DOKEZO Kijiji cha Kazuramimba (Uvinza, Kigoma): Mauaji yaliyofanywa 4/10/2023 ninayekemea kwa nguvu zote, Majeruhi wako wapi?

DOKEZO Kijiji cha Kazuramimba (Uvinza, Kigoma): Mauaji yaliyofanywa 4/10/2023 ninayekemea kwa nguvu zote, Majeruhi wako wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ila hali imayoendelea huko siyo haki, ule ni udhalilishaji kwakweli. Unamtambuaje mchawi kama na wewe siyo mchawi?
Nakumbuka stori yako ya kutoka Kgm to Dar ilikuwa kama unatupanga hivi kumbe ndio kweli upo safarini! [emoji3]
 
Wakuu, hii Nchi ya Ovyo sana, Kuna wajinga wanapopewa nafasi Huwa wanageuka kua Miungu watu.

Jana tarehe 4/10/2023 Kijiji Cha Kazuramimba, Wilayani Uvinza kulitokea vurugu baina ya Polisi na Raia, zilizopelekea Polisi kutumia Silaha za moto, hali hii ilipelekea Raia Kadhaa kufa na wengine kujeruhiwa .

RC, RPC na DC, wakaamua kuzitembelea Hosp zilizopokea majeruhi kimyakimya na kuwaonya kutotoa Taarifa.

Chanzo cha Ugonvi...

Kuna waganga walipelekwa Kijiji huko Kwa Imani za kijadi kwamba wanatafuta wachawi, Kuna mji Mmoja mwenye mji huo akagundulika na Mchawi, Akakimbilia Polisi kishtaki.

Polisi wakamficha hapo na Raia wakamfata hukohuko.

Kukosekana Kwa Busara baina ya Polisi na Raia,. Fuji zikatokea na kituo Cha Polisi hiko kikavunjwa.

Polisi wakaanza kutumia Silaha za moto yaan Bunduki kushambulia Raia.

Raia wengi sana wamejuruhiwa, Vijana, Wanawake na watoto na wazee wameumizwa sana.

Polisi wamewakamata watu Kadhaa na majeruhi Kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana, mpaka Sasa Ndugu wanafuta Ndugu zao .

Ni majeruhi wachache tu Tena waloamua kujipeleka Hosp ndio ambao wamejulikana mpaka Sasa ,huku wengine wakiwa hawajulikani.

Polisi wa Kigoma, wanaongoza kuwa na matukio ya "Majeruhi alinyakua Bunduki ya Polisi nakuanza kurushiana risasi ".

Ndugu zangu nawaomba sana Mnisaidie Kupaza sauti,. Ndugu yangu Yuko huko Kikazi, amesombewa humohumo , mpaka Sasa hatuma Taarifa ya uhai au lolote kumhusu yeye.
Kwa hili nipo upande wa police,mm nipo Congo kwa sasa naona hasara kubwa ya wana inchi kuto kutii sheria kila mtu ni katili ni kama hakuna serikali, ndiyo maana amani ziro police wetu na nilazima wazibiti hayo mambo kwa nguvu zaidi.
 
Unamtambuaje mchawi kama na wewe siyo mchawi?
Nadhani kuna vifaa maalumu vinatumika, kuna mtu alikuwa anaitwa Mwandulami alitaka kuanzisha mafunzo ili mambo ya jadi yatumike kwa faida ikiwa ni pamoja na usafiri wa anga kwa mtu mmoja mmoja ila serikali ikamtia pini
 
Kama haki inapatikana kirahisi hivyo hapa bongo daini mpewe katiba mpya.
Ewe mjuvi wa mambo....

Unafananisha haki za kawaida na mambo ya katiba mpya?!! [emoji15][emoji1787]

Unafeli wapi mwanamji wewe ? [emoji1787]
 
Kwa ninavoona askari wapo sawa kabisa.....hao raia ni washenzi kabisa yaani unabomoa kituo cha polisi kisa mambo ya ajabu na aliyekimbilia huko kafanya sawa kabisa kiusalama.Hao kamchape wakamatwe na hizo kesi za mauaji wapeww wao sababu wao ndio chanzo.
[emoji2956]
 
Hawa raia walikosea kuvamia kituo cha Polisi.Yule aliyekimbilia Polisi,alikwenda mahali,ambapo atapata usalama.Sasa inakuwaje wengine wamfuate huko ili wamuadhibu?
 
Wangepigwa mabomu kabisa, wao wanabakia kituo cha polisi itakuwa n majambazi ya Burundi yanataka kupora bunduki zetu
 
Kwa ninavoona askari wapo sawa kabisa.....hao raia ni washenzi kabisa yaani unabomoa kituo cha polisi kisa mambo ya ajabu na aliyekimbilia huko kafanya sawa kabisa kiusalama.Hao kamchape wakamatwe na hizo kesi za mauaji wapeww wao sababu wao ndio chanzo.
Maoni yako ni mazuri sana.Kwa nini wanaletwa watu wakuwazulia wenzao uchawi?Hao wakamatwe,wafunguliwe kesi ya mauaji,hao Kamchape.
 
Kwa hili nipo upande wa police,mm nipo Congo kwa sasa naona hasara kubwa ya wana inchi kuto kutii sheria kila mtu ni katili ni kama hakuna serikali, ndiyo maana amani ziro police wetu na nilazima wazibiti hayo mambo kwa nguvu zaidi.
Huko Congo waambie taifa pekee lililobarikiwa sana tena sana duniani ni Tanzania....

Ngorongoro ndiko atokako nabii Adam (A.S)....

Waukane uraia wa kwao waje kuomba huku "pepo ya dunia".....

#Alhamdulillahi kwa kuwa mtanzania [emoji120]

Thanks Yahweh [emoji120]
 
Watu wanasemaga Waha ni wabishi sana.Sasa unakwenda kuvunja polisi unategemea nini na bado unalalamika eti watu wameuwawa.Polisi wako sawa niko upande wao Waha shida sana
 
Mwijaku popote ulipo....

Tafadhali yakemee hayo MAMBO ya ndugu zako hapo WASAFI FM [emoji120]

#Polisi Wetu Ni Wa Kwetu[emoji120][emoji120]
 
Wenzake wa kabwe wilaya ya nkasi walijidanganya hivo hivo Ila unaelekea kukata mwezi sasa watu wanazidi kusota rumande na waliokufa waliShazikwa kijjn mambo yanaendelea kama kawa. Walipiga vitisho vingi Ila mwisho wa siku wananchi ndo wanabaki kua wahanga wakubwa.
Nchi ni yenu...

Askari ni wenu....

Mahakama zipo....

Mnatumiaje njia za kihuni kuitafuta haki yako ?!!!! [emoji15][emoji15][emoji15]
 
Back
Top Bottom