- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na machapisho yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii yenye nukuu mbalimbali zinazodaiwa kuwa zimetolewa na viongozi wa nchini Tanzania.Moja ya kurasa hizo ni mjadala tv na siasa za kweli ambazo huchapisha maudhui hayo mara kwa mara
- Tunachokijua
- Kume Kuwepo na machapisho yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii yenye nukuu mbalimbali zinazodaiwa kuwa zimetolewa na viongozi wa nchini Tanzania.Moja ya kurasa hizo ni mjadala tv na siasa za kweli ambazo huchapisha maudhui hayo mara kwa mara
Miongoni mwa nukuu hizo ni kauli inayodaiwa kusema, “Chadema haina viongozi wenye utimamu,” huku nukuu nyingine ikidaiwa kutoka kwa Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ikisema, “Kikwete aomba Tundu Lissu kuachiwa ndani ya wiki hii maana Tanzania tuna amani.”
Nukuu hizo zimechapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kusambazwa na baadhi ya watumiaji, licha ya kutokuwa na ushahidi unaothibitisha kuwa zilitolewa na viongozi hao.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu katika hotuba, kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za viongozi husika pamoja na mahojiano yao na vyombo mbalimbali vya habari, haikubainika sehemu yoyote ambayo viongozi hao walitoa nukuu hizo.
Sambamba na hilo, machapisho hayo yametumia vichwa vya habari vinavyopotosha uhalisia wa taarifa, huku yakiambatanisha viungo vya YouTube vinavyolenga kuvutia watazamaji na kuongeza idadi ya watu wanaotembelea maudhui yao.
Aidha, kurasa hizo zimekuwa zikichapisha mara kwa mara maudhui yenye taarifa za kupotosha, hali inayodhihirisha kuwa lengo lao ni kuvutia watazamaji kupitia maudhui yenye vichwa vya habari vya kushtua au vinavyoweza kuibua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.