Kijiji chote kimesombwa na Mafuriko, Kanisa limebaki

Kijiji chote kimesombwa na Mafuriko, Kanisa limebaki

Hapo nadhani ubora wa ujenzi na mazingira. Tukitaka kujenga nadharia ya kiroho inabidi tuweze kutofautisha kwanza kati ya Kanisa na jengo la kanisa. Kanisa ni muumini/waumini, na jengo la kanisa ni mahali popote pale palipojengwa na muumini/waumini wanapoweza kukutana. Hata bar unaweza kuikodisha na kuitumia kwa shughuli za kuabudu.

Simple waumini huabudu katika majengo mbalimbali pakiwemo kumbi za starehe na burudani, shuleni, vyuoni, hospitalini, sokoni, Bar, hosteli, ofisi, na majengo kadhaa ya umma na binafsi.
Uko nje ya madam mkuu
 
Inamaana hicho Kijiji hakina Shule,zahanati, Police post, mbona hamsemi kama vimesombwa AU laa
AU mnataka kubadilisha mada
 
View attachment 2833512

"Kwenye madhara haya tumepata majeruhi pia wapatao 116, wanaume ni 56 na wanawake ni 60, ndugu Watanzania haya maafa ni makubwa sana, pia tumepata uharibifu mkubwa wa nyumba za kuishi, mashamba na mitambo mbalimbali ya magari, nimepata bahati ya kwenda Gendabi nyuma ya milima, kile kijiji nyumba zimeachwa upande wa kulia na kushoto eneo la katikati nyumba zote zimeondoka limebaki kanisa tu, hali sio nzuri,"

Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

===

Salamu,

Huko Hanan'g kijiji cha Ngendabi nyumba zote zimesombwa na maji ila kanisa limesimama vilevile.
Je hii ni sababu ya matereal za ujenzi au Koroho zaidi?
Nimewahi kuwa mjumbe wa kamati za ujenzi wa makanisa kadhaa.
Kusema ukweli ujenzi wa makanisa husimamiwa vyema sana sana,mimi ni shuhuda katila hili.
Kiroho hili pia linawezekana japo sina ushahidi usio na shaka.
 
Back
Top Bottom