Habari, kuna aina nyingi sana za biashara kwa mtaji wako, japo ingefika milion 15 ingependeza zaid, unaweza fungua duka la kuuza malidhafili za kutengenezea chakula cha kuku, kama mashudu ya alizet, mashudu ya pamba , damu,chokaaa, pumba nk, hii biashara inalipa na hizi bidhaa kuna baadhi unafuata mkoani nyingine zipo hapa dar,
Biashara ya pili ni kununua nafaka mikoani na kuja kuuza dar, hasa mahindi hii pia iko vuzuli japo kwa kipindi hiki maindi yapo juu sana lkn unaweza kuvuta subila ikifika mwezi wa 5 unaanza na mahindi ya mtukula kwa milioni kumi inatosha kuna kipindi maindi yanauzwa sh 600 kwa hiyo ukiwa na milioni 10 unakwenda kuchukua tani 15 - 18 na ukija kuuza unapata faida nzuli tu,
Kuna biashara ya kufungua mashine, kiukweli hii ndio biashara ya ndoto yangu , biashara hii imegawanyika makundi 3.
Unafungua mashine kwa ajili ya kusaga vipeto vya watu tu, hii kwa cku hukosi kuanzia 20-50 kutokana na eneo ulilopo lkn unawez kuwa na mashine ndogo kama SB 30 kwa ajili ya kukoboa mpunga kwa watumiaji wa chini biashara hii ni nzuli sana kwa nje ya dar.
Biashara nyingine ni kufungua mashine ya kusaga sembe hii unaweza kufanya hapa dar tena ukiwa na mtaji mzuuuli unachofanya unafungua mashine yako unaleta mahindi kutoka shamba unakoboa kwa mashine yako, , kuna wale wasiokuwa na mashine watakuja kukoboa kwako lkn pia kama unamtaji wa kutosha unawakopesha mahindi wajasiliamali wadogo pale pale mashineni wanasaga wanauza sembe wanakulipa pesa yako.
Baishara ya tatu ni kufungua mashine ya kukoboa mpunga ,hii inakuwa ya kukoboa mpunga tu, unanuna SB 50 unafunga mahali pazuuli kisha unakuwa na stoo kuuubwa ya kuhifadhia mpunga ,wakulima wanaleta mpunga kwako wahifadhi kisha ukifika msimu wanakoboa, lkn pia wafanya biashara wanakuja hako kukoboa na kununua mchele hii ni nzuli sana, karibu mp boss,