Kuna jambo ningependa nikwambie ndugu mleta uzi. Unajua kitendo cha kupromote ndoa as if watu hawajui umuhimu wake huku ukifumbia macho changamoto zinazotokana na tabia za kisasa za wanaoingia ndoani pia ni aina ya upotoshaji?
Mfano wa kulinganisha na hili swala la ndoa ni issue ya elimu ni ufunguo wa maisha ambapo wazazi waliwakazania watoto wao kuachana na kila kitu katika haya maisha yakiwamo mahusiano na wakazanie shule hadi kufika elimu ya juu kabisa yaani chuo kikuu wakiwaahidi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na kutoboa ni lazima. Fast forward leo, elimu iliyosisitizwa na wazazi ndio imekuwa chanzo cha umasikini na ujinga mara mbili kushinda mtu ambaye hata hajaenda shule.
Hii inakupa picha gani? Kwangu mimi inanipa picha kuwa sometimes unaweza kuwa unasisitiza jambo fulani unalo amini kuwa ni sahihi na ni kweli ni jambo sahihi ila sasa shida ikaja eneo la manufaa, je, hilo jambo lina manufaa kwa walengwa ama la?
Sasa rejea kwenye ndoa, ndoa msingi wake ni kuishi pamoja na kushare kila kitu, kitanda, miili, watoto, chakula, pesa, hisia, ndugu, mapenzi, upendo, yaani hakuna cha binafsi katika ndoa.
Ila unakutana na mifumo ambayo inaleta elements za ubinafsi na zinaharibu sasa mantiki ya ndoa. Nadhani ungewekeza mjadala kuwa ni wapi watu wanapishana uone shida. Wanawake wana tabia zao ambao wanazileta kwenye ndoa na zinazaa sura ya ubinafsi kwa wanaume. Wanaume ili kujilinda maslahi yao baada ya kustukia ubinafsi wa wanawake nao wanaamua kuwa na namna zao za kuishi ambazo zitawapa security dhidi ya ubinafsi wa wake zao.
Nadhani tungekuwa na mahaka halali kisheria inayosimamia maslahi ya wanandoa na kuwaadhibu wale wanaowafanyia visa wenzao bila upendeleo wowote wa kijinsia ndoa zingekuwa salama sana.
Sasa mfano mwanamke anamkatalia mwanaume wake tendo la ndoa kwasababu hajisikii kufanya chochote unataka mwenzako afanyeje kutuliza hamu zake, akisema anataka mke mwingine unaanza kuleta bange ndoa inavunjika?