Lakini pamoja na mambo yote ya kuogofya yanayoendelea kwenye Tasinia nzima ya mahusiano, binafsi naona Bado mtu akiamua kuoa na kuifurahi ndoa inawezekana....
Ni aina tu ya uchaguzi wa mwanamke unaoufanya.
Ukichunguza kwa makini utagundua hii mifarakano tunayoiona kwenye mahusiano siku hizi ni kutokana na sisi wanaume kuchagua wanawake ambao hawana Tena zile characters au mienendo tunayoitaka.
Wengi tunataka mwanamke ambaye yuko obedient, mwenye nidhamu, atakaeyapa kipaumbele mahusiano yetu na asiyekuwa na tamaa za mambo makubwa makubwa yaliyo nje ya uwezo wetu.... Na mara nyingi wanawake wa dizaini hii hawapo mijini maana Hawa ni conservative women wanapatikana vijijini hukoooo...
Hapa mjini wamejaa modern women ambao ndio Wana hizi sifa ulizozitaja hapa.
Kinachowatesa wanaume wengi ni kumchukua modern woman akitegemea kwamba atakuwa na sifa au ataishi kama conservative traditional women.... Mwisho wa siku anakuja kuwa disappointed tu.
Hawa modern women nao pia wana wanaume wao wanaowafaa na ndio maana pia wanaolewa,.. Hawa modern women hili uweze kuishi nao basi yakupasa uwe gynocentrised kama walivyo akina
Tsh na
Half american na sio wewe mwenzangu na Mimi ambaye Bado una traditional masculine elements.
Ukitaka kuoa na uishi na furaha basi oa mwanamke ambaye ataithamini ndoa na ataiona ndoa inabeba sehemu kubwa ya maisha yake na siku zote ataipigania kuilinda kiroho na kimwili na huwezi kumkuta na sifa hata moja kwenye hizi ulizozitaja hapa na mwanamke huyo ni traditional conservative woman.
Hawa modern women ndoa kwao ni kitu Cha ziada sana na hawaoni ajabu kuipoteza hata kama Ina wiki mbili, wao career na kutafuta hela katika mazingira yoyote Yale ndio kitu kilichopo akilini mwao na kwanza hata kwenye ndoa hizo ndoa zenyewe huwa wanaingia kimikakati kutimiza malengo yao binafsi.
Kwa hiyo kuwa na ndoa yenye furaha kwa Karne hii ni jambo ambalo Bado linawezekana kabisa.