Kijana mwenye wazo la Biashara la mtaji wa Mil 5-10

Kijana mwenye wazo la Biashara la mtaji wa Mil 5-10

Hassanjk

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2023
Posts
333
Reaction score
689
Anatakiwa kijana mwenye wazo la Biashara linaloendana na taaluma yake ambapo ana hakika litaleta faida, anitafute ni muunganishe afanye hiyo Biashara mwenyewe; (faida watagawana kwa makubaliano)

Biashara iwe halali na isiwe ya Kilevi na pia isiwe mikopo umiza
 
Anatakiwa kijana mwenye wazo la Biashara linaloendana na taaluma yake ambapo anahakika litaleta faida, anitafute ni muunganishe; (faida watagawana kwa makubaliano)

Biashara iwe halali na isiwe ya Kilevi na pia isiwe mikopo umiza
Chap kwa haraka mil5-10 fungua game lounge. Weka ndani PS4, PS5 weka game zingine za mashine umo. Weka goli lako mjini, jirani na masoko makuu na ulipo Kisha ulete mrejesho baada ya mwaka mmoja au miezi 6 tu
🥴
 
Anatakiwa kijana mwenye wazo la Biashara linaloendana na taaluma yake ambapo anahakika litaleta faida, anitafute ni muunganishe; (faida watagawana kwa makubaliano)

Biashara iwe halali na isiwe ya Kilevi na pia isiwe mikopo umiza
Unajua kupewa idea za biashara. Ni utajiri mkubwa sana.
Watu wakikuletea idea uwalipe hata kama haukubaliana nao.
 
Unajua kupewa idea za biashara. Ni utajiri mkubwa sana.
Watu wakikuletea idea uwalipe hata kama hikukubaliana nao.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Umeshtukia mchezo,hakuna mkopo wala fund hapo.
Mara nyingi watu ndio hutafuta pesa za capital na si pesa ziwatafute watu.
 
Mkuu Mimi nakushauri ufungue Steshenari, hii inafaida kubwa sana, haina stress za vitu au bidhaa kuisha muda wake.

Mchanganuo wake uko hivi, printer nzuri ni ya Epson ambayo ni L850 bei yake ni 850,000 Hadi 1,000,000, photocopy mashine ina-range kuanzia 1,000,000 Hadi 2,000,000

Bidhaa mfano limu moja ina uwezo wa kukuingizia Hadi shilingi 50,000 hii ni minimum ikiwa utatoa kopi tu, bado kusafisha picha, 4x6 ni sh 200 Hadi 300, kwenye box moja zimo karatasi 100.

Hii ni kwa ufupi mkuu,
 
Habari, kuna aina nyingi sana za biashara kwa mtaji wako, japo ingefika milion 15 ingependeza zaid, unaweza fungua duka la kuuza malighafi za kutengenezea chakula cha kuku, kama mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba, damu, chokaaa, pumba nk, hii biashara inalipa na hizi bidhaa kuna baadhi unafuata mkoani nyingine zipo hapa Dar.

Biashara ya pili ni kununua nafaka mikoani na kuja kuuza Dar, hasa mahindi hii pia iko vizuri japo kwa kipindi hiki mahindi yapo juu sana lakini unaweza kuvuta subira ikifika mwezi wa 5 unaanza na mahindi ya Mtukula kwa milioni kumi inatosha kuna kipindi mahindi yanauzwa sh 600 kwa hiyo ukiwa na milioni 10 unakwenda kuchukua tani 15 - 18 na ukija kuuza unapata faida nzuri tu.

Kuna biashara ya kufungua mashine, kiukweli hii ndio biashara ya ndoto yangu, biashara hii imegawanyika makundi 3.

Unafungua mashine kwa ajili ya kusaga vipeto vya watu tu, hii kwa siku hukosi kuanzia 20-50 kutokana na eneo ulilopo lakini unawez kuwa na mashine ndogo kama SB 30 kwa ajili ya kukoboa mpunga kwa watumiaji wa chini biashara hii ni nzuri sana kwa nje ya Dar.

Biashara nyingine ni kufungua mashine ya kusaga sembe hii unaweza kufanya hapa Dar tena ukiwa na mtaji mzuuuli unachofanya unafungua mashine yako unaleta mahindi kutoka shamba unakoboa kwa mashine yako, kuna wale wasiokuwa na mashine watakuja kukoboa kwako lakini pia kama una mtaji wa kutosha unawakopesha mahindi wajasiliamali wadogo pale pale mashineni wanasaga wanauza sembe wanakulipa pesa yako.

Biashara ya tatu ni kufungua mashine ya kukoboa mpunga, hii inakuwa ya kukoboa mpunga tu, unanuna SB 50 unafunga mahali pazuuri kisha unakuwa na stoo kuuubwa ya kuhifadhia mpunga, wakulima wanaleta mpunga kwako wahifadhi kisha ukifika msimu wanakoboa, lkn pia wafanya biashara wanakuja hako kukoboa na kununua mchele hii ni nzuri sana, karibu mp boss.
 
Habari, kuna aina nyingi sana za biashara kwa mtaji wako, japo ingefika milion 15 ingependeza zaid, unaweza fungua duka la kuuza malidhafili za kutengenezea chakula cha kuku, kama mashudu ya alizet, mashudu ya pamba , damu,chokaaa, pumba nk, hii biashara inalipa na hizi bidhaa kuna baadhi unafuata mkoani nyingine zipo hapa dar,

Biashara ya pili ni kununua nafaka mikoani na kuja kuuza dar, hasa mahindi hii pia iko vuzuli japo kwa kipindi hiki maindi yapo juu sana lkn unaweza kuvuta subila ikifika mwezi wa 5 unaanza na mahindi ya mtukula kwa milioni kumi inatosha kuna kipindi maindi yanauzwa sh 600 kwa hiyo ukiwa na milioni 10 unakwenda kuchukua tani 15 - 18 na ukija kuuza unapata faida nzuli tu,

Kuna biashara ya kufungua mashine, kiukweli hii ndio biashara ya ndoto yangu , biashara hii imegawanyika makundi 3.

Unafungua mashine kwa ajili ya kusaga vipeto vya watu tu, hii kwa cku hukosi kuanzia 20-50 kutokana na eneo ulilopo lkn unawez kuwa na mashine ndogo kama SB 30 kwa ajili ya kukoboa mpunga kwa watumiaji wa chini biashara hii ni nzuli sana kwa nje ya dar.

Biashara nyingine ni kufungua mashine ya kusaga sembe hii unaweza kufanya hapa dar tena ukiwa na mtaji mzuuuli unachofanya unafungua mashine yako unaleta mahindi kutoka shamba unakoboa kwa mashine yako, , kuna wale wasiokuwa na mashine watakuja kukoboa kwako lkn pia kama unamtaji wa kutosha unawakopesha mahindi wajasiliamali wadogo pale pale mashineni wanasaga wanauza sembe wanakulipa pesa yako.

Baishara ya tatu ni kufungua mashine ya kukoboa mpunga ,hii inakuwa ya kukoboa mpunga tu, unanuna SB 50 unafunga mahali pazuuli kisha unakuwa na stoo kuuubwa ya kuhifadhia mpunga ,wakulima wanaleta mpunga kwako wahifadhi kisha ukifika msimu wanakoboa, lkn pia wafanya biashara wanakuja hako kukoboa na kununua mchele hii ni nzuli sana, karibu mp boss,
Hizo mashine za
1. Kukoboa mpunga
2. Kukoboa na kusaga unga, natakiwa niwe na mtaji kiasi gani kwa kila mashine?
 
Back
Top Bottom