Nyerere ni Alikua ndiye Nabii au mshika Maono Wa Taifa hili. Hakuna Rais atakayelijenga taifa hili nje ya maono ya Mwalimu Nyerere.
Taifa hili Kwa uwiano wale kikabila ,kidini na Sasa kimuungano na rasilimali tulizopewa na Mungu kamwe haitawezekana kuliacha ligeuke kuwa Taifa la hovyo kama Kongo .
Kuna watu Wajinga na washenzi na makopo ya chooni ya kusafisha makalio ya wazungu walitumika kumhujumu Mwalimu Nyerere Kwa manufaa Yao .
Hata hivyo maono ya Mwalimu hayatakufa japo yanapigwa Vita sana na majizi kushirikiana na wageni.
Tuna wasomi Kwa mamiloni halafu tunakuwa na Rais au mawaziri wanaouza Vitu vyepesi kama Ardhi na Bandari !!! KAZI ni kupeana vyeo tu kikada za CCM na Sasa wamewafanikiwa kuwavuta na waroho Wa Mali kutoka Upinzani Kama Zito na Mbowe.
Nyerere ndiye Mbeba maono na alijenga falsafa ya utaifa ,utu na umoja ambayo wezi wanaitumia kuiba Badala ya kujenga nchi.
Kwa nini watanzania Hawa Hawa waweze kuendesha Kampuni ya Airtel lakini washindwe TTCL.
MTU AKITAKA kuwaadhibu wanaotuhujumi Anaitwa dikteta. Hatuko siriaz mpaka Siku wenye nchi halisi ambao ni wengi wanaoumizwa leo watakapoamua kusema basi na kuwatoa madalali Wa kuuza nchi.
Kama watanzania wameshindwa kweli kusimamia rasilimali na mashirika Yote ya umma Kwa nini tusianzie na mismamizi Wa Ikulu na wizara ZAKE.?
Hivi inaingia akilini kweli kuwa Wasomi Wote wameshindwa kuendesha Idara walizopewa lakini Rais na Serikali yake na Bunge lake na Majeshi yake na mahakama zake ziwe zinafanya Vizuri wakati zinaongozwa na watanzania wenyewe Kwa asilimia mia moja?
Basi tuuze na kubinafsisha Ikulu, Bunge, mahakama, Majeshi Ili tuletewe Teknolojia ya kisasa kama kule Uarabuni na China.
Kwa nini tunakwepa ukweli kuwa Hao walioendelea wameendekea baada ya kuwa na SHERIA Kali na Hata kuwaua wale wote waliotumia nafasi zao kuiba Mali za umma?
Hiví Hata wawekezaji wawekeze mpaka kwanye Vijiji na miji Kila MAHALI kama hakuna watu waadilifu ni muwekezaji Gani ataacha kuiba na kuwahonga wale tuliowapa nafasi ya kutuwakilisha !!
Leo hili almasi ,dhahabu, Vito vya thamani, wanyama ,madawa yanaingizwa na kutoka Kila sehemu Kwa kushirikiana na Wale tuliowapa dhamana Kwa sababu TU hakuna anayewasemesha Kwa ukali na kuwafunga au kuwanyonga watu Hao . Nani asiyetaka Mali nyingi Kwa namna yoyote kama SIO Imani na Tabia za MTU Binafsi na malezi yake. ?
Kwa nini tuwaache watumishi Wa umma wajiongoze Kwa hulka zao Binafsi .? Yaani wakiamua kuiba waibe na wakiamua kuacha waache na asiyeona cha kuiba shauri yake na asiyetaka kuiba ni Mjinga Hana akili na atachekwa na kuzomewa na Hata kuuawa? Kila MTU Kwa urefu Wa Kamba yake.
Tumejenga mfumo Wa waovu kuwadhibiti watu waadilifu na Hata kuwaua na kuwatoa kwenye mifumo ya kiutawala na Sasa wamefanikiwa kuiteka mihimili Yote kuanzia Bungeni mpaka mahakama. Muovu kumuua MTU mwadilifu ni haraka sana Kama hajadhibitiwa lakini muovu akidhibitiwa anaogopa mana muovu anaogopa kufa na kuacha starehe za Dunia.
Nyerere alifanikiwa kutuletea uhuru na kujenga umoja chini ya makabila Mengi na Dini Tofauti lakini miaka 60 baadae wale aliowashinda wamerudi Kwa Gia ile ile ya Dini,Ukanda na Sasa wanajiita wawekezaji Badala ya wakoloni. Badala ya Watu kujengewa uwezo Wa kujiajiria katika rasilimali nyingi tulizo nazo Watu wanaletewa wakoloni Wa kuja kuwafanya watanzania watumwa kwenye nchi iliyopita uhuru miaka 62 iliyopita.
Watawala hawana muda Wa kufikiri zaidi ya kushawishiwa Kwa mipango isiyoweza kufanikiwa kwenye nchi isiyo na sharia Kali.
Kiongozi Badala ya kukemea wavunja Sheria anawaliwaza . Kiongozi anavunja Sheria Mfano za usalama Barabarani akikamatwa na polisi anakuwa mbishi na Kutumia majukwaa ya kisiasa kuwashambulia Trafiki Badala ya kujiuliza kuwa Kwa Nini amekamatwa na Sasa Kwa nini anataka achekewe na kusamehewa . Je,Wote wakivinja Sheria inakuaje?
Leo hii akatokea Mwekezaji Wa usalama Barabarani Toka Dubai au China atakimbilia hiko na atapata pesa nyingi sana mana anajua kuwa watanzania wanawaheshimu Wageni na kuwanyenyekea Hata kama wanakosa.