passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,828
- 3,922
Kuna mmoja anakuambia ndoa ni mkataba wa kitapeli lakini haonyeshi mkataba huo utapeli upo wapi ila yeye anasikia tu kwa watu ni mkataba wa kitapeli.huwezi kuwa na chuki kwa jambo jema na lenye heri,changamoto zake zitakufanya uwe na wasi wasi nalo tu lakini sio chuki.
wavulana wanakwambia kataa ndoa,na hawakupi sababu kwanini ukatae😂
Mkuu Loading,Kama huwezi kuwajenga wanawake kuwa wake wema wa baadae sahau wanaume kuoa. Tutapiga mimba na kubakia kuhesabu tuu watoto huko nje.
Mkuu nitake radhi hakuna sehemu yeyote ambapo nimeeleza kukataa ndoa .YESU hakuoa ana sababu za hayo,wala hakuna sehemu alinukuliwa akiinanga ndoa.
yule hakuwa muumini wa mbususu wala mipini kama wengi wenu humu.
sasa wewe hutaki ndoa una sababu zipi??
kila jambo lina vigezo na masharti.hata hao waoaji pia si kila mtu ana sifa za kuoa,wengine ndio kama hawa wa hii kampeni ya kataa ndoa,ipo siku ataoa kwa shinikizo la wazazi,kazi ama jamaa na marafiki halafu asiweze kabisa kutosha humo ndoani.Ndoa ni jambo la lazima tatizo hao wanawake wa kuoa wapo?? Unafunga ndoa katika mazingira ambayo prostitution/ukahaba ni kama imehalalishwa, mke anaolewa kutoa nuksi na fashion akitoka hapo anarudia kudanga kudai divorce na mgawanyo wa mali mahakamani, wanawake wenyewe ni dizaini ya kina Wema, Uwoya na Zaylissa nd
Ndoa sio lazimaNdoa ni jambo la lazima tatizo hao wanawake wa kuoa wapo?? Unafunga ndoa katika mazingira ambayo prostitution/ukahaba ni kama imehalalishwa, mke anaolewa kutoa nuksi na fashion akitoka hapo anarudia kudanga kudai divorce na mgawanyo wa mali mahakamani, wanawake wenyewe ni dizaini ya kina Wema, Uwoya na Zaylissa ndiyo wamejaa sasa hivi kuachana nje nje
Mkuu hebu ainisha hasara ambazo mtu anazipata endapo hasipooa.jamaa hajaingilia uamuzi wa mtu,anasemea kampeni ya kataa ndoa,ndio sababu hata ameainisha aina ya watu anaofikiri wako nyuma ya kampeni hiyo.
ukiamua kukandwa kisamvu ni uamuzi wako,shida ni pale unapotafuta kuungwa mkono ndipo upinzani na mashaka huibuka😂😂.
ndoa ni jambo jema na lenye kupendeza mbele ya jamii,kama yalivyo mengine kama kufanya kazi halali,kutopenda ugomvi,kusaidia watu wenye uhitaji,kujenga nyumba nzuri ya kuishi nk.ni ishara ya kupiga hatua ktk maisha.
kama una mahusiano mazuri au yasiyo na mawaa na bado unahubiri kataa ndoa,bado una tatizo pia😂😂.
hasara kubwa kuliko zote unayopata kwa kukosa kuoa,ni watu kukosa imani na akili zako,kwamba huenda unakua mvi tu ila akili bado ni za vidudu,utadharaulika hata na watoto wa mtaani kwako kwamba hujitambui.Mkuu hebu ainisha hasara ambazo mtu anazipata endapo hasipooa.
Ningependa utoe mawazo bila kuwa biased
Mbona huna hojahasara kubwa kuliko zote unayopata kwa kukosa kuoa,ni watu kukosa imani na akili zako,kwamba huenda unakua mvi tu ila akili bado ni za vidudu,utadharaulika hata na watoto wa mtaani kwako kwamba hujitambui.
sijui utaweza vipi kulibeba hilo lisikuletee madhara no 2,ya kisaikolojia.
baada ya kushinda na hali ya kutojiamini inafatia hatua ya tatu 3,afya ya akili au stress.
hapo unachukia ndoa,unachukia wenye ndoa au wanaopendana na kuishia kuiponda kama wafanyavyo watoto wengine humu jukwaani.
Mkuu hebu rudia Tena kusoma ulichoandika.hasara kubwa kuliko zote unayopata kwa kukosa kuoa,ni watu kukosa imani na akili zako,kwamba huenda unakua mvi tu ila akili bado ni za vidudu,utadharaulika hata na watoto wa mtaani kwako kwamba hujitambui.
sijui utaweza vipi kulibeba hilo lisikuletee madhara no 2,ya kisaikolojia.
baada ya kushinda na hali ya kutojiamini inafatia hatua ya tatu 3,afya ya akili au stress.
hapo unachukia ndoa,unachukia wenye ndoa au wanaopendana na kuishia kuiponda kama wafanyavyo watoto wengine humu jukwaani.
Mkuu Analyse,Mkuu hebu rudia Tena kusoma ulichoandika.
1. Unamaanisha jamii itakuona hujitambui kisa hujaoa??. Nilitoa mfano mwanzoni kuhusu masister na mapadri ambao hawaingii kwenye ndoa, vipi jamii inawaonaje?. Kama ndoa ni kipimo Cha utimamu wa akili na kujitambua, mbona pamekuwa na matukio mengi ya wanandoa kudhuriana
2. Kutojiamini? Umemaanisha nn mkuu? Kwamba watu hawaingii kwenye ndoa sababu wamekataliwa au ni vipi??
3. Stress zinatokana na nini ikiwa mtu ameamua kwa hiari yake kutoingia kwenye ndoa?. Nikuulize swali, kati ya waliooa na wasio oa ni kundi Gani lipo very stressed?
Mkuu desayi,Mbona huna hoja
Sasa mkuu, umekuja na wazo la takwimu alafu unataka mimi ndio nilitekeleze? Sio kwamba wewe hayo maneno yako ndio yangeambata na takwimu??Mkuu Analyse,
Ningependa twende kwa takwimu sasa.
Embu tuletee takwimu za watoto waliolelewa ndani ya ndoa baba na mama pamoja wakaishia kuwa watoto wa mitaani? , halafu tuangalie takwimu za watoto ambao hawakuzaliwa ndani ya ndoa au wazazi walitengana.
Nataka tuangalie kwanini ndoa kuwepo ni muhimu, kwanini lipo ongezeko kubwa la watoto mitaani? Kwanini watoto wanaishiwa kubakwa kukosa uangalizi sababu wazazi hakuna mawasiliano?
Twende taratibu weka takwimu.
Mkuu,Sasa mkuu, umekuja na wazo la takwimu alafu unataka mimi ndio nilitekeleze? Sio kwamba wewe hayo maneno yako ndio yangeambata na takwimu??
Kingine mkuu jaribu kutokuwa biased unapojadili jambo lolote. Hivi aliyekwambia watoto wote wa mitaani wanatokana na watu ambao hawajaoa ni nani?.
Ngoja nikupe baadhi ya sababu kubwa za watoto wa mitaani:
1. Wanaume waliopo kwenye ndoa kuzaa nje ya ndoa zao, hivyo kushindwa kuwakubali hao watoto ili kuokoa ndoa zao.
2. Wanandoa kutalikiana hivyo kupelekea watoto kukosa usimamizi refer dessertation ya Shanny M Malinda yenye title inayosema ''ASSESSMENT OF DIVORCE ON CHILD DEVELOPMENT IN TANZANIA:A CASE STUDY OF KINONDONI MUNICIPALITY'' humu pia unaweza kuona kwamba familia (ndoa) yenye migogoro huwa inapelekea baadhi ya watoto kukosa malezi mazuri na hivyo kupelekea kuondoka nyumbani wakiwa na umri mdogo.
Alafu hapo juu kuna maneno yako nimeyabold, ningependa ujue kwamba kuna watoto wanazaliwa nje ya ndoa ila wanatokana na wahusika waliopo kwenye ndoa. Lakini pia kuna watoto wanaangukia mtaani baada ya wazazi wao ambao walikuwa kwenye ndoa kutengana. Makundi haya yote mawili ni matokeo ya ndoa.