Telewolth bin champion
JF-Expert Member
- Dec 11, 2018
- 2,386
- 6,473
Hao jamaa huwa wanachukua vijana mafukara wakiwa wadogo wanawapa elimu ya kuharibu utu wao yaani wanakuwa sawa na mnyama kifikra mpaka kiutu(kiroho) ndiomaana wakishakomaa ktk hayo matendo yao ya ugaidi hawaoni shida kuua mtu yeyote mpaka mtoto mdogo asiye na kosa, wanapandikizwa chuki mbaya sana ya kiimani na kuaminishwa mtu aliye nje ya imani yao ni shetani afai kuwepo dunian, kumbe masikin wanaenda kupambania maslahi ya wajanja fulaniKuna maswali huwa najiuliza:
- hivi hawa watu huwa na ndugu/jamaa
- hivi nchi ikiamua kuwa serious kabisa kutokomeza ugaidi inashindwa?
Hawa magaidi utawakuta baadhi Wanajiita wapigania uhuru, je mpigania uhuru yupi ataacha kupigana na mwanasiasa direct badala yake anakwenda kupambana na raia wasio na kosa? Kibaya zaidi mpaka kuharibu mali zisizowahusu.
Kuhusu kutokomezwa hawa inawezekana sana tu, pale serikali ikiguswa yaani wanasiasa matatizo yakiwagusa mbona utauona uwajibikaji wao, kama hao magaidi wangekuwa wanapambana na familia za wanasiasa kamwee usingeuona ugaidi maana ungetokomezwa haraka sana, wanaua raia wasiohusika wala kuwagusa wanasiasa ndiomaana hawapati uchungu wa kupambana nao,
pia kuna rushwa, maslahi na hiyo mikataba wanayosainishwa viongozi wetu ndipo wafadhiri wanawaamulia njia zipi za kupambana na gaidi, huku wakiwapandikiza watetezi wa ugaidi kwa majina ya mvuto wajiitao WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU,
Ukitaka kuona maajabu ya hawa watetezi wa haki za binadamu, ni pale raia wanapouawa vibaya na hao magaidi, lkn serikali inapojaribu kupambana nao either kuwaua adharani, utawaona hao wajinga wakisema wasiuawe bali washitakiwe kisheria baada ya uchunguzi, yaani upuuzi mtupu unapangiwa mpaka njia za kumuhukumu jambazi asiye na huruma kwa wengine.
Nigeria ni nchi mojawapo za kipuuzi ukiitoa Congo Drc, Sudan hizi nchi zote ni upuuzi unaofanyika