Kijana usiingie kwenye ndoa kwa tumaini la kusaidiana na mkeo kifedha

Kijana usiingie kwenye ndoa kwa tumaini la kusaidiana na mkeo kifedha

Upo sahihi Kama mumeokotana na hampendani.
Na hamjui nini maana ya Familia.

Siku zote familia yenye mfumo uliousema kamwe haiwezi kuendelea.
Hiyo ni Familia yenye ubinafsi, na kwenye ubinafsi kuna unyanyasaji.

Unakuta mume anamnyanyasa mke kisa Mke Hana kipato, au kisa mume ndiye analisha familia. Halikadhalika na Mke naye anamnyanyasa mume kisa Hana kipato na yeye ndiye analisha familia.

Msingi Mkuu wa ndoa ni Upendo na wala sio pesa.

Ushauri wako ni mzuri Kutokana na Dunia ya sasa ilivyo, wanawake ni selfish Kwa watu wasiowapenda. Hilo ulizingatie Sana.

Pesa zako hazimfanyi mwanamke akupende, hilo pia uliweke akilini.
Na Mwanamke lazima Ajue uzuri wake na kujitoa kwake hakumfanyi mwanaume akupende.

Upendo WA kweli hautengenezwi.
Kuupata upendo wa kweli ndio kipengele.

Na hapo ndipo mtoa mada hoja yake inapopata nguvu
Huwezi kulazimisha mke akupenda hata siku moja kama yeye anaona pesa yake ende kujanga kwao, jambo hambalo huwezi kugundua kabla ya kumuoa, na ni ujinga kumpa talaka kisa hela yake inaishia kwao
 
Kabla ujaingia kwenye ndoa rasmi jiakikishe una uwezo wa kifedha kuhudumia familia yako na wazazi wako pamoja na wamke wako kwa kiasi, otherwise ukienda na matumaini ya kuchangiana na mwanamke wako utakua disappointed bure na kua frustrated unabadilika kua mdokozi tapali jizi kwenye mali ya mkeo, utajaa wivu fitna kwa pesa ya mkeo ambao sio yako.(chako ni chetu chakwangu ni changu tu) hiyo ndo formula ya wanawake.

Kiasilia sie wanaume kazi yetu ni ku-pambana na kuhudumia familia zetu bila kuangalia kipato cha mkeo, akiamua kuchangia bora ni vizuri ila naturally wanawake ni selfish raha wataka wapate wao tu sio wengine, kwahiyo bora kujiandae mapema hiyo hali ikifika ķwako usivunje ndoa yako au kulalamika au kua mwizi ndani ya familia, msaada wa mwana mke kwenye ndoa ni just bonus sio lazima wanaume tutafuteni pesa tuache Umario kutegemea vya bure.
Ndio maana nitaendelea kugegeda tuu na sio kuweka ndani
 
Wewe angalau umeongea logic[emoji122][emoji122]

Yaan unakuta hela ya mwanaume haionekani au hayuko responsible kabisa afu anasema hela ya mwanamke lazima ionekane na isaidie nyoooo [emoji1787][emoji1787]
Binafsi naona hawa wanaume wa JF sio hawa waliopo majumbani, ambao wanawake hasa waajiriwa .....kutwa kucha wanalalamika hela za wanaume hazionekani. Na ikiwa wana kazi nzuri na wanalipwa vizuri.
 
Huwezi kulazimisha mke akupenda hata siku moja kama yeye anaona pesa yake ende kujanga kwao, jambo hambalo huwezi kugundua kabla ya kumuoa, na ni ujinga kumpa talaka kisa hela yake inaishia kwao

Mwanamke kama huyo unafukuza mapema Sana ni hatari Sana huko mbeleni utakapokuwa hauna nguvu
 
Sidhani kama kulikuwa na haja ya kuandika comment ya kidhaifu namna hii. Watu kama wewe ndio mnapotosha uma wa wanawake kuwa wanaume mbele yao hatuna ujanja na ni dhaifu halafu wanakuja kutana na majambazi wanapigwa na kitu kizito wanaishia kusema wanaume ni mbwa.

Sifa ya mwanaume ni kutokukubali kuonekana dhaifu. Umeandika kizembe sana , sijapenda kwakweli. Nikiwa kama Kaka yako mkuu na kiranja wa mwenendo wako nakuagiza uedit hii comment iwe ya kibabe au uifute ili kusafisha hadhi yako ya kiume.
Hahaha asante bro nimekuewa , lakini si edit wala kufita!!
Nimeongea kwa uzoefu wangu kwa wanawake, na hapo nimewaongelea kwa sehemu ya kuwastahi!
Hata hivyo kila mwanaume ana experience yake juu ya wanawake.
 
Watu si wanafikiria maisha ni burudani tu. Maisha ni fumbo mkuu, kuoa ni mtihani unahitaji akili sana. Binafsi mi ntao mke wa mfano wa huyo shemeji yako. Hata nikifa watoto wangu wako sehemu salama coz mama yao ni strong.
Unakuta mume kaugua au kaachshwa kazi au biashara zinakufa familia inataabika.
 
Pet 3:7 SUV

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Keyword ni Kaeni na wake zenu kwa Akili
Mwanamke asiye na akili hawezi ishi na mwanamke

Ukiona mwanaume akamshindwa mwanamke ujue ajili hana

Na ukiona mume kaachwa ujue akili huyo mwanaume hana
 
Mwanamke kama huyo unafukuza mapema Sana ni hatari Sana huko mbeleni utakapokuwa hauna nguvu
Unadhani kufukuza mwanamke wa kileo kirahisi hivyo unalo .Eti fukuza unaota enzi za mfumo dume zilishaondoka mtaburuzana mahakamani hadi ujute kuzaliwa na kumfahanu
 
Mimi naishi kwa kutegemea pesa ya mke wangu, na Maisha yanasonga, tatizo watu wanayachukulia haya Maisha too serious utadhani wanampango wa kuishi miaka 500 kwenye uso wa dunia.

Don't complicate life, tuumia pesa ya mkeo , akudharau poa , asikudharau poa, siku ukishindwa kuvumilia tafuta mwingine maisha yasonge

Nasema hivi kwakuwa juzi tu wife kanitumia 2M nikahemee vitu vya ofisi yetu.Sasa Mkuu Kama wewe umeangukia kwa mke mbovu usilinganishe Wala kutupangia wale ambao tunawanawake wanaotupeti-peti.

Nampenda sana mke wangu, maana ananitii na kuniheshimu
 
Ndoa ni tamu, ni Taasisi iliyoanzishwa na Muumba pale bustani ya Edeni, hamna sababu za kutishana. Mwanaume mpe Yesu maisha yako umche Mungu kisha Mungu atakuunganisha na mwanamke mcha Mungu mtakaeendana. Utayafurahia maisha. Apataye mke apata kitu chema.



YESU NI BWANA
 
Ila kwel Kila mtu aoe saiz yake.la si ivyo utaishia kugombana na kuugua bure..
 
Mkuu ukitambua kwamba mwana mke ndani ya nyumba she is "a friendly enemy" hapo ndo ujue jinsi ya kupambana na rafiki adui wako, ukiwa mshamba ukiaza kuzimia eti honey I love you 100% hao watu ndo wanao jinyonga baada ya kusalitiwa na wake zao, ukiwa kwenye deep love na wife jicho moja ziba jingine liwe wazi, ukiziba yote umeisha.
Hakika, hii ilinitokea mwaka 2012, kama sio ule ujasiri wa kiume ambao si kila mwanaume anao ningefanya tukio lingelo nigarimu, hii ni kutokana na kuizingatia kauli ya mwanamke kwamba "wewe ndio mwanzo na mwisho kwangu , usiniache please, usiniumize please,nimeweka maisha yangu kwako, wewe ni zaidi ya baba yangu" na mengi mengi ya mna hio, sasa kama mwanaume unaamini na kuyazingatia na kuyaishi. L

Kesho unakuta amelala n mwanaume mingine na kuhamia kwake kabisa hai ya kua wewe ushaweka maisha yako kwake, ndio maana watu wanaua!!
 
Kwa UELEWA WANGU!
Me ni mkristo
Ki bible mke analetwa kwangu kama msaidizi.
Sifa namba moja ya msaidizi ni KUJUA KAZI INAYOFANYIKA!
Huwezi kua msaidizi wakati hujui kitu unachosaidia
Mkeo anatakiwa akujue wewe 100%
Na wewe umjue yeye 100%

Kuna mistake moja inafanywa na wanaume wengi
Kuwaficha wake zao uharisia wao
Mke anaishi na mumewe lakini hajui a-z ya mume wake kama
Viwango na kipato,
Upatikanaji wake wa fedha’
Mazingira yake ya fedha’
Namna yake ya kupata fedha,
Balance ya fedha
Kiwango kilichopo
Malengo na mikakati ya familia kiujumla


Japokua kwa namna furani naweza kuunga mkono usiri hu wa wanaume kwa wake zao(kwa zile kabila zenazoaminika kuuwa wenza wao wakifanikiwa)

Ila kwa namna ya kawaida ni vyema mke akimjua memewe na akamuelewa ili wasaidianapo wawe wanafahamiana wao kwa wao sababu zao

Kuna mapungufu ya kimaisha na kininadamu ambayo hayo ni kawaida na ni vyema ukiyatambua kabla ya kuingia kwenye ndoa
Mfano
Uchoyo
Uchafu
Na mambo yanayohusiana na hayo

Je mkeo anajua uharisia wako? Au anakukadilia tu? Hafahamu na haelewi

Mwanamke ni financial mzuri sana wa fedha
Akijua malengo na mikakati yako anaweza kukusaidia hata ku control mambo ya nyumbani huku akikumbuka Target zenu
Ila ikiwa anajua malengo yenu ila still yuko opposites hili ni janga kuu
 
Back
Top Bottom