Kikwete alishindwa uongozi kama Rais na sasa ameshindwa tena kama Mstaafu

Kikwete alishindwa uongozi kama Rais na sasa ameshindwa tena kama Mstaafu

Uzi wako unahisia nyingi,Mzee Kikwete hana baya hakuwa na husda,chuki wala visasi.

mimi ninachojua utawala wa Kikwete alifungua sana nchi hasa kwenye kukaribisha wawekezaji ajira zilikua nyingi mzunguko wa pesa wa uhakika,watu waliuza na kununua biashara zilifanyika.

watu walikula bata wakasaza,siku za weekend majiji kama ya Dar,Mwanza na Arusha yalikua ya moto ni full hekaheka.
We mtoto wa juzi kama bata waulize vijana wa enzi za Mzee ruksa watakupa majibu, na haijawahi kutokea hela kufunguka nchi hii kuliko awamu ya Mwinyi. Ndiyo hadi wa vipato vya kati walikuwa na jeuri ya kujenga katikati ya jiji
 
We mtoto wa juzi kama bata waulize vijana wa enzi za Mzee ruksa watakupa majibu, na haijawahi kutokea hela kufunguka nchi hii kuliko awamu ya Mwinyi. Ndiyo hadi wa vipato vya kati walikuwa na jeuri ya kujenga katikati ya jiji
Nyie wazee wa Laizoni,wazee wa Lang'ata,Mbowe club,kipindi chenu pia amkupoa.
kwa kifupi Mwinyi na Kikwete walifanya vitu fulani vya tofauti ukilinganisha na tawala za wengine.
 
Wakati wa Utawala wake...

Huyu bwana ana Bahati mbaya sana. Haya ni Matokeo ya kuforce uongozi wakati hauna karama hizo, kuongoza watu siyo jambo jepesi inahitaji maono na busara hasa unapokuwa kwenye nafasi nyeti kama ya uraisi.

Enzi za utawala wake nchi ilikuwa ya hovyo tena hovyo kupitiliza kiufupi nchi aliiikabizi kwa mabwenyenye wachache. 2005 alipita wa kura nyingi sana 88%, lakini Awamu ya Pili pamoja na kuiba kura aliambulia kama sikosei ni 59% watu walikuwa wamechoka mithili ya harufu mbaya.

Huyu mwamba alipuyanga sana. Hakuna mtu alitaka hata kumsikia. Bila uongozi mbovu wa Kikwete Magufuli asingekuwa Raisi, Magufuli alikuja kunusuru nchi isiende kwa Wapinzani.


Kwa Nini kashindwa kama Mstaafu

Kwa utamaduni wa Kitanzania Raisi mstaafu ni Nguzo muhimu sana hasa pale taifa linapotaka kukosa mwelekeo, lakini pia anajukumu kuwaelekeza njia bora za kupita aliowaacha.

Nafikiri mnakumbuka ni namna gani Nyerere alivyokuwa macho hata baada ya kustaafu, alikuwa akisimama kusema jambo taarifa lazima litulie.

Vile vile Mkapa alikuwa akisimama kidete pale mambo yalivyokuwa yanaenda kombo hasa kipindi cha uchaguzi, sauti yake iliheshimika sana.

Leo hii tuna Kikwete sijui hata anafanya hini, suala lililoniuzi ni hili la Sukuma na Msoga gang kutokalipiwa hadharani tena kwa ukali; limeleta mgawanyiko makubwa sana. Mstaafu yupo anaongea kwa kujificha ficha, ovyo kabisa.

Kikwete anazidi kushindwa kwasababu hata ushauri anaotoa kwa Rais Samia unaonekana ni wa ovyo kwasababu unapingwa kila kona ndani na nje ya nchi. Mbaya zaidi hataki kutoka hadharani kuweka mambo sawa kama Mstaafu.

Kiufupi nafasi ya ustaafu haintendei haki, hii inatokana na kutokuaminika na watu wengi maana uongozi wake ulikuwa ni fedheha.

Namshauri Kikwete awe Mzalendo, kashazeeka atapendwa na wengi, aache kumpoteza Rais Samia na kuyumbisha Serikali.
Asili ya watu weusi walio wengi ni shida, utumwa na ukatili ndio maana akitokea mtu kama Kikwete au Samia hawaridhiki nawo. Asilimia 90 ya maombi yao kwa wengine ni kuwaombea wapate shida tu. Dar es Salaam unayoiona leo ujenzi wa majengo binafsi na ya umma au kampuni ni matokeo ya Kikwete. Hizo Bata za Sinza na Tabata ni kwasababu ya sera za Jakaya. Usione vyaelea.
 
Binafsi namkubali sana kikwete ni miongoni mwa Marais waliofanya watanzania wajikwamue kiuchumi, ajira zilikuwa nje nje, mzunguko wa fedha ulikuwa mkubwa pia aliruhusu watu wawe huru kumkosoa

Nikiwaga free hua naangalia speeches zake you tube mzee alikua na karama ya kuongea na watu wote! Anaweza akaelezea jambo gumu katika namna nyepesi na wote mkamuelewa vzr!
Nasikia aliwahi kuulizwa kwanini Tanzania ni masikini akashindwa kuelezea.
 
Huyu Mzee mwacheni apumzike!yaani katulea wengi sana!!

Unafikiri bila kikwete kuongeza pesa bodi ya mikopo ningesoma chuo kikuu Mimi!!?tena Bachelor of science!!

Tunajua ana mapungufu Lakini hatuwezi sahau maisha Bora KWA KILA mtanzania!huwezi leta maisha Bora bila kuachia matajiri waachie pesa mtaani ziwafikie hata masikini!!

HADI mkapa anaondoka BADO maisha yalikua magum SANA KWA watz! watumishi wa umma n.k SASA ALIPOKUJA alikuja kuleta unafuu!!

Hayo mengine ni mapungufu ya ki binadamu tu ambayo KILA Rais anakua nayo KILA awamu!!

Mungu ambariki pia ampe moyo wa kuachilia utawala na uongozi wa nchi !sio lazima watu wake ndio washike hatamu !watz tupo wengi!!!


Mungu IBARIKI Tanzania nchi yetu niipendayo SANA
 
Duuh hivi guts za kumkosoa Amiri Jeshi mstaafu mnatoaga wapi jamani
huo uoga hatutaki hili taifa ni letu sote tunahtaji ujasiri taifa linahtaji watu wenye uwezo wa kuhoji chochote kile paspo kuvunja sheriaa na ikiwezekana kuvunja sheria kama utawala ni mbovu ili kuhimiza maendeleo ktk nchi yetu....kwa lazima
 
M

mi nataka akae kwa kutulia, awamu yake ilishapita aache uswahili
Anavyozurura duniani kwa kutumia kodi zetu zinamtosha!

Screenshot_20230618_092348_Chrome.jpg
 
utawala wa Magufuli ulijaza Wakristo wizara zote waislamu mbona walipiga kimya, wakristo wakiwa wengi kwenye teuzi waislam wanavumilia awalalamiki, ila wakiwa waislam wengi inakua kelele,why?
Mama si ndiyo anafukia mashimo sasa? Katika teuzi ya watu kumi nane ni vibaraghashia na 2 Wagalatia.

Tutulie!
 
Back
Top Bottom