Kikao Kizito: Rais Samia akutana na Makamu wake Dkt. Philip Mpango na Gavana wa BoT, Prof. Luoga

Kikao Kizito: Rais Samia akutana na Makamu wake Dkt. Philip Mpango na Gavana wa BoT, Prof. Luoga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamo wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Isidor Mpango na Gavana wa Benki Kuu nchini Prof .Florens Luoga ,Ikulu jijini Dodoma leo.

View attachment 1753844
View attachment 1753845

Ramadhan Kareem!
Hapo kwenye kiti cha Jambo Plastic ndo Ikulu ya Dodoma iliyojengwa na Hayati Magufuli?
 
Marekani ishawahi kuwa na Supreme Court justices ambao hawakuwa kabisa na shahada ya sheria. Hii ni kweli. Si uzushi wala usadiki.

Kuna mmoja hata high school hakuwahi kumaliza.

Huko kwenye judiciary committee na kwenye senate, hawawezi kumkataa mtu kisa hana shahada ya sheria maana katiba haijakataza hilo.

Na kama katiba haijakataza basi uwezekano wa kuwepo tena Supreme Court justice asiye na shahada ya sheria, upo.

Ni kama vile ambavyo katiba haijakataza watu wa rangi za ngozi zisizo za Kizungu kuwa marais, hata kama hakujawahi kuwepo na Rais Mlatino, hiyo haina maana haitotokea siku moja Mlatino akawa Rais.

Ni Justices watano tu kati ya 60 ambao hawakusoma sheria chuoni. Unayemsema kuwa hakumaliza High School ni James F Byrnes ambae alikuwa Justice 1941 mpaka 1942. Huyu aliacha shule akiwa na miaka 14 kufanya kazi katika ofisi ya wanasheria. Alijisomea mwenyewe sheria na 1903 alipasi Bar Exam na hivyo kutambulika rasmi kuwa ni mwanasheria.

Mwingine ni John Hessin Clarke (1916-1922) ambae alifundishwa sheria na baba yake na 1878 alipasi Bar Exam cum laude na hivyo kutambulika kama mwana sheria.

Wengine ni James Iredel ( 1790-1799) alikuwa appointed na George Washington, huyu alisoma sheria chini ya Samuel Johnson na alipasi mtihani wa Bar 1771.

Thomas Johnson (1792-1793), alisoma sheria katika kampuni ya wanasheria na alipasi mtihani wa Bar mwaka 1753.

Samuel Chase (1796-1811) alikuwa home schooled na alisoma sheria chini ya mwanasheria John Hall na alipasi mtihani wa Bar 1761.

Utaona kuwa hakuna Justice ambae hakusomea sheria kabla ya kuteuliwa. Kwa hivi karibuni wengi walioteuliwa walisoma Ivy League Schools ( Harvard, Yale n.k.) na ni wachache tu wamesoma university za kawaida.

Kwa mazingira ya sasa ni vigumu kuamini kuwa itatokea siku Senate itampitisha mtu ambae hajasomea sheria kabisa kuwa justice. Ni kama vile hamna requirement ya uraia lakini sidhani kama kuna siku mtu asie raia wa Marekani anaweza kupitishwa kuwa justice wa Supreme Court.

Hiyo ya mlatino, mwanamke au hata shoga kuwa Rais wa Marekani ni suala la muda tu maana kwa hawa ni wananchi wanaoamua na sio jopo la watu fulani.

Amandla...
 
Maandalizi za kuficha ripoti ya uchunguzi wa CAG na TAKUKURU pale BoT. Maana taarifa za ndani zinaonyesha Makamu wa Rais na Gavana wapo kwenye hiyo scandal.
Nilisikia hao jamaa wamechota minoti,sidhani kama kuna jipya tena ripoti ya Ukaguzi wa benki kuu.
 
Ni Justices watano tu kati ya 60 ambao hawakusoma sheria chuoni. Unayemsema kuwa hakumaliza High School ni James F Byrnes ambae alikuwa Justice 1941 mpaka 1942. Huyu aliacha shule akiwa na miaka 14 kufanya kazi katika ofisi ya wanasheria. Alijisomea mwenyewe sheria na 1903 alipasi Bar Exam na hivyo kutambulika rasmi kuwa ni mwanasheria.

Mwingine ni John Hessin Clarke (1916-1922) ambae alifundishwa sheria na baba yake na 1878 alipasi Bar Exam cum laude na hivyo kutambulika kama mwana sheria.

Wengine ni James Iredel ( 1790-1799) alikuwa appointed na George Washington, huyu alisoma sheria chini ya Samuel Johnson na alipasi mtihani wa Bar 1771.

Thomas Johnson (1792-1793), alisoma sheria katika kampuni ya wanasheria na alipasi mtihani wa Bar mwaka 1753.

Samuel Chase (1796-1811) alikuwa home schooled na alisoma sheria chini ya mwanasheria John Hall na alipasi mtihani wa Bar 1761.

Utaona kuwa hakuna Justice ambae hakusomea sheria kabla ya kuteuliwa. Kwa hivi karibuni wengi walioteuliwa walisoma Ivy League Schools ( Harvard, Yale n.k.) na ni wachache tu wamesoma university za kawaida.

Kwa mazingira ya sasa ni vigumu kuamini kuwa itatokea siku Senate itampitisha mtu ambae hajasomea sheria kabisa kuwa justice. Ni kama vile hamna requirement ya uraia lakini sidhani kama kuna siku mtu asie raia wa Marekani anaweza kupitishwa kuwa justice wa Supreme Court.

Hiyo ya mlatino, mwanamke au hata shoga kuwa Rais wa Marekani ni suala la muda tu maana kwa hawa ni wananchi wanaoamua na sio jopo la watu fulani.

Amandla...
Hoja haikuwa si mtu aliyesoma sheria.

Hoja ilikuwa ni ‘shahada’ ya sheria kama takwa la kikatiba.

Katiba ya Marekani haijaweka katazo la watu wasio na shahada ya sheria kuwa majaji kwenye mahakama kuu.

Madhali hakuna katazo, uwezekano wa kutokea mtu asiye na shahada ya sheria kuwa jaji wa mahakama kuu au jaji mkuu wa mahakama kuu, bado unakuwepo.

Ila kiuhalisia, kama ulivyosema, kwa mazingira ya sasa inaweza ikawa vigumu.

Hivyo, kuwezekana inawezekana. Ila ikija kwenye mwelekeo wa hilo kutokea, itakuwa ngumu.

Kwa kimombo wanasema it is possible, but unlikely.

Na historia huwa ina tabia ya kujirudia....
 
Yani mama ofisini meza yake nyeupee ina vi file sijui vingapi vile

na huyo ndio head of state,sasa Njoo ofisini kwangu mimi ambae hata ujumbe

wa mtaa sina uone meza ilivyojaa ma file na monitor kama ofisi ya Meridian Betting
 
Prof. Luoga alisomea Kilimo na Tax law leo amekuwa Gavana wa Benki Kuu. Ukisikia mtu kupewa uendeshe Semi-Trailer wakati leseni yako ni ya Bajaji ndio hapo.

Alale mahali pema peponi mzee wa kutumbua na kuteua papo kwa papo!
Waliosomea uchumi hadi nje ya nchi walituletea ufisadi wa kutisha reference ni EPA. Hapo hata msukuma anaweza kua governor. Nchii hii haina mwema
 
Prof. Luoga alisomea Kilimo na Tax law leo amekuwa Gavana wa Benki Kuu. Ukisikia mtu kupewa uendeshe Semi-Trailer wakati leseni yako ni ya Bajaji ndio hapo.

Alale mahali pema peponi mzee wa kutumbua na kuteua papo kwa papo!

Mkuu, analogy yako sio nzuri sana. Governor sio driver per se. Yeye ni mwezeshaji na mratibu wa shughuli za drivers wa aina zote katika taasisi yake. Ni mbeba maono anayepaswa kuwapanga drivers wake ili hatimaye wayatafisri maono yake kwa vitendo.

Ingawa ni kawaida kwa central bank governor kuwa mchumi, sio lazima iwe hivyo. Governor ana wataalam wa kila aina. Kinachohitajika ni uongozi; yeye kuwa kiongozi mzuri na mwenye maono. Mchumi mzuri ambaye sio kiongozi mzuri hawezi kuwa governor mzuri.

Hata kwenye level ya nchi mambo yako hivyo hivyo. Rais anaweza kuwa mbobezi katika military science tu, lakini akaipaisha nchi yake katika nyanja zote muhimu, kwa sababu ya uongozi wake mzuri na wenye maono!
 
Report ya CAG kuhusu BOT kama kuna shida, kuna kafara lazima zitatolewa.

Mpango alikuwa waziri wa fedha, kama kuna uchafu kwenye matumizi, ni vigumu yeye kuchomoka. Unless iwe hakujua, jambo ambalo bado linaleta ukakasi, iweje hakujua? Gavana, Dotto na Bashiru wakae mguu pande mguu sawa. VP hakuna namna ataguswa.
 
Prof. Luoga alisomea Kilimo na Tax law leo amekuwa Gavana wa Benki Kuu. Ukisikia mtu kupewa uendeshe Semi-Trailer wakati leseni yako ni ya Bajaji ndio hapo.

Alale mahali pema peponi mzee wa kutumbua na kuteua papo kwa papo!
Hivi kipo wapi chuo cha kusomea ugavana?
 
Hapo hapo mbowe amepata chanjo ya corona na anafanya social distance kwa joyce mkuya.

Chadema wana kipaji cha ujinga
Nafikiri wewe huna updates au umepitwa na wakati, iko hivi kupata chanjo ya Corona hakukufanyi kutokua na vimelea na kuwaambukiza wengine,ndiyo maana hata huko nchi wanazochoma raia wake, bado wanavaa Barakoa, kwa sababu aliyepata chanjo anakua na virus lakini havina madhara kwake, ila bado anaweza kuambukiz wengine kuputia mate, mafua au chafya.
Japo umeliweka kisiasa, ambayo mimi huko sipo, ila nimeelezea kadri ya huko wenzetu wanavyoishi na hiyo Pandemic!
 
Hoja haikuwa si mtu aliyesoma sheria.

Hoja ilikuwa ni ‘shahada’ ya sheria kama takwa la kikatiba.

Katiba ya Marekani haijaweka katazo la watu wasio na shahada ya sheria kuwa majaji kwenye mahakama kuu.

Madhali hakuna katazo, uwezekano wa kutokea mtu asiye na shahada ya sheria kuwa jaji wa mahakama kuu au jaji mkuu wa mahakama kuu, bado unakuwepo.

Ila kiuhalisia, kama ulivyosema, kwa mazingira ya sasa inaweza ikawa vigumu.

Hivyo, kuwezekana inawezekana. Ila ikija kwenye mwelekeo wa hilo kutokea, itakuwa ngumu.

Kwa kimombo wanasema it is possible, but unlikely.

Na historia huwa ina tabia ya kujirudia....
Mimi sikuzungumzia shahada ya sheria. Nilisema "mwisho mtasema Chief Justice sio lazima awe amesomea sheria". Mtu unaweza kusomea sheria bila kupata shahada kama walivyofanya ma justices wa Marekani.

Bottom line ni kuwa hatuwezi kuepuka kuwa kuna kazi ambazo zinahitaji uelewa wa fani husika. Gavana wa BOT asiyejua lolote kuhusu masuala ya uchumi ni disaster in the making. Mimi sijui kama wa sasa ana hiyo exposure au la kwa hiyo siwezi kumhukumu.

Amandla...
 
Pote duniani MAGAVANA wengi wao ni Wachumi na wale wenye uelewa katika Sekta ya fedha. Tuwe wakweli Gavana wa BOT anatakiwa kuwa mchumi kama alivyokuwa nazo Marehemu Prof. Ndullu.
 
Ingawa unachosema ni kweli kuwa sio lazima awe ana shahada ya sheria lakini kuna caveats. K.m. anatakiwa apitishwe na Senate kabla ya kuwa confirmed. Huko jina lake linapita kwanza kwenye Senate Judiciary Committee ambayo imejaa wanasheria. Likitoka hapa anahojiwa na Senate nzima kuhusu uwezo wake na ufahamu wake wa mambo ya sheria. Vigingi hivi ni vigumu sana kwa mtu asie na shahada ya sheria na ambae hajawahi ku practise sheria kwa njia moja au nyingine. Sio bure kuwa Justices wengi wali Clerk kwa majustices kabla ya kuteuliwa.

Kwetu sisi Rais anaweza kumteua mtu yeyote anayempenda katika nafasi yetote ya uongozi bila kizuizi chechote. Ingekuwa Marekani Gavana wetu asingeona ndani maana Senators wangemhoji vilivyo.

Amandla...

Tukubali kwamba eneo la justices pengine ni exception, kwa sababu ya nature ya kazi yao!

Generally, ukiliangalia hili swala kwa marefu na mapana yake, nadhani utakubaliana nami kuwa kazi kubwa ya CEO ni kuongoza taasisi yake. CEO wa engineering company sio lazima yeye naye awe engineer. CEO ana wataalam wa kila aina at his or her disposal. Quality ya lazima kwa CEO ili ahesabike kuwa CEO mzuri ni yeye kuwa na uwezo mkubwa wa kiuongozi. Taasisi inahitaji visionary leadership. Kiongozi mzuri anajua jinsi ya kuunda team ya ushindi na kuiwezesha team hiyo kupata ushindi. Kumbuka, a CEO of an engineering company, ambaye yeye mwenyewe ni engineer mzuri sana lakini hana talanta ya uongozi, anaweza kuwa weakest link katika taasisi ambayo vinginevyo ilikuwa na kila sababu ya kufanikiwa!
 
Pote duniani MAGAVANA wengi wao ni Wachumi na wale wenye uelewa katika Sekta ya fedha. Tuwe wakweli Gavana wa BOT anatakiwa kuwa mchumi kama alivyokuwa nazo Marehemu Prof. Ndullu.

Ni kweli lakini sio lazima. BOT ni taasisi ambayo ina wataalam wazuri wa uchumi na maeneo mengine chungu nzima. At any time, kinachohitajika zaidi ni leadership. Hata kama governor angekuwa mchumi mzuri kiasi gani, kama hana talanta ya uongozi ni bure na anaweza kusababisha taasisi kushindwa vibaya sana kwenye mission yake!
 
Ikulu ya Dodoma ni ya hadhi ya chini sana, duh
1618605512835.png
 
Back
Top Bottom