Kwa maoni yangu ndoa ni jambo jema, kuwa mke na familia ni jambo Zuri sana tena takatifu.
Tatizo letu sisi vijana wa siku hizi ni ujuaji mwingi, na tamaa, pia tuna penda sana ngono, starehe ambazo hazina mipaka hivyo kupelekea kushindwa kuchagua mchumba mmoja wa kudumu nae.
Ndoa ni rahisi sana, cha msingi ni kuwa na heshima na kujishusha kwa mwenzio, kuepuka malumbano yasio kuwa na tija , kumpenda mwenzio na kumjali, pia chagua mwanamke au mwanaume unae endana nae.
Ugumu wa ndoa unakuja pale vijana wanaingia kwenye ndoa wakiwa na mahusiano mengine, kwa hili hamtakaa sawa na ndoa itakutoa jasho, acha ku intertain x wako kama unataka kudumu katika ndoa.
Pili acha kuja kwenye ndoa kutafuta pesa , hili wengi wao ni kina dada, ingia kwenye ndoa ili mtafute wote , mpambane kwa pamoja , kwa kufanya hivyo mtadumu.
Epuka ndoa kwa ajiri ya kufanya sex tu , yaani kijana uko kwenye ndoa unawaza sex masaa 24 ndoa itakutoa jasho , cha msingi ni upendo sex ipo tu, focus zaidi kufanya kazi kujiletea kipato ili familia yako ipige hatua, waafrica tuna penda kujisifia sex kana kwamba ni mafanikio, hivyo kusahau nguzo kuu katika mausha ni kazi, hayo mengine ni ziada tu, mfano mimi nilifanya kazi na wachinese for 10 yrs nikiwa nje ya nchi, hawa watu walikuwa wana kuja business trip one year, in one year wana rudi kwao mara moja tu kwa likizo ya siku 30, tena una kuta mchina huyu kakaa africa or Europe or America 5 yrs, kila mwaka anaenda kutaza familia yake mara moja kwa mwaka, ndani ya miaka mitano una kuta kafanya maendeleo ya kutisha na maisha yana songa, bongo mtu wiki moja bila sex ana ona kama ni adhabu ya kifo, so hata akioa au kuolewa na asipate sex just two days ana hisi mke wake yuko vile au ana cheat, ohh simuelewi, haya yote ni mawazo ya kimasikini, ndio maana Africa hatuendelei.