Asante sana mkuu tatizo vijana wenzetu Hawa wanaolia Lia humu asilimia kubwa ya changamoto zoa zimesababishwa na wao wenyewe bila kujua.Umeelezea vyema kabisa mkuu, modern women kuendana nae na uifurahie ndoa yapasa ukubali uhalisia mapema kabla hata ya kumpata na kumuoa vinginevyo utajitaftia matatizo matupu.
Mtu anaoa/kudate na mwanamke mwenye degree na exposure ya vitu Kibao, halafu eti anataka kuishi na mwanamke huyo kama ambavyo angeishi na Kuruthumu aliyeishia Form Four B Tena shule ya Kata.
Kama wewe unaamini kwenye patriarchy basi tafuta mwanamke ambaye amelelewa kwa kuamini kwenye mfumo dume(asili) mbona wapo?
Mwanamke A: hivi unajua kwenye jamii yetu wapo wanawake ambao wewe mwanaume ukimpa uhakika tu wa Kula ubwabwa na maharage Kila siku iendayo kwa Mungu halafu ndani Kuna king'amuzi Cha Azam ambapo Kila akimaliza kupika na kuosha vyombo anakuja kuangalia Sinema Zetu, yeye anaridhika kabisa na wewe mume wake atakutii na kukuona kama YESU na kamwe hawezi kukupa stress za aina yoyote ile?
Mwanamke B: Kwenye hii hii jamii yetu pia wapo wanawake ambao Kila wakilala na kuamka wanakuja na ndoto mpya au mitazamo mipya ya kimaisha.. na mwanamke huyu unakuta anawaza siku Moja kupitia career yake awe na uwezo wa kuzalisha angalau ajira 2,000 kwenye jamii yake na yeye asomeke kwenye FORBES MAGAZINE kama akina Folorunsho Akija, mwanamke huyo unakuta anapanga siku Moja aje afanye Space Tourism..na wanawake wa dizaini hii mahusiano kwao yemebeba sehemu ndogo sana.
Sasa kimbembe unakuta kijana ana muapproach mwanamke B halafu matarijio yake ni ya mwanamke A, Sasa ni nini kitatokea hapo kama sio mifarakano?