Kijana ukitaka kuoa oa msichana anayeishi nyumbani kwao

Kama kaajiriwa mbali na nyumbani sawa. Ila eti mtu ni mpambanaji anaishi mwenyewe mjini afu tena ana watoto/mtoto. Kimbia nakushauri we kimbia (kwa sauti ya Langa kileo)
Hahahahaha,kimbia fasta toka nduki ...
 
Binti akiishi mwenyewe bila muongozo kupotea ni rahisi sana,na changamoto za mahusiano kwenye familia zimekuwa nyingi kwa sababu uoaji wa hovyo umekithiri vijana wanaoa wavuta shisha,wapigwa three some wadangaji etc bila kujua.

Binti akiwa chini ya familia hawezi kukaa nje ya nyumba mpaka saa nne usiku but akiwa na ghetto lake atakesha mpaka asubuhi sasa huko kukesha ndiko atavutishwa bangi,unga kunywa pombe kali na takataka nyengine akifika umri wa ku-settle akikutana na kijana innocent anamuektia utulivu akiingia ndoani ndipo mume anagundua kumbe alioa teja,levi na mal.aya.

Mimi hata nilikuwa sijui wala sijawahi kuwaza kama nao kuna watu huwa wanawaoa
 
Mwisho watu wanajilia kimasihara na kisela
 
Amini alichoandika mleta mada hapo juu ana point.

Binti ambaye hajazoea kujibizana na wanaume hovyo (anayeishi bado na wazazi wake) kujibizana na mumewe ndani ya ndoa ni tofauti na mwenye uzoefu wa kujibizana na wanaume(waliopanga) kwenye ma-bar,siku hizi wapo mpaka wanaobishana masuala ya mipira na wanaume na kwenye mabanda ya mpira wanaingia.

Hao ni vitu viwili tofauti
 
Hawa hapa
 
Unataka kufundisha watu ujinga mtupu wakati wewe mwenyewe hujielewi. Hivi unajua madhara ya binti anaeandamana au kushea kila kitu na mamske ni mwanamke wa aina gani?
Unajua kila kitu mtachotofautiana atamshirikisha mamske kitu ambacho sio sahihi kwenye ndoa?
Hivi wewe unaweza somesha binti yako umemwaga pesa kwa elimu yake halafu aje akae nyumbani kwa babake na mamake asuburie kuolewa?
Suala la mahusiano halihusiani kbs na uwepo wa mwanamke au mwanaume mjini au kijijini nyumbani au maofisini. Ishi hapa ni nani anamchukua nani kwa kuangalia kupendana sio mali. Unataka kuoa binti anaekaa na baba na mama au unataka kuoa mwanamke kwasababu umempenda?
Acha kuvuka daraja kabla hujalifikia, ingia kwenye ndoa uishi kwa miaka 5 ndio uzungumzia maisha ya ndoa.
 
Umeandika mengi sana huo ni mtazamo wako lakini mimi humo nilimo-bold,usije ukamshauri mwanao kuoa mwanamke kwa sababu amempenda mshauri amuoe kwa sababu ameona ndiye anayefaa kumuendelezea kizazi chake.

Kupenda apende mwanamke mwanaume sifa yake kuu ni kumthamini kwa yale atakayoyafanya huyo mwanamke.
 
Wewe ni mwanaume wa dar. Huwezi elewa.... Basi unaona umeandika points. Sema haya uliyoyaandika mbele ya wanaume wenzako watakucheka na wakikuweza watakupiga vibao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…