Tetesi: Kijana toka Kanda ya Ziwa anaandaliwa baada ya Mihula ya Rais Samia kuisha

Hakuna sababu hata moja inayoweza kusimama Samia aendelee 2025..kwake akikubali ghilba hii ni kukosa shukurani kwa Mwenyezi Mungu na ufinyu wa kufikiri kwa wale wanaomsemea aendelee sababu kazi hii ni mzigo mzito, kipindi alichofanya km Makamu na Rais kinatosha si kwake tu kwa mtu yeyote..hivyo anastahili kupumzika, uongozi si kula na kufanya anasa!
 
Hii nchi hamfikirii tena kama Kuna uchaguzi ulio huru na haki

Badala yake mnajitengenezea viongozi toka chama Tawala pekee, utadhani hii nchi ni ya mfumo wa chama kimoja😎
Tanzania hatumo kwenye mfumo wa vyama vingi.
 
Point iko hapa "Kanda ya Ziwa Magharibi ila Sio Ngosha"
 
Mawazo ya kijinga ya kikanda!
 
Biteko awe waziri mkuu..?unaongea kutoka kichwani..au tumbo ndio linaongea..
Ndio cheo angalau chenye kutufaa sisi watu wa mikoa ya kanda ya ziwa. Urais hautufai kwa kigezo cha kumtazama JPM akiwa ndio mfano hai wa aina ya utendaji kazi wa mtu wa mikoa ya kanda ya ziwa.
 
Huyo mbona ni mrundi hata hivyo
 
Je, wananchi wasipomtaka?
 

Hii Kanda ya ziwa Magharibi si ndio Kigoma?
 
Kafulila?
 
Endeleeni kudanganyana tu. Vijana hawana mpango na Rais atakayeandaliwa na CCM. Vijana Wana mpango na Rais atakayetatua changamoto zao.

Na mbaya zaidi waliopo kwenye mfumo hawaonekani kuyaweza hayo. Wamelewa na posho na madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…