Uchaguzi wa 2020 nilifika mapema saa tatu na nusu kituoni kupiga kura, nilishangazwa na uwepo wa wapigakura wachache kituoni lakini maboksi ya kupigia kura karibu yote yalikuwa yamajaa karatasi za kura.
Nilimuuliza askari aliyekuwepo pale lindoni, mbona kama fréquence ya wapigakura kama ndogo? Jamaa akajibu kwa mkato tu, watu wameamka mapema wamekuja kupiga kura, wamemaliza kazi hiyo wanaendelea na shughuli zao....
Matokeo yalipotoka ilokuwa dhahiri kuwa kulikuwa na mpango wa kuiba kura kwa kuipendelea CCM dhidi ya upinzani, kwa jinsi Rais wakati huo John Pombe Magufuli alivyofanya kazi inayopigiwa mifano hadi siku ya leo ....Sikuona kabisa sababu ya CCM na vyombo vya Dola kupanga njama za ushindi wa kishindo.
Kikwete anashangaa na kujiaminisha kuwa mambo yako sawa... Kama kweli hivyo ndivyo basi huo uchaguzi uendelee tu ili tupate matokeo yatakayoonyesha nani yuko sahihi kati ya wanaotaka Reforms zifanyike tena kabla ya uchaguzi na wale wanaodai reforms zimeishafanyika.