Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Mkulungwa1 hata kama alikuwa kibaka sheria ipi inaruhusu apewe adhabu kubwa kiasi hicho na wahalifu ambao si mahakama?

Usijitoe ufahamu...acha hoja dhaifu...
 
Mheshimiwa raisi, Mama Samia Suluhu Hassan, sisi wanawake tuna Imani sana na wewe, tutakupa kura zetu zote za urais mwaka 2025 ila kuna mambo machafu sana yanayofanyika katika serikali yako.

Sisi wanawake wa Tanzania tumesikitishwa sana na mauaji ya kijana mdogo mkazi wa kata ya Mabibo kitongoji cha Soweto yaliyofanywa na watu wanaojiita Sungu sungu.

Kijana huyo anaitwa Jumanne Jongo.Ameuawa kikatili sana kwa kukatwa miguu na mikono.

Cha ajabu wauaji wa kijana huyu wanajulikana na hawajakamatwa hata mmoja.Taarifa nilizokuwa nazo bado wameahidi kuua vijana wengine wanaowahisi vibaka.

Genge hili la mauaji ya vijana linaongozwa na watu wanaojiita Sungu sungu kutoka kata ya Jitegemee ,Mabibo wilaya ya Ubungo.

Haya sio mauaji ya mara ya kwanza,huko nyuma sungu sungu hao wa Jitegemee wameshawahi kuua vijana wengi kwa kisingizio kuwa vijana hao ni vibaka.Hata kama ni vibaka kwa nini wasiwakamate na kuwapeleka Polisi?

Kwa nini sungu sungu wanajichukulia sheria mkononi?

Mh.Rais nchi yako ni nchi inayofata utawala wa sheria, iweje wapumbavu wachache watie doa uongozi wako?

Taarifa nilizokuwa nazo mauaji hayo yanapata baraka kutoka katika uongozi wa serikali ya mtaa wa Jitegemee chini ya mwenyekiti Kilema.

Hivi OCD wa Kinondoni hana taarifa ya tukio hili? Mpaka sasa hivi amechukua hatua gani? Anapata kigugumizi kipi cha kuwakamata wauaji hao wakiongozwa na mpumbavu mmoja anayeitwa Samwel?

Kwa taarifa yako mh.rais sisi wanawake wa Mburahati na Jitegemee tumeguswa sana na kifo cha huyu kijana, tunatafakari mara mbili mbili kuwa wanachama wa CCM.

Embu ukiwa kama rais tumia mamlaka yako kushughulikia suala hili.Maana sisi wanawake wenzako tuna wasiwasi sana kuhusu maisha ya watoto wetu wanaouawa kila kukicha na hawa watu walio juu ya sheria wanaojiita Sungu sungu.

Kuna hoja kwamba huyu kijana alikuwa kibaka,lakini sheria inasemaje? Kwani hukumu ya kibaka mauaji?

Chonde chonde mh.Rais fanyia kazi suala hili ikibidi mwajibishe kamanda wa Polisi wa Kinondoni kwa kushindwa kuwakamata hao wauaji wa huyu kijana.

Umaskini kitu kibaya sana,huwezi kusikia madudu ya sungu sungu huku kwetu masaki,oysterbay,upanga,kisasa,
Haya madudu yapo uswahilini tu,
 
hiyo Sura tu ina onesha n mmoja wa hao vibaka wasumbufu wa hapo mtaani


mimi kibaka akiingia kweny 18 zangu lazima nimtangulize makao ya milele iwe kwa upanga au moto
 
Nyinyi waropokaji bado hamjanipa kifungu cha sheria kinachoruhusu kujichukulia sheria mkononi....kwa akili zenu fupi nini kazi ya Polisi ,mahakama na magereza?
Mama waizi hawajaanza kuchomwa/kuuwawa leo kama una mtoto unae mpenda lakin ana tabia chafu za wizi kaa nae na umuonye ikiwezekana muhamishe mazingira ili asiwe karibu na hao marafiki maana mwizi rafiki yake ni mwizi.

Ukiendelea kutetea kwa kuuliza vifungu vya sheria ipo siku msiba utakukuta na bahati kundi la wananchi likiamua kumuua mwizi hapo hamna kesi jalada linafunguliwa na kufungwa fasta halikai hata siku mbili. Hiyo inaitwa kauwawa na wananchi wenye hasira kali itabaki unaulizia sheria zinasemaje ila umeshakosa mtoto.
 
Arovera nchii hii ni ya utawala wa sheria...kaa ukijua je upande wa pili wakiamua walipize kisasi itakuaje?

Huyo Samwel jela inamuhusu....
 
Ndugu niache Mimi.Nioneshe kifungu Cha sheria kinachowapa mamlaka sungu sungu kuua?
Mimi sitetei mauaji ya hovyo, lakini sheria zipo kwa ajili ya wakubwa tu.
Wanyonge wanakabwa, kuibiwa na watoto zenu wakikamatwa kesi mahakamani ni mzunguko weeee wanataka evidence wakati mmeamkamata mwizi "readyhanded".
Kwangu wameniibia pikipiki kwa Kuvunja Fence nimeripoti polisi wala hawahangaiki.
Sasa nimenunua mshale wenye sumu nikimkuta mwanao usiku mbaya ndani ya uzio wangu najua ji mwizi namdungua mshale kimya kimya, mwanzoni waliniibia kuku wangu wa kienyeji kibao yani sasa hivi pikipiki ya 285,000,000.
Wakileta vitu vya dhuluma nyumbani mnachekelea wakati kuna mtu kaumia.
Wezi wamenirudisha nyuma sana sasa hivi napiga ng'ondi kwa mkuu hadi kazini maana kipato kidogo siwezi kugharamia boda boda kila siku.
 

Iam Lucha hamna kitu kama hicho...kwa hiyo tufute jeshi la polisi na mahakama,magereza?

Tuache sungu sungu wakijichukulia sheria mkononi?
 
Ndugu sinajinasasa kwa akili zako tufute polisi,mahakama na magereza tuwaache sungu sungu wajichukulie sheria mkononi?
 
huyu dogo jumanne taarifa zilizo nifikia kuwa.mwizi wa pikipiki na kukaba watu.

kituo cha mburahati kilitoa baraka kwa kumchoka kwa matukio yake na popote hakipatikana kifo.

kesi imeshafungwa mburahati.

maaana RB nyingi hapo mburahati zimekuwa nyingi
Hakuna namnaa wauwawee tu,wanalostisha Sanaa alafuu mama zao na dada zao wanakuja kuwatetea hapa kwa kutumia gender upuuzi mtupu.eti mama Samia Sasa raisi atafatilia Hadi issue ya vibaka wadogo wadogo kama hawaaa
 
Ni ujinga na upungufu wa akili kuua Binadamu wenzetu kwa kigezo eti ni Kibaka. Uhai wa mtu uulinganishe na kitu?
Hata Kama Mtu kaiba kiasi gani bado kuna sehemu maalum za kumpeleka au kumshitaki na akawajibishwa.
Eti mtu kaibiwa sijui taa ya gari tu au kuku, basi akimkamata huyo mwizi ni kuua huo ni upumbavu na roho ya kimaskini tu.
Vitu vinatafutwa Lakini uhai hautafutwi. Tuache kuhalalisha mambo ya kipumbavu kwa sababu za kimaskini tulizonazo
 
B'REAL hasira zako za ugumu wa maisha umalizie kwa mtu anayedhaniwa kibaka?

Kama una hasira kweli nenda kaue wauzaji unga, mafisadi au kaue viongozi wala rushwa.

Acha ujinga.
 
Mh.Rais SSH amesema "wazazi wajitahidi kulea watoto wao vyema"....

Mzazi anaacha mtoto wake alelewe na mitaa....maumivu huja baadaye....

#MaadiliKwanza
#SiempreJMT
 
Nilishawahi kuibiwa VITU VYANGU nikaripoti polisi....baadaye Mzee wa huyo kijana mwizi akanitangazia ubaya mtaani....kwa sababu ya kiitwacho "uzawa"....

Mkewe akasema kuwa WAMESHAZOEA KUMTOA KIJANA WAO VITUONI MARA KWA MARA KWA HIYO NITAJISUMBUA TU MWENYEWE.....


Wazazi wakumbuke wajibu wao kwa watoto wao....kumpenda mtoto ni kumfundisha TABIA NJEMA kwani hii dunia ni ngumu mno na inahitaji "mental strength" zaidi ya UZWAZWA NA MAZOEA YA KIJINGA......

#MaadiliKwanza
#SiempreJMT
 
Nyinyi ropokeni tu...kaeni mkijua mnachofanya ni unyama wa Hali ya juu...unawezaje kumuua binadamu mwenzako kama unaua paka?

Kama mna hasira nendeni kuua wauza madawa ya kulevya,wala rushwa na wahujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom