Kijana wa miaka 28 anywa sumu baada ya kuambiwa mtoto aliyekuwa akimlea si wake

Kijana wa miaka 28 anywa sumu baada ya kuambiwa mtoto aliyekuwa akimlea si wake

Washenzi hawa wanafikiri issue ni pesa. kuna emotional attachment kati ya Baba na huyo mtoto ambayo ndio ndio inawezekana ilimuumiza jamaa zaidi. Ila vijana wa sasa wana low EQ.
Hata spiritual strength hawana
 
Wazee kwa vijana wanateseka sana na suala hili.
 
Ninadhani hali hii inachangiwa pia na vijana wengi kulelews na mama pekee bila baba.
Mtoto aliyelelewa (hasa wa kiume)na mama pekee yake bila baba au ndugu wa kiume kwa asilimia kubwa huwa anaiga uhusika wa kiuanamke. Mwanamke hutegemea zaidi hisia kuliko uhalisia!

Angalia wengi wa wanaume wanaoleta malalamiko ya kimahusiano humu jamvini wamekaa kihisia zaidi (sifa kuu ya kike) yaani wamekaa kudekadeka! Yaani ishu ndogo anaileta jamvini badala ya kufanya uamuzi au kupotezea!

Wewe mwanaume uliyeacha mtoto hasa wa kiume huko,ipo siku huyu mtoto atakuwa na sifa hizo coz mwanamke anajua huruma ndiyo malezi!
 
Duh hili binti litamtesa maisha yake yoote, sawa walitaka kumlipa laki 8 yake,je vi na muda alioupoteza qatamlipa??
Una maana kila kitu alicha mfanyia mtoto Alikuwa ana record Huyo mwanamke? Akimnunulia nguo anauliza ni bei gani, akileta sukari anauliza...........
 
Ila wanawake watakuja kutuua tuishe wote. Amembambikizia mimba jamaa.... Jamaa kailea, kalea na mtoto halafu anakuja kuambiwa chukua 850k yako mtoto si wako 🙌

Hapo ukute baba halisi wa mtoto kapata maisha sasa kamwambia binti achana na huyo fala njoo ule maisha huku kwangu
Ubapa wa panga ungehusu ukoo mzima😀😀😀😀😀
Na laki nane nachukua...
 
Ubapa wa panga ungehusu ukoo mzima😀😀😀😀😀
Na laki nane nachukua...
Tumeanza mapenzi tukiwa vidudu huko...uhuni mpaka umri huu..

Hiyo familia ingekula mbata na drama za kutosha...

Laki nane hii ni ndogo...vijana tuwe tunasema mambo hata kwa masela ...bro ameenda na 28..Kinda kabisaaa..anaacha watu wanakula ugali na hewa ya bure.
 
Jitahidi uwe malaya kidogo ili siku yakikukuta usijiue bali ujipigepige kifua
Hata ukiwa malaya kiasi gani kutatokea mmoja ambaye moyo wako utamchagua alafu wewe mwenyewe utashangaa hata imekuwaje kuwaje ukamchagua........

Alafu sasa kwa bahati mbaya yeye hana hata time na wewe......

Na ndio mateso yanapoanzia.....
Mapenzi hayana mwenyewe omba Mungu tu usinase.....

Wote wanaopigania mapenzi sio kwamba hawana wapenzi wengine bali wamekwama....
 
Mama mkwe na mtoto wake wote hawana akili. Thamani ya mtoto unaithaminisha na pesa!?? Tena 850k?? Aaaah
 
JUSTINE AMEFARIKI BAADA KUAMBIWA MTOTO SI WAKE

Mwili wa kijana Justine Mbaga mwenye umri wa miaka 28 ambaye amefariki dunia jana Februari 11,2025 ikidaiwa ni kwa kunywa sumu baada ya kupewa taarifa kuwa mtoto aliyekuwa anamhudumia si wake, umezikwa leo katika makaburi ya Magegele yaliyopo Halmashauri ya mji Makambako.

Taarifa zinaeleza kuwa siku ya jumapili Februari 9,2025 familia ya binti ya aliyekuwa naye kwenye mahusiano walimwita Justine Mbaga, na familia yake na kumweleza kuwa mtoto ambaye alikuwa anamlea si wake, jambo ambalo lilipelekea kuathirika kisaikolojia na kuchukua uamuzi huo.

Baadhi ya majirani wa Justine Mbaga wamesema kifo cha mpendwa wao kimewaacha na majozi mazito kwani alikuwa ni kijana mwenye maadili mema.

Ratifa kibiki ni, mama mzazi wa binti mwenye mtoto huyo anayedhaniwa ni mtoto wa Justine Mbaga akizungumza na El olama fm amesema waliamua kumuita Justine Mbaga na Familia yake na kuwaeleza kuwa mtoto huyo si wao kwani aliona si busara Justine aendelee kulea mtoto ambaye si wake.

Aidha Mama huyo amesema binti yake alikuwa tayari kurejesha gharama za matunzo ambazo Justine Mbaga alizitumia kumlea mtoto huyo ambazo ni 850,000/=.

Diwani wa kata ya kitisi Nevy Sanga na mtendaji wa mtaa wa Kisingire,wameiasa jamii iache tabia ya kuchukua sheria mkononi hasa inapojitokeza changamoto yoyote kwenye maisha.

🎥
✍️

View attachment 3234433
Ninachojua GENTAMYCINE ni kwamba 85% ya Wanaume nchini (Mimi wala simo) wanalea 'Mabao' ya Wanaume wenzao.
 
Back
Top Bottom