Mkuu mimi nimezaliwa miaka ya 80, miaka ya 90 hata kukuta TV kwenye Majumba ya watu ilikua ni Anasa, ila wakati wa mkwere sio tu karibia kila Nyumba unakuta TV na vitu vyengine vya Anasa bali ni vya Bei ghali zaidi. Zamani TV ziliuzwa bei rahisi ila siku hizi watu wengi wananunua TV za Malaki.
Kipindi chake biashara ilishamiri Tukaanza kuona kukua kwa loose Cargo wa Tanzania wenyewe wakawa wanaenda Dubai na China kuleta mizigo Makabila yanayojielewa Yakaanza kukua kiuchumi.
TBC ambayo ilikua ikipatikana Dar na miji mikubwa Ikasambazwa Tanzania Nzima, sababu ya Tido Mhando, Tido alikuwa poached toka BBC akaletwa Nyumbani, TBC ikaanza kuonesha ligi ya Uingereza na vipindi kama Ze comedy, wakati huu TV ya Taifa Ikawa Inaangalizika.
Muulize Mhenga yoyote Zamani ilikua kumaliza La saba ni big deal, ukifaulu ukipangiwa sekondari Boarding kijiji kizima lazima wajue, Kikwete Akajaza Mashule Ya kata kibao na Vyuo vikaongezeka maradufu mpaka kufikia Stage degree imekua kama la 7
Mitandao ya Simu ikaletwa kwa Kasi, Internet ikaanza kupatikana kwa kila mwananchi, vifurushi vikashuka bei, akawaleta hadi Halotel ambao walisambaza internet hadi vijijini,
Kutokana na charisma yake jamaa alifanikiwa kuwashawishi watu wengi kuja kuwekeza Tanzania kama Dangote,
View attachment 2661248
Kifupi jamaa alifungua nchi sana.