Kiingereza ni majanga kwa Rais wetu

Kiingereza ni majanga kwa Rais wetu

Status
Not open for further replies.
Hii thread inamdhalilisha Raisi

Haimdhalilishi ila yeye ndiye anajidhalilisha kuongea lugha asiyokuwa na ufasaha nayo wakati angeweza kuongea Kiswahili au Kisukuma na zikatafsiriwa kwa kiingereza.

Kwahiyo post hii ni kama inampa taarifa tu kwa sababu mleta post hawezi kwenda Ikulu kumueleza jambo hili,---- na hii ndiyo faida ya huu ukumbi na wapo wahusika bila shaka watamfikishia hizi taarifa.

Na kumbuka kutojua Kiingereza siyo fedheha bali kuongea kulazimisha kuongea lugha usiyoiweza wakati zipo zile unazoweza hapo imekaa vibaya.😁😁
 
we una angalia kingereza embu angalia alichoenda kukifanya kule malawi kina faida sana kwa taifa ndugu,.... swala la upanuzi wa bandari ya mtwara litaleta ajira kwa vijanaaa, miji kama ya nyasa itachangamka sanaa kibiashara,... ujenzi wa HEP project ni faida pia kwa taifa ..kingereza sio issue bro ata putin hajui english
Shida miradi yake inakuaga ya maneno tu.rejea Bomba la mafuta
 
Unajua Mkuu nimetembea huko vijijini kuanzia Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Mbeya, na Tanga kwa kama miezi mitatu hivi nimekaa na wakulima, kwa kifupi mazao mengi yanaharibika shambani. Barabara hazipitiki misimu flani Ukosefu wa mbolea, Tractors, vifaa vya irrigation. Ila uwezo wa Tanzania bado ni mkubwa. Tatizo lingine ni soko unavuna mahindi halafu hakuna soko, unakata tamaa. Mwaka ujao haulimi tena kwa nguvu. Kuna matatizo mengi yanayoweza kutatuliwa tukiwa makini.

Ni kweli unayoyaongea. Mimi ni bwana shamba, na kwa kweli huwa inaniudhi sana kuona mkulima anaposafisha shamba, kulilima, kulipalilia, kuweka mbolea ya mkopo na hata kupiga dawa huwa yupo PEKE YAKE na hamna anayemsaidia. Ila AKIVUNA. Hapo ndio utaziona road blocks, ndipo utaona ushuru na tozo za kila namna, utaziona marufuku za kuuza mazao yake nje ya eneo fulani, ghafla kuna wasomi na viongozi wenye hofu na maono kuwa huyu mkulima asipodhibitiwa ataishia kuomba asaidiwe chakula au anamaliza chakula kwa ajili ya sherehe za kumtoa binti yake nje. Mkasa huu huwa unawakumbuka SANA walimaji wa mahindi. Hatusikii marufuku kwa walimaji wa viazi vya chips au mbogamboga. Ni kweli kwamba Ukanda wa Nyanda za juu Kusini peke yake unatosha kuuza mahindi yetu hadi Sudan ya Kusini bila hata kuwa na upungufu humu ndani. Lakini haya ni mambo ya kiuongozi na sera, yapo nje ya taaluma yangu.
 
Kama huwezi umejuaje kama na yeye hawezi. Kiuhalisia Mimi sjaonaga mtanzania anayeongea kingereza straight. Hichi kingereza tunajifunza tuu ili kutusaidia kwenye baadhi ya mambo mfano biashara, kusaini mikataba ya kimataifa, ushirikiano wa kimataifa na international cooperation Kwasababu imechaguliwa kama lugha ya Umoja wa mataifa duniani. Kwasababu wanaongea kingereza straight ni waingereza tu. Ambako ndio asili ya kingereza. Onaga hata wanaigeria wanachapia. Accent yao haiendani kabisa na kile kingereza straight. Ilimradi anachozungumza mtu unamsikia na yeye anakuelewa inatosha. Mbona hata watanzania wengi ambapo Kiswahili ndio asili take Kinawazingua.
Mimi siwezi ndo maana naongea full kiswahili.
 
Ndio nchi ya watu zaidi ya 18 milioni. Hawazalishi chakula cha kujitosheleza wakulima wa kusini wa mahindi, mchele, mbaazi, mihogo, njegere nk wanaweza kupata soko la kudumu.

Nini kinakushangaza? Kwamba Wamalawi pia ni binadamu wanahitaji chakula? Ila hawana uwezo wa kujitosheleza, sisi tunaweza kuwapa chakula kizuri bei poa. Win win situation tatizo wapi?

Ukizunguka hapa kwa majirani, soko ni kubwa sana Kenya 50m, Rwanda 12m, Burundi 10m, South Sudan 12m, Zambia17m, DRC 90m tumeisaidia sana kupata amani. Jumla watu zaidi ya millioni 200 wanahitaji chakula chetu, kupititia kwetu.

Hatujaenda Nigeria, Saudi, Qatar, Dubai, China, India, German, UK, USA, Canada, France?

Kama tunaweza ku-leverage these natural advantages tutawakomboa wakulima wetu. Tuanze na majirani.
Haaa.....ila sijasikia maongezi ya maana zaidi ya kuzindua kiwanda cha tumbaku
 
Jamani Rais wetu bora aongee kiswahili tu. Everyone have ndo nini?
Ni kweli Ila kadri anavyokizungumza zaidi ndo anakuwa mzuri,Mimi sioni Kama tatizo lake kubwa ni lugha Ila kwa mtanzamo wangu tatizo lake kubwa ni UWEZO,uwezo wa Kujenga hoja na kuitetea either kwa kutumia hiyo broken English au kiswahili au kisukuma ndo hana, Ila lugha hiyo ni petty issue
 
Kama huwezi umejuaje kama na yeye hawezi. Kiuhalisia Mimi sjaonaga mtanzania anayeongea kingereza straight. Hichi kingereza tunajifunza tuu ili kutusaidia kwenye baadhi ya mambo mfano biashara, kusaini mikataba ya kimataifa, ushirikiano wa kimataifa na international cooperation Kwasababu imechaguliwa kama lugha ya Umoja wa mataifa duniani. Kwasababu wanaongea kingereza straight ni waingereza tu. Ambako ndio asili ya kingereza. Onaga hata wanaigeria wanachapia. Accent yao haiendani kabisa na kile kingereza straight. Ilimradi anachozungumza mtu unamsikia na yeye anakuelewa inatosha. Mbona hata watanzania wengi ambapo Kiswahili ndio asili take Kinawazingua.
Wanaccm bwana shida kweli,hao watanzania unataka uwaone kwenye mikutano ya ccm,je unajua Kama Kuna watz wanaongoza makampuni huko US and they flow like Americans?jamani elimu Kwanza then ukada uwe second
 
Wote mnaomtetea ni wapuuzi yaani Rais anatema yai bovu vile bado mnamsifia badala ya kumwambia ukweli kuwa mzee hujui jaribu kisw
 
Watanzania na sisi tumezidi jamani, muhimu kuelewana. Lugha ni kwaajili ya mawasiliano na hapo wamemuelewa hadi na makofi wamepiga. Hilo ndilo la msingi.
Kumbe wakati mwingine unakuwa na busara.

Hongera
 
Kama huwezi umejuaje kama na yeye hawezi. Kiuhalisia Mimi sjaonaga mtanzania anayeongea kingereza straight. Hichi kingereza tunajifunza tuu ili kutusaidia kwenye baadhi ya mambo mfano biashara, kusaini mikataba ya kimataifa, ushirikiano wa kimataifa na international cooperation Kwasababu imechaguliwa kama lugha ya Umoja wa mataifa duniani. Kwasababu wanaongea kingereza straight ni waingereza tu. Ambako ndio asili ya kingereza. Onaga hata wanaigeria wanachapia. Accent yao haiendani kabisa na kile kingereza straight. Ilimradi anachozungumza mtu unamsikia na yeye anakuelewa inatosha. Mbona hata watanzania wengi ambapo Kiswahili ndio asili take Kinawazingua.
Umeeleza meeengi kwa utetezi kiduchu.Kuielewa lugha ni muhimu.Kutoelewa tusentensi twepesi kwa mtu aliyetumia miaka zaidi ya theluthi mbili ya maisha yake kujifunza lugha hiyo ni ukilaza.Hakuna utetezi wa hivyo.Lugha kipaji.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom