!
Na lau kama ungekuwa unajua kusoma between the lines ungejua nimeongea kauli hiyo kwa uchungu wa kuona wanasiasa wanajali maslahi yao zaidi kuliko ya wananchi ndo maana wapo tayari kufanya lolote kuhakikisha wana-retain madaraka huku wananchi wa kawaida wakishangilia kama mazuzu, wakati si ajabu wengine hata ajira hawana!!!!
Na ikiwa kauli kama hii:-
Kama upo kwenye system basi shangilia kuendelea kupata fursa ya kuitafuna nchi manake hicho ndicho wanachojua CCM lakini kama haupo kwenye system basi narudia ni upumbavu kufurahia kwa mbwembwe kuwa na bunge la chama kimoja!!!
Kama kwako kauli kama hiyo ina-sound selfishness then you have a very very long way to go hadi kufikia kuelewa hoja mbalimbali!!