Kijana wa miaka 28 anywa sumu baada ya kuambiwa mtoto aliyekuwa akimlea si wake

JUSTINE AMEFARIKI BAADA KUAMBIWA MTOTO SI WAKE

Mwili wa kijana Justine Mbaga mwenye umri wa miaka 28 ambaye amefariki dunia jana Februari 11,2025 ikidaiwa ni kwa kunywa sumu baada ya kupewa taarifa kuwa mtoto aliyekuwa anamhudumia si wake, umezikwa leo katika makaburi ya Magegele yaliyopo Halmashauri ya mji Makambako.

Taarifa zinaeleza kuwa siku ya jumapili Februari 9,2025 familia ya binti ya aliyekuwa naye kwenye mahusiano walimwita Justine Mbaga, na familia yake na kumweleza kuwa mtoto ambaye alikuwa anamlea si wake, jambo ambalo lilipelekea kuathirika kisaikolojia na kuchukua uamuzi huo.

Baadhi ya majirani wa Justine Mbaga wamesema kifo cha mpendwa wao kimewaacha na majozi mazito kwani alikuwa ni kijana mwenye maadili mema.

Ratifa kibiki ni, mama mzazi wa binti mwenye mtoto huyo anayedhaniwa ni mtoto wa Justine Mbaga akizungumza na El olama fm amesema waliamua kumuita Justine Mbaga na Familia yake na kuwaeleza kuwa mtoto huyo si wao kwani aliona si busara Justine aendelee kulea mtoto ambaye si wake.

Aidha Mama huyo amesema binti yake alikuwa tayari kurejesha gharama za matunzo ambazo Justine Mbaga alizitumia kumlea mtoto huyo ambazo ni 850,000/=.

Diwani wa kata ya kitisi Nevy Sanga na mtendaji wa mtaa wa Kisingire,wameiasa jamii iache tabia ya kuchukua sheria mkononi hasa inapojitokeza changamoto yoyote kwenye maisha.

🎥
✍️

View attachment 3234433
Unajinyonga alafu iwe nini, anyway rest in peace champ.
 
Washenzi hawa wanafikiri issue ni pesa. kuna emotional attachment kati ya Baba na huyo mtoto ambayo ndio ndio inawezekana ilimuumiza jamaa zaidi. Ila vijana wa sasa wana low EQ.
 
Washenzi hawa wanafikiri issue ni pesa. kuna emotional attachment kati ya Baba na huyo mtoto ambayo ndio ndio inawekana ilimuumiza jamaa zaidi. Ila vijana wa sasa wana low EQ.
Kabisa mnama
 
Dah kama ni hivyo wangu wote ni nnje hadi mimi pia nipo nnje.
Ahahha ili siku mwanamke akisema hawa sio watoto wako unamwambia haya ondoka peleka kwa baba yao waje wakae wangu sasa mnajaza nafas kwa makusudi unamleta kidume wako wa njee anakaa utaona nan anapata mhaho
 
hata tusimlaumu, roho ya mauti ikikuambata yeyote anaweza kufanya lolote, hata kama hangejinyonga ila as long as roho ya mauti ilikuwa inamwandama, angekufa kwa kingine hata ajali tu. Uzuri uliopo ni kwamba, Yesu Kristo alikufa, akazikwa, siku ya tatu akafufuka kwa kuishinda mauti, uwapo uchungu wako ewe mauti, Yesu Kristo ana nguvu kuliko mauti yeyote ile, Yesu KRisto anao uwezo kureverse mauti yeyote, Yesu Kristo, ukisoma Isaya 53 inasema alipigwa na kuuawa badala yetu, chochote alichofanyiwa, ilikuwa kwa niaba yetu kwa ajili ya kutukomboa sisi toka kwenye hiyo hali.

Ushauri kwenu, kama hauna Yesu Kristo moyoni, okoka haraka, ili Yesu akuponye na mauti, akuepushe na mauti, au la, wewe binafsi utapambana na mauti na hautashinda, na elewa kwamba, kwa uwezo wako hautaishinda mauti, anahitajika yeye aliyeishinda mauti, ndiye Yesu Kristo mnayemkataa. Mungu awasaidie.
umeanza porojo zako
 
siku hizi marehemu nao wanalaumiwa. Cc: Kiranga
mpumbavu huyo, ilo ndio jambo la kujiua yaan kuambiwa mtoto si wako unakimbilia jiua

na binti anakaa kwao, je angekuwa anakaa nae akapata ule usumbufu wa kulala macho kubembeleza mtoto na baadae unaambiwa sio wako na wala hakuna matata,

dogo nae akili ndogo
 
Ahahha ili siku mwanamke akisema hawa sio watoto wako unamwambia haya ondoka peleka kwa baba yao waje wakae wangu sasa mnajaza nafas kwa makusudi unamleta kidume wako wa njee anakaa utaona nan anapata mhaho
Kila siku nasisitiza unywaji wa bia zaidi kuliko kuendekeza mapenzi mnaniona kibwengo , ukinywa bia kidogo na kuvuta bangoooo kidogo hauwezi kuwa na akili ya kinyumbu hivi .
 
Haahh sawa tutakunywa

Kuna jamaa alizaa mtoto wa njee akawa analinga umri na mtoto wa ndani ya ndoa sasa wale watoto wakawa wanasoma shule moja bila kujuana mkubwa ambaye ni wa ndani ya ndoa akasikia kuna mtoto mwingine wanafanana majina ya mwisho akamfwata kumuuliza yule mtoto we jina lako nani akamtajia majina yote akamuuliza baba yako anafanya kazi wapi akamwambia sehemu ambayo baba yake anafanya kazi alipo rudi nyumban yule mtoto aka mwambia mama yake palinuka nakwambia
 
Back
Top Bottom