Kikwete ni mmoja ya Marais ambao miaka Ijayo watoto wetu watatushangaa sana kuwa ilikuaje....

Kikwete ni mmoja ya Marais ambao miaka Ijayo watoto wetu watatushangaa sana kuwa ilikuaje....

Yaani akatumia pesa za wananchi maskini kukusanya maoni ya katiba. Yakapatikana.

Akatumia mabilioni ya pesa za Maskini kuliitisha Bunge la Katiba....likakaa...wakalipana mapesa mengi.

Kisha akavuruga mchakato. Akakaa pembeni akicheka mchezo aliofanya....watanzania ni wasahaulifu sana.

Leo wameshasahau kabisa ufisadi huo mkubwa wa Kikwete. Wamesahau kabisa.

Huwa nikikumbuka naumia sana akilini. Kwa nini awatendee hivi watanzania hawa maskini.

Leo kuna watu wengine tena wanaenda kulipwa kwa ajili ya Tume ya Uchaguzi.... Wanalipa pesa hizi hizi za watanzania maskini.
Tusaidieni wenye data, tujue kiasi kilichotumika kwa hayo mambo mawili..."Figures always zinaongea zaidi kuliko maneno"
 
Yaani akatumia pesa za wananchi maskini kukusanya maoni ya katiba. Yakapatikana.

Akatumia mabilioni ya pesa za Maskini kuliitisha Bunge la Katiba....likakaa...wakalipana mapesa mengi.

Kisha akavuruga mchakato. Akakaa pembeni akicheka mchezo aliofanya....watanzania ni wasahaulifu sana.

Leo wameshasahau kabisa ufisadi huo mkubwa wa Kikwete. Wamesahau kabisa.

Huwa nikikumbuka naumia sana akilini. Kwa nini awatendee hivi watanzania hawa maskini.

Leo kuna watu wengine tena wanaenda kulipwa kwa ajili ya Tume ya Uchaguzi.... Wanalipa pesa hizi hizi za watanzania maskini.
On top of that Maza akawa Makamu Spika wa Bunge ..... akalamba posho na kujipatia umaarufu wa kuwa Makamu na baadaye Rais. Leo hii hataki kuisikia wala kuizungumzia hiyo katiba aliyoshiriki kuipitisha .... Kaja na ubadhirifu mbadala wa Kamati ya demokrasia (mwenyewe anadai kuwa ni shamba lake) ambayo itadumu mpaka 2029 ..... Seriously!!
 
Wakati wa Magu watu wakamkumbuka JK na kusema ni bora mara 1000!!

Magu hayupo imekuwa tena kinyume chake ha 😄
Pitia michango yangu ya nyuma utaelewa ninacho kisema Magu alikiwa best kwangu mimi hapana mfano
Ila ndo ivo tena wa tz tunasahau mapema enzi za JK ufisadi na rushwa, kukosekana kwa uwajibikaji watumishibwa uma, wanafunzi kukosa madarasa na kusoma wameka chini, wanyamapori kubebwa kwenye ma-box kwenda ulaya na asia n.k Magu vyote alizibiti kwa muda machache sana
 
Ni Rais mbovu kabisa kuwahi kutokea Tanzania tokea tupate Uhuru. Cha kusikitisha kuna Mazuzu wengi Wanamkumbali na walikuwa Wakimpenda huyu Mswahili ambaye wana CCM walimpitisha mwaka 2005.

sasa kama nchi inaruhusu mpaka zuzu kuwa Rais basi hilo Taifa wote watakuwa mazuzu wakiwemo Marais wote walioshindwa kujenga mfumo utakaozuia mazuzu kuwa marais...

Katika hili hata wewe ni zuzu maana uliruhusu kutawaliwa na zuzu 10yrs...usingekuwa zuzu ungezuia hata kwa kujitoa mhanga na kumuua zuzu...
 
Hongera mleta Mada ur clever!
Huenda topic hii ika mwamsha Mzee JK, atoe ushauri Sahihi! Kwa maslahi ya Taifa letu, waugwana wote hawapendi Katiba yetu isiyo na meno mdhibiti kiongozi na fairness kwa Zanzibar.

Moja ya sababu kuu za kukwamishwa ule mchakato ni yale mabadiliko ya muundo wa Muungano
 
Watoto wetu watatushangaa sana ilikuwaje Tanzania tuliongozwa na mtu mwenye sonona Magufuli.
 
Nashangaa tukiwalaumu akina Chief mangungo wa msovero alipopigwa changa la macho na aliyekuwa kijana wa kijarumani bwana Karl Peters...Nashangaa Sana tu
 
Hivi Salma na Riz1 Dodoma huwa wanaishi Hotel? Oooh sorry Riz 1 ni Waziri kweli atakuwa anaishi kwenye makazi yasiyo salama ya Tundu Lissu( area D)

Haiwezekanai Kikwete asiwe na Nyumba yake mwenyewe pale Dodoma. Mkewe anakaa kwenye nyumba yao akiwa bungeni!
 
Na hii ndio fact ambayo watu wengi hawaijui
Wananchi wa Tanzania wameingia makubaliano yasiyo rasmi kuwaamini wanasiasa huku wao wakijiweka pembeni.
Kwamba wanasiasa wao wafanye wanayoweza kufanya... wananchi kazi yao ni kuishi na kutekeleza!
 
Hapana rasimu ilishapitishwa shida ni serikali imeshindwa kumalizia mchakato uliobakia.
Kama ni serikali iliyoshindwa! Basi ni serikali ya Jiwe, maana ndiyo iliyofuata baada ya mchakato wa kwanza kukwama.
 
Back
Top Bottom