Kiinua mgongo cha Wabunge chashushwa toka Milioni 238 kuwa Milioni 130!

CAG anahusikaje katika hili?
 
Ikiwa habari hii ya kweli basi nitakuwa na furaha ya ajabu wiki hii, na kwa kuonyesha msisitizo nakwenda kufanya booking sasa hivi kuja kula EID home sweet home Tanganyika weraa weraaa
 
Wangewaambia kabla ya miswada ya mafuta na gas ingefanyika collabo ya hatari lakini ccm watajuta..
 
Na baba Ritz atakuwa ametundea HAKI wadanganyika pale atakapo waruka kwa asilimia 100,kwa kutosaini ule MUSWADA FEKI wa GAS na PETROL

Hili swala la mafao limepelekea Kigwangala kuomba mwongozo asubuhi kwa mwenyekiti wa bunge ila alichoambulia nikuambiwa linashughulikiwa. Maskin Kigwangala anataka hayo mafao kwa kila njia.
 
Wabunge wa CCM hata MKIGOMA au hata MDODOMA na potelea mbali iwe MIRINGA kama siyo MSHINYANGA, bado mtarudi tu kwa KIKWETE maana Kikwete ndiyo Mwenyekiti wenu hadi uchaguzi utakapofanyika.

Msumeno hukata mbele na nyuma - YOUR TURN.

 
Kingwangala ela yote ameimalizia kuzunguka kutafuta wadhamini wa Urais,,Jimbo lake la Nzega Bashe atalichukua kiulaini teh teh teh

Hatari kashafulia tayari na alichokua anakitarajia ni hayo mafao alipopata hzo tarifa alipanic mpaka akaomba mwongozo.
 
Kama hao wabunge wana msimamo kesho wagomee speech ya JK kuvunja bunge. Wakienda nitawaona vilaza wa mwisho wa dunia.
 
Hata hiyo milioni 130 ni pesa kubwa sana kwa uchumi wa Tanzania.
Leo kuna watu waneitumikia serikali kwa miaka zaidi ya 40 lakini kiinua mgongo chao hakifiki hata milioni 50 sembuse hao wa miaka mitano tena huku wakipata mishahara,marupurupu,posho na mikopo mikubwa na yenye masharti nafuu!!!
 
Wakiendelea kutunisha misuli zaidi tunawakokotolea mafao yao kwa formula ya wafanyakazi wa kawaida ya kiinua mgongo (severence pay) as per ELRA No. 6 of 2004 Section 41.

(Daily Wage x 7) x years of service

(120,000 x 7) X 5

840,000 x 5

= Tsh. 4,200,000

Haya, wachukue hyo 130M kabla hatujaghafilika chaap.
 
Bongowood!
 
Hili swala la mafao limepelekea Kigwangala kuomba mwongozo asubuhi kwa mwenyekiti wa bunge ila alichoambulia nikuambiwa linashughulikiwa. Maskin Kigwangala anataka hayo mafao kwa kila njia.

Wezi tu hawa.Waache wamalizane,hawana ubavh wa kumsusia Baba Ritz.
 
Haa haa haa mh. Rage alichekelea sana, sasa nahis atakuwa akiongoza mgumo wa kumsusia raisi
 

Nakuapia wabunge wa ccm hawana ubavu wa kugomea hotuba ya raisi wao. Wanaelewa fika Kikwete akikabidhi madaraka ya serikali atabaki kuwa m/kiti wa chama kwa muda na majina ya wabunge wote watakaogomea hotuba ya raisi kwa kupunguzwa viinua mgongo vyao majina yao hayarudi. Nafasi watakayobaki nayo ni kujiunga haraka Act ya Zitto wagombee vinginevyo ukawa hawana nafasi zote zimejazwa.
 
Hahahahaha,kina LETICIA NYERERE walibaki ilikutetea huo mtonyo sasa sipati picha wapo kwenye hali gani.
 
Nani anajua kanuni ya kukokotoa mafao ya wabunge? Kwa nini kuwe na kutofautiana mara 238 mara 130 CAG kapendekeza. Yaani mtu mmoja tua anamua wapewe kiasi gani bila mwongozo wowote?
 

Ni kubwa mno na hawaistahili kabisa.

Hao sana sana wanayostahili labda ni milioni 10 ingawa hata hizi bado ni nyingi vilevile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…