HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Hakimu alimtia hatiani mshtakiwa kwa kigezo kuwa alikiri kosa lake, mshtakiwa akikiri kosa anaweza hukumiwa hata Siku ya kwanza kuletwa mahakamani. Lakini ukiangalia kwa undani kesi hii, inaonekana mshtakiwa alikiri with condition kwamba hakumaanisha kuwa atamuua, hivyo basi hiyo condition ina maanisha hakukiri kosa la kutishia kuua, akipata wakili mzuri anaweza achiwa na kesi kuanza upya huku upande wa mashtaka ukitakiwa kuthibitisha mashtaka ya kutishia kuua.Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.