Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Kijana aliyetelekezwa na mke siku ya harusi atunukiwa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na Waziri Gwajima

Juzi tu mke wangu kanifata nikiwa chakari nimeshindwa kuendesha gari ikabidi nimpigie aje nilipo. Hoja hapa si matumizi ya pombe, hoja ni Tuzo baada ya matumizi ya pombe sehemu isiyo sahihi.

Nikuulize, hapo wizarani kijana aje kwenye mkutano maalumu na mh Raisi wa Jamhuri ya muungano akiwa amelewa raisi akamfukuza kazi utampa tuzo sababu hakuchana mafile wakati anaondoka?
Ni hivi, hata wewe na wenzako kadhaa mkimkuta jambazi anaiba, badala ya kujichukulia sheria mkononi na kumuua ingawa mnazo silaha, wewe na wenzako mkaamua kumfikisha Polisi salama, hakika tutakupongeza tu kwa kudhibiti hasira kali
 
Tunakupenda waziri wetu
Wazalendo hatupingi kila kitu
Mungu awabariki. Bahati mbaya ni kuwa, Hawa wanaopinga hapa, kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia hata hawaji, sauti zao hazisikiki, na hata hawajui kuwa, ukatili wa kijinsia sehemu kubwa ni wali kwenye mahusiano kushindwa kudhibiti hisia za hasira. Watuache tu wapambanaji tunajua kitovu cha adui kuwa ni jazba na hasira.

Acha tukimpata mmoja tumpongeze.

Natoa wito kwa wote wanaotoa sauti kwenye mjadala huu jamani tuungane kukemea JAZBA.... Na kuhamasisha UTULIVU wakati wa mapito magumu yakiwemo ya ghafla ..
 
Ni hivi, hata wewe na wenzako kadhaa mkimkuta jambazi anaiba, badala ya kujichukulia sheria mkononi na kumuua ingawa mnazo silaha, wewe na wenzako mkaamua kumfikisha Polisi salama, hakika tutakupongeza tu kwa kudhibiti hasira kali
Hii ni sawa. Tumefanya jambo zuri, kujichukulia sheria mkononi ni jinai.

Ila, Kama huyu aliachwa sababu kalewa siku ya kukabidhiwa mke na wazazi na akapewa tuzo sababu hakufanya fujo, kwanini madereva walevi wasipewe tuzo wakifikisha magari salama wakiwa wamelewa?

Anyway, binafsi naona kutoa tuzo katika mazingira yake ni kuwaambia wazazi serikali inasimama na walevi wasio na mipaka.
 
Sendoff ni tukio la wazazi kumkabidhi binti kwa mume. Kwa wazazi si mapenzi yale ni tukio muhimu linalohusisha rasilimali watu na fedha ndo maana kuna mavazi rasmi. Mapenzi ni kwenye honeymoon huko.
Jamaa apewe tu tuzo yake kwakweli, inaonekana watu wake wa karibu wanaomzunguka Wana utulivu sana kwenye kufanya maamuzi.
Hiyo pombe anaweza akawa alikunywa kiasi kidogo tu kwa lengo la kuchangamka lakini bahati mbaya ikamzidia..
Hakutakiwa kupewa hukumu hiyo labda kama Kuna jambo jingine halisemwi
 
Hii ni sawa. Tumefanya jambo zuri, kujichukulia sheria mkononi ni jinai.

Ila, Kama huyu aliachwa sababu kalewa na akapewa tuzo sababu hakufanya fujo, kwanini madereva walevi wasipewe tuzo wakifikisha magari salama wakiwa wamelewa?

Anyway, binafsi naona kutoa tuzo katika mazingira yake ni kuwaambia wazazi serikali inasimama na walevi wasio na mipaka.
Hapana siyo hivyo, unalinganisha vitu viwili tofauti. Huu ni ukatili wa kijinsia ambapo, kichocheo kikubwa ni watu 2 kukosa utulivu. Na ukumbuke walikuwa kwenye sherehe na hizo pombe ilikuwa bajeti yao wote hao. Na harusi ni kunywa na Kula. Na wakipeana ahadi ya kuwa wanandoa walijuana. .

Huko kwenye Barabara hakuna sherehe ni kazi.
 
Yule mwamba aliyenyimwa mke siku ya harusi kwa kisingizio cha kwenda kwenye send off akiwa chakari,amepewa tuzo.

Amepewa tuzo ya mwanaume bora wa mwaka na waziri Doroth Gwajima

Kwa kweli jamaa anastahiki tuzo kweli maana mimi mwanamke anikatae siku ya harusi nyumba yao ningeichoma moto

Hongera sana kwako mheshimiwa waziri
Ma mimi mahitaji tuzo
 
Hakuna mzazi atavumilia hiyo dharau. Unamkabidhi binti kwa mlevi? Serious? Kalewa chakari? Hata kuheshimu tu hiyo siku moja muhimu imeshindikana? Kama ni wazazi wameshinikiza Walikuwa sahihi kabisa. Kama wanapendana sana wakafunge ndoa bila hizi taratibu za sendoff.
Safi sana Mkuu,wewe ni kati ya watu wachache sana walioelewa huu uzi kwa kuangalia na upande wa pili,

Hakuna mzazi anayejielewa atakubali mume mtarajiwa kuja kwenye send off kalewa chakari,hiyo ni dharau kubwa sana.
 
Juzi tu mke wangu kanifata nikiwa chakari nimeshindwa kuendesha gari ikabidi nimpigie aje nilipo. Hoja hapa si matumizi ya pombe, hoja ni Tuzo baada ya matumizi ya pombe sehemu isiyo sahihi.

Nikuulize, hapo wizarani kijana aje kwenye mkutano maalumu na mh Raisi wa Jamhuri ya muungano akiwa amelewa raisi akamfukuza kazi utampa tuzo sababu hakuchana mafile wakati anaondoka?
IRrellevant,mwamba kapewa tuxo kwa kuweza kuhimili mihemko na hasira za ghafla.mimi ningekuwa jela
Safi sana Mkuu,wewe ni kati ya watu wachache sana walioelewa huu uzi kwa kuangalia na upande wa pili,

Hakuna mzazi anayejielewa atakubali mume mtarajiwa kuja kwenye send off kalewa chakari,hiyo ni dharau kubwa san
 
😀😀😀 Haya kwa stori ipi ya kishujaa uliyonayo? Sana umenipa wazo kuwa, kumbe tunahitaji search ya mashujaa wa kudhibiti jazba Ili event ya tuzo zetu ipendeze na kuhamasisha kuwa, maisha bila jazba inawezakana
Itengwe bajeti na hili jambo liwe endelevu kwa mashujaa wengi
 
IRrellevant,mwamba kapewa tuxo kwa kuweza kuhimili mihemko na hasira za ghafla.mimi ningekuwa jela
Wewe ni mtu mkweli kwenye hoja. Nawe ni Shujaa wa ukweli.

Unajua tulipofika sasa kwenye jamii yetu tunahitaji pia mashujaa wa hoja....

Watu wengi wamekuwa wakipotezea hoja ya msingi Ili tu roho zao zifurahi kwa ajenda yao. Dunia haiwezi kujengwa vizuri kwa misingi ya kukwepa ukweli. Wewe umejinenea kweli kabisa na upongezwe tu🤝
 
Jamaa apewe tu tuzo yake kwakweli, inaonekana watu wake wa karibu wanaomzunguka Wana utulivu sana kwenye kufanya maamuzi.
Hiyo pombe anaweza akawa alikunywa kiasi kidogo tu kwa lengo la kuchangamka lakini bahati mbaya ikamzidia..
Hakutakiwa kupewa hukumu hiyo labda kama Kuna jambo jingine halisemwi
Hao watu wake wa karibu na huyo mlevi,wote ndio wale wale tu,wangekua na busara wasingemuacha ndugu yao akalewa chakari siku muhimu kama hiyo,walipatwa na aibu ya ndugu yao kwenda kalewa chakari ndio maana wakawa wapole.
 
Jamaa apewe tu tuzo yake kwakweli, inaonekana watu wake wa karibu wanaomzunguka Wana utulivu sana kwenye kufanya maamuzi.
Hiyo pombe anaweza akawa alikunywa kiasi kidogo tu kwa lengo la kuchangamka lakini bahati mbaya imamzidia..
Hakutakiwa kupewa huku hiyo labda kama Kuna jambo jingine halisemwi
Hahaha, sio kwamba alimshukuru baba mkwe kwa kumpa chombo japo yeye ana sura ngumu?
 
IRrellevant,mwamba kapewa tuxo kwa kuweza kuhimili mihemko na hasira za ghafla.mimi ningekuwa jela
Ukijadiliana na nyapara madhara ya ndoa.
Ukifanya uhalifu unashtakiwa kwa sheria.
Binafsi simtazami huyo kijana kama shujaa anayestahili tuzo kwa kutokufanya uhalifu baada ya kuadhibiwa kwa makosa yake ya kutoheshimu wazaza wa mchumba wake.
 
IRrellevant,mwamba kapewa tuxo kwa kuweza kuhimili mihemko na hasira za ghafla.mimi ningekuwa jela
Wewe pia ungeenda kwenye send off ukiwa umelewa chakari? Huyo mlevi alikua sahihi kwenda kwenye send off akiwa kalewa chakari?

Naona mnashindwa kuangalia chanzo cha tatizo kabisa,

Sasa huyo Mwanaume angewezaje kufanya fujo wakati huo kalewa chakari? Mtu aliyezidiwa na pombe,anatakiwa alale tu,huyo hana cha busara bali pombe zilimzidi.
 
Kususwa au kuachwa kunauma jamani duh!!! Nakumbuka nakaribia kwenda kujitambulisha ukweni ndo mchumba hataki kuongea nami kila KITU ni kigumu , halafu muda mwingine Nakula blacklist, niliumia sana aseeee.unaweza ua,,, ila hiii Dunia Ina watu wapole sana
Duuh,na haukufanikiwa kumuoa mkuu? Em jazia nyama kidogo! Pole sana mkuu Ighughuyi
 
Wewe pia ungeenda kwenye send off ukiwa umelewa chakari? Huyo mlevi alikua sahihi kwenda kwenye send off akiwa kalewa chakari?

Naona mnashindwa kuangalia chanzo cha tatizo kabisa,

Sasa huyo Mwanaume angewezaje kufanya fujo wakati huo kalewa chakari? Mtu aliyezidiwa na pombe,anatakiwa alale tu,huyo hana cha busara bali pombe zilimzidi.
Pia hata kama angefanya fujo angekutana na mkono wa sheria. Hiyo tuzo aliyopewa ni ya kimatukio tu, kutrend na tukio hakuna ushujaa wowote aliouonyesha huyo kijana.

Kama ni kuzuia mihemko ya kutokufanya fujo wapo watu wanasalitiwa na wake zao na kutapeliwa mali zao kupitia mahakama kwa kuwagawai mali baada ya kuomba kuachana kwa amani na wanajizuia hawafanyi ukatili wowote na ni wengi tu.

Ushaona mtu kapewa tuzo baada ya kumfumania mkewe na kuachana kwa kugawana mali kwa amani bila kumdhuru mke?
 
Back
Top Bottom